Marioo (TotoBad) amekuwa msanii lulu bongo kwa sasa

Idrissou02

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2018
Posts
354
Reaction score
656
Nimepata wasaa leo nikaskiliza album mpya ya barnaba classic. Ni album nzuri kwakweli lakini nilivyofika kwny track aliyomshirisha Marioo, kuna kitu tofauti kabisa nikagundua kwny ngoma hiyo. Yule kijana sasa hivi ni kana kwamba yupo ndani ya beat anaflow nalo kama mawimbi kwny bahari ,anafanya uone mziki kwny taswira nyingine kabisa.

Nikalinganisha na ngoma zake kadhaa nilizoweza zisikiliza ndani ya mwaka huu, nikasema kweli tumewakariri wakina Mondi, Kiba, Konde na wengine wengi ila bila shaka huyu kijana ana kipaji cha kipekee mno, ameweza kuupeleka mziki wake level nyingine kabisa.

Wadau wa muziki mzuri tu ndo tukutane kwny thread hii, sio wale wa kuja kuanza kuniita mi chawa. Appreciate good things and people will appreciate yours one day.
 
Wengi sana ni wakali wa kuimba Bongo hii, lakini kubali kataa Mondi ndiye dereva wa gemu la Bongo Flava wakati huu!!

Ili msanii afanikiwe kwa sasa Tanzania ni lazima ahusishwe na Mondi, yaani ajitie kabiif flani hivi na Mondi ndio wa Tanzania watamzingatia!!

Si kweli kuwa Kiba, Harmo au Vanny wanajua sana kazi kuliko Jux au Mario na wengineo bali wao wanapita na nyota ya Mondi kwenye mziki wao na kazi zao kwa ujumla!!

Ukilikataa hili unabaki kuwa mwanamuziki wa kawaida tu sawa na Aslay au Baraka da prince!!!
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣we ndo chawa sasa.kila la kheri.
 
Hamna kitu anavimba tu ninavyomuona dogo anapenda kuiga swaga za msanii fulani namba moja hapa Tz.
 
Marioo anawanyoosha aisee kinachomtofautisha ana original sound yan ka evolve kwa kujitafuta sio kuiga sound za wengine kama wengi wao, akiimba amapiano anaweka signature yake ila wakubwa wakiimba amapiano utahisi kisauz kinatafsiriwa tu na kiswahili 😁 akiendelea hivi atakua marketable kuliko wengine, alipo tu hapo ni threat sana... even zeros recognize heroes! Kwahyo wanajua anawanyoosha!
 
Wengi sana ni wakali wa kuimba Bongo hii, lakini kubali kataa Mondi ndiye dereva wa gemu la Bongo Flava wakati huu!!

Ili msanii afanikiwe kwa sasa Tanzania ni lazima ahusishwe na Mondi, yaani ajitie kabiif flani hivi na Mondi ndio wa Tanzania watamzingatia!!

Si kweli kuwa Kiba, Harmo au Vanny wanajua sana kazi kuliko Jux au Mario na wengineo bali wao wanapita na nyota ya Mondi kwenye mziki wao na kazi zao kwa ujumla!!

Ukilikataa hili unabaki kuwa mwanamuziki wa kawaida tu sawa na Aslay au Baraka da prince!!!
Rudisha ada shuleni
 
Back
Top Bottom