Labda Kuna jambo hujaligundua kati ya hii kauli yangu "Kulipwa" huendana na "kutumika"
Yeyote anayelipwa basi ujue Kila anachokifanya ni kwa niaba ya maslahi ya anayelipwa...
Kama mwanaharakati analipwa basi ujue hatopambania maslahi ya wananchi Bali ni ya wale wanaomlipa. Mwanaharakati yeyote anayelipwa hayupo kwa ajili ya maslahi ya wananchi Bali ni ya wachache wanaomfadhiri
Uko sahihi na nakuelewa kwa hilo...
Lakini tukiwapima kati ya mwanaharakati anayelipwa ili kuhubiri haki za binaadam
na
Mwanasiasa ambaye ni kibaraka wa mafisadi...
Utagundua angalau mwanaharakati ana athari ndogo hasi kuliko mwanasiasa...
Maria Sarungi analipwa na Ford International, huenda ni kweli lakini harakati za Maria zikishinda kipi kitatokea?
1. Tutakua na katiba mpya
2. Tutakua na tume huru ya uchaguzi
3. Tutakua na utawala wa sheria
Upande mwingine ukishinda
1. Tutaendelea kuibiwa rasilimali za nchi na hakuna sheria za kumbana anayeiba
2. Tutaendelea kushuhudia mauwaji na utekaji bila kujua mwisho wake
Kwahiyo mimi naona ni bora huyu anayelipwa kukutetea kuliko huyu anayekukandamiza.