Mark 11 grande inatumia angalau kilomita 10 kwa Lita 1 kama unasafiri,lakini kwa mishemishe ya mjini inakadilia kilomita 7 au 6 kwa lita, Mimi nina Cresta 1g kavu, pia nina Bighorn 3.0 turbo diesel 4jx1 engine, bighon yangu inakula mafuta vizuri sana kuliko hiyo Cresta, hii bighorn kwa mishemishe ya mjini kwa kweli inatumia kilomita 10 hadi 11 kwa Lita, ninaposafiri inatumia kwenda kilomita 12-13 kwa Lita 1 nikiwa na air condition on. Nikiangalia hapo labda kama una Bighorn ya petroli V6 kweli inakula mafuta, ila kama ni diesel 3.1 turbo 4jg2 bola endelea kuendesha bighorn kuliko Mark 11, maana hiyo mark 11 ninavyofahamu agiza ambayo haina engine ya 1g. Kama itakuwa 1g basi ulaji WA mafuta ni sawa na Cresta yangu,utakuwa hujasave kitu, bora u shift kwenye premio au gari ambazo hazizidi 1500cc.