Public Enemy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2011
- 3,029
- 3,520
Huu Mzigo huwa Siusahau Matukio.... Halafu Kuna
Predator
Terminator Zote 1,2 na 3
No retreat No Surrender
John Rambo
Drunken Master ya Jackie Chan
Escape from Sobibor
Sarafina
Neria akiweko Mwanamuziki Nguli Oliver Mutukudzi
Hizo na Nyinginezo mkimiliki nyumbani nyie washua haswa....
Kwenye burudani
Koffi Olomide -Quarter Latin na Loi
Hapa wakitoka Vijana waliokuja Itikisa Afrika baadae kama Fally Ipupa
Wenge Musica BC BG 4*4- Pentagone(1996)
Humu ndimo walitoka Wanamuziki wakubwa baadae kama Noel Ngiama Makanda almaarufu kama Werrason, Didier Masela, Adolphe Dominguez, baadae Akajiunga J.B Mpiana na Ferre Gola. Baada ya Kutengana Baadae ndipo kukawa na Wenge BCBG ya J.B Mpiana na Wenge Musica Maison Mere ya Werrason, Adolphe Dominguez na Didier Masela.
Madilu System jina la album nimesahau
Wenge El Paris jina la album nimesahau, hii ndio Ilikua kama Part B ya Wenge Musica BC BG ambapo Ilikua huko Jijini Paris, Ikiundwa na Aime Buanga ambaye alienda Ulaya kwa sababu za Kimasomo na wakafanikiwa kutia album.
Nyboma album nimesahau Jina
King Kester Emeneya&Victoria Eleison (DREAM TEAM DREAM BAND) -Mboka Mboka humu vibao ninavyovikubali sana Ni Mifume na Moto na Tembe.
Awilo Longomba- Coupe' Bibamba ambapo kulikua na Vibao vikali kama Coupe Bibamba na Gate le Coin
Empire Bakuba ikiwa na wakali kama Papy Tex , Pepe Kalle (Kabasele Yampanya) na Bileku Mpasi wakiwa na Madamsa wao mbilikimo maarufu kama Emoro album FULL OPTION. Nyimbo zao Maarufu pasipo kuangalia album ni Kama Roger Miller, Yanga Afrika, Full Option, Swabila (pesa wax) Mpenzi Bupe (utunzi wa Papy Tex) pamoja na Hidaya;nyimbo Hizi mbili za Mwisho waliimbiwa Mabinti wa Kitanzania.
https://m.youtube.com/watch?v=NII0zSThFGE
https://m.youtube.com/watch?v=yffmok3VBCU
Extra Musica Etat Major (1998) na Shalai (1999)
https://m.youtube.com/watch?v=SAIbCxVqiDM
Wenge Musica Maison Mere Bendi ikiongizwa na Werrason, Didier Masela na Adolphe Dominguez ambao wawili wa mwisho baadae watatoka na kumuacha Werrason pekee kama kiongozi. - Solola Bien jina la Album ( meaning Speak Properly, Hii ilikua ni diss kwa J.B Mpiana na Wenge BCBG yake) humu ndani Kulikua na Vibao hit kama Solola Bien Yenyewe na Vita Imana ya Fere Golla. Golla alikuja Kujiunga na bendi hii akitokea BCBG kwa J.B Mpiana.
Album Hii ilikua na mafanikio makubwa na kuibua Vipaji vikubwa kama Rapa wa Bendi Bill Clinton Kalonji. Pia wakafanya remix ya Wimbo Kalayi Boeing (orijino ya Huu wimbo Iliimbwa kabla Hawajatengana na J.B Mpiana)
Wenge BCBG ya Jibe Mpiana- Titanic jina la Album akimaniisha Wenge Yao imesambaratika na Kuzama kama Meli ya Titanic baada ya Werrason na wenzake kuunda Kundi jipya la muziki. Wimbo wa Titanic ukibeba jina la Album
Kabla ya Album hii, J.B alitoa album Feux De l'amour ikiwa na Hit song kama Ndombolo, Feux De l'amour, na masuwa
Mwaka 2000 akaja na Album Toujours Humble ikiwa na Hit Songs kama TH, 48 Heures Gecoco,
https://m.youtube.com/watch?v=09JP...pa Wemba Hii Comment inabidi Niifanye Uzi.