Maridhiano ya shinikizo yana faida gani?

Manyanza

Platinum Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
22,269
Reaction score
58,563
Swali ambalo Watanzania wengi wanapaswa kujiuliza ni hili:

Maridhiano yanayoshinikizwa na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi yana faida gani ikiwa hayatajibu hoja za msingi kuhusu haki, uhuru wa kisiasa, utawala wa sheria na uaminifu wa mifumo ya uchaguzi?

Maridhiano sio lengo lenyewe; Maridhiano ni matokeo ya mchakato unaojengwa juu ya ukweli, haki na uwajibikaji. Pale ambapo sababu za mgogoro hazijashughulikiwa, maridhiano hubaki kuwa kauli ya kisiasa badala ya suluhisho la kudumu.

Wananchi wanahitaji kuona taasisi zinazotenda kwa haki, sheria zinazotumika kwa usawa, na mazingira ya kisiasa yanayowapa wote nafasi ya kushiriki bila hofu wala upendeleo. Bila misingi hiyo, ni vigumu kujenga imani kwamba maridhiano yatazaa matokeo yenye manufaa kwa taifa.

Ndiyo maana hoja muhimu sio kuuliza "kwa nini hamkubali maridhiano?" Bali ni kuuliza:

Maridhiano ya aina gani? Yatajenga haki gani? Yatalinda uhuru gani? Yataimarisha utawala wa sheria kwa namna gani? Na yatarejesha vipi imani ya wananchi katika mifumo ya uchaguzi?

Maswali hayo yakikosa majibu ya wazi, maridhiano yanaweza kuonekana kama njia ya kutuliza mjadala wa kisiasa badala ya kutatua chanzo cha migogoro.

Amani ya kweli haijengwi kwa shinikizo. Maridhiano ya kweli hayajengwi kwa kauli pekee. Taifa lenye umoja wa kudumu hujengwa kwa ukweli, haki, uwajibikaji na kuheshimu utawala wa sheria. Hapo ndipo maridhiano hupata maana halisi na kukubalika na wananchi.
 
Imagine una dispute ya mgawanyo wa ardhi ya shamba na ndugu yako. Unamuambia mtatue huo mgogoro kabla ya msimu wa kilimo. Yeye anakataa; anakuambia tutashughulikia huu mgogoro baada ya kulima.

Je, dispute resolution approach ya style hiyo ina lengo la kutatua mgogoro au kuhalalisha mgawanyo wa ardhi kulingana na mashamba yalivyolimwa? Mazafakas wa CCM wanadhani Watanzania wapumbavu!
 
VITA ya wanasiasa imelenga mkate ndo maana baada ya watu kuuliwa , kuuwawa , kuumiza , kufungwa n.k

Wao wanatafutana privately wanaongea na kukubaliana huku familia zao zikiwa privilege n.k

Ukiona hawajakubaliana issues Fulani ujue ni mkate tu.

Niliona Juzi Dereva wa Heche Guest alivyokuwa amelala , Guest ya chini sana .

Kitu ambacho MTU kama Mnyika au Heche hawezi.

Deep down , hawaangalii usalama na ustawi wa watu wao wakaribu je ndo waje waangalie ustawi wa watu wengine.
 
Ina maana CCM walikuwa hawasikii kelele za upinzani kabla ya uchaguzi?
Yaani wajipe ushindi kimabavu ndio waseme maridhiano.
Kwanini yasingefanyika kabla ya uchaguzi?
 
VITA ya wanasiasa imelenga mkate ndo maana baada ya watu kuuliwa , kuuwawa , kuumiza , kufungwa n.k

Wao wanatafutana privately wanaongea na kukubaliana huku familia zao zikiwa privilege n.k

Ukiona hawajakubaliana issues Fulani ujue ni mkate tu.

Niliona Juzi Dereva wa Heche Guest alivyokuwa amelala , Guest ya chini sana .

Kitu ambacho MTU kama Mnyika au Heche hawezi.

Deep down , hawaangalii usalama na ustawi wa watu wao wakaribu je ndo waje waangalie ustawi wa watu wengine.
Upo sahihi kabisa Hayaland, nimeshuhudia enzi za Kolona mwanasiasa akilazwa Agakhan mwezi mzima almost milioni 40 ikitumika na kutoka salama,huku dereva wake akijifikiza na kupoteza maisha

Wanasiasa watabaki kuwa wanasiasa
 
Yule dereva amelishwa sumu na huo ndio ukweli na siku zote ukitaka kugundua hilo ni kwamba serikali piga ua haikubaligi Independent Autopsy to be performed on the decreased.

Wanalazimisha wenyewe ndio wafanye na hii tuliiona hata kwa marehemu Zakayo Wangwe.
 
Back
Top Bottom