Mbona kuna majimbo WAPINZANI walishinda? Yaani CCM ni wezi kiasi hicho ila kuna sehemu wanaamua kuachia kidogo? Mie sidhani kama hali ni mbaya kiasi hicho. Kama watu wote tukisimama wima na kwenda kupiga kura kwa wingi na kusimamia kura wakati wa uchaguzi kuwa hakiibwi kitu, basi amini kwamba hawataiba. Na hata wakifanya hivyo basi si kwa asilimia kubwa sana.
CHDADEMA kama chama kinaweza kuweka karibu kila sehemu mtu mwenye computer na Internet LIVE wakati wanahesabu. Na wakimaliza, matokea yanatangazwa palepale. Hata kama si LIVE, watu wanaweza kuwa wanarekodi kwenye simu/Camera zao na kuwa na kumbukumbu.
Wakati wa UCHAGUZI nchi kama za Czech, Bulgaria, Rumunia, Hungury nk Wakoministi walikuwa wametawala kila sehemu na kuweka watu wao. Maadamu watu walikuwa wamechoka, WALIBANANA hadi kikaeleweka.
Inasikitika sisi kukata tamaa mapema namna hiyo.
Moto wenu VIJANA uwe "SLAA FOR PRESIDENT 2010"
Mengine haya wala MSITISHWE kihivyo. Mbona Slaa alishinda? Zitto, Wangwe, ....... na wengine wengi? CCM kweli iliruhusu? Kuiba kura imekuwa ni LUGHA inayotumika na UPINZANI mara wakishindwa kwa uzembe wao. Kama sasa hivi tukiwa NGANGARI na tulivalie njuga hili swala, TUTASHINDA.
JENDA KAJIANDIKISHE na siku ikifika, wewe, familia yako, Wapwa na Washikaji mnamchagua SLAA.
Ila kama kwako wewe, kuwepo kwa CCM unafaidi, basi hapo hakuna cha kujadili. Labda na mie ningelikuwa mtoto wa FISADI/Kigogo wa CCM au mtu wa karibu na Kikwete, basi ningelipinga Usiku na Mchana maana imesemwa "Aisifiaye Mvua........."
Ndugu yangu inakatisha tamaa sana,
Kwa jinsi navyoona mwenendo wa chaguzi zetu upinzani kushinda kiti cha uraisi ni kama ndoto za alinacha. Kura zinavyoibiwa, mawakala wa vyama wanavyogeuka mamluki wa CCM na vitu kama hivi huwa inanikatisha tamaa sana. Unaweza kupiga kura kwa Slaa kumbe kura yako inahesabiwa kwa JK na kuzidi kumwongezea pasenti kwenye ushindi wake. Sasa skuli meti, si ni heri nisipige kura ili nipunguze pasenti ya ushindi wa JK?
Naungana na wengine, Slaa kugombea urais wapinzani wamepunguza sauti yao bungeni. Na hili ni kosa kubwa sana. Kwa gharama yoyote ile JK atashinda. Iwe kihalali au kilanguzi au hata kiubabe.