Marks ya chini kabisa ambayo ulishawai pata kwenye mtihani ni ngapi

Wakati niko darasa la tatu niliwahi kupata nusu. Yaani katika maksi 100% mimi nikapata 1/2.

Hata moja kamili sikupata.

Ndo maana nikaishia kubeba boksi.
 
Mimi shule nilikuwa kilaza, nikipata juu 30 ni furaha kwangu. Kufeli ilikuwa desturi hayo masomo ya sayansi kupata chini ya kumi ilikuwa kawaida.
 
Nina pepa langu la physics advance baada ya kupewa maswali 14 nikachagua 10 ninayoyaweza nikaishia kupata 1.5% nime u laminate mpaka leo ule mtihani though sometimes nahisi sio kua sikua na akili ni pepa lilikua gumu maana wa kwanza alikua na 38%


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Nakumbuka nikiwa darasa la 5 mwaka 1999 alikuja ticha mmoja kutufundisha hesabu sasa kimbembe kikawa kwenye mtihani wa kumaliza mhula wa mwisho. Mimi nilipata 18/100, yaan 9/50. Mtu wa kwanza ambae ni mdogo wake alipata 72, yaan 36. Watu tulidata ila baada ya pale nilienda twisheni kwake, nikaanza kuigonga hesabu vizuri. Ticha Braison uliekuwa Buzuruga ubarikiwe sana kunifanya nikafaulu shule ya msingi. Ila nilipokuja sekondari kikawa kisanga kingine tena eeeh
 
Sekondari toka form 2 mpaka namaliza sijawaji kupata 25 za hesabu[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28] ila Mungu wa ajabu Phy nilipiga C mtihan wa mwisho

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waliopita SJUT 2008 wanaukumbuka mgomo baridi kwa Wandera,jamaa alitupa marks had negative 5,yaan ukifanya pepa nyingine ndo utakuja pata kuifidia hiyo -5 uliyoipata kwenye test one

Hiyo ni REGIONAL AND URBAN SYSTEM

TUKAANDAMANA TUKIDAI JAMAA SIYO MTANZANIA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Advanced Chemistry nipo form five. Test ya kwanza imekuja imejaa maphysical chemistry kila swali linaenda shida ikawa kwenye calculator..! Naingiza naona napatia kumbe chaka..! Matokeo yanakuja nna bonge la buyu..! Naitwa mbele kusolve nayapata yote..! Ticha ikabd anionee huruma na nakunipa 5/100

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maths namba zangu zilikuwa hazizidi vidole vya miguu, 7, 10, 15 zilikuwa kawaida
 
12 ya Digital signals and processing ........Kwa aliyesoma bachelor degree ya electronics na communication chuo kikuu ataelewa mbinde ya huu mziki , hatari sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi juzi tu hapa semister iliyoisha nilipata 0 kwenye test two ya financial management. Mwalimu alitoa sehemu ambayo sikuwa nimesoma kabisa so nilichokifanya, zile hesabu nilajitungia njia yangu binafsi na kuzifanya. Nachoshukuru nilijaza karatasi zote nilizopewa na mwalimu but ndo hivyo nikaikwaa sifuri.
 
Nilikua cjawahi pata zero ila nimeipata chuo kikuu aisee sitasahau naingia pepa cjui hata cha kudanganya ila nusu au nusu na robo tulipata zero

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…