Mleta maada huwezi kueleweka na wengi. Ndiyo sababu unaona comment kama "ndefu sana hii". Sababu ni nyingi tu.
1. Ngozi nyeusi ni ngumu kusoma maandiko marefu hata yawe muhimu.
2. Kwa sehemu kubwa fanbase imekuwa distorted. Ni ngumu kutofautisha baina ya Pogba fan na United fan hata kwa msaada wa venn diagram. Utakuta mtu ni fan wa Barca/Chelsea. Hapohapo anamhusudu Pogba.
Hapo hata Pogba aoneshe conduct mbovu kiasi gani, such fan hawezi ona ubaya since yeye yuko concerned na kanzu, vidali, na pogpass. Atakayeumia hapo ni yule real fan wa United.
Nakumbuka enzi zile kipenzi cha mashabiki David Beckham alipoonesha dharau fans walimuunga mkono babu kumuuza japo ilikuwa ngumu kumeza. Aliyemhusudu kupita kiasi ilimbidi kuanzisha mchepuko kwa Real Madrid iloyokuwa imetoka kututoa UCL msimu mmoja nyuma. Timu kwanza.
3. Sehemu kubwa ya fanbase haijui "mpira". Hawawezi analyse onpitch football. Hivyo hata mchezaji anayecheza kwa ajili yake uwanjani hana shida ilimradi tu ana-drible na kupiga watu kanzu. Hawajui umuhimu wa discipline ya mchezaji ndani na nje ya uwanja.