Maridhiano yalileta amani kiasi fulani, sasa mambo yamebadilika. Hofu na Uhasama vinatamalaki

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
16,419
Reaction score
26,594




Niliandika majuzi kuwa upepo wa kisiasa hausomeki kwa sasa. Wengi tulipata amani wapinzani walipoonyesha ushirikiano na chama tawala na serikali yake.

Sasa naona upepo umebadilika kabisa, uhasama na hofu za kisiasa zimerudi kwa kasi. Mzizi wa fitna umetembea na wasi wasi umeanza kutanda.

Wazee wa busara okoeni jahazi na mustakabali wa nchi yetu pendwa, Tanzania.
 
Wakatwaji kamwe hamwez simama wima kuna namna lazima mshike ukuta.
 
..maridhiano yalikuwa danganya toto tu, hakukuwa na nia ya dhati kwa Samia kuleta mabadiliko ya kweli. Hata wewe umesikia Samia akitamba kwamba sheria za kikatili bado zipo.
 
Samia amechezea nafasi muhimu, asije akamlilia mtu
 
MODS mmebadili kichwa cha habari sasa mada imekosa mvuto.
Msisitizo ulikuwa nanani kaingiza mzizi wa fitna.
 
Kwanini ccm wanakuwa wanafique na vigeugeu kwenye hayo maridhiano?
Kwanini wanaogopa sana maandamano?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…