Marlaw, Mwanamuziki ninayemkubali sana: Nyimbo zake hizi mpya za ‘Taa’ na ‘Baraka’ ni hatari fire

Marlaw, Mwanamuziki ninayemkubali sana: Nyimbo zake hizi mpya za ‘Taa’ na ‘Baraka’ ni hatari fire

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Marlaw ni msanii wa Kiume ninayemkubali sana hapa Tanzania aisee maana anajua sana kuimba anajua kupanga mashairi yake aiseee huyu mwanaume, na wala hana makuu kabisa

Sasa hebu angalia na sikiliza hizi nyimbo mbili alizoachia hivi karibuni ya ‘Taa’ na ‘Baraka’ yaani bora amerudi kwenye game japo sio kwa kishindo kikuu ila mimi roho yangu kwatuuu sana kwa sasa.

Mimi hapo nimependa nyimbo zote ila zaidi mahadhi ya Baraka yamenikosha aisee, huyu Mwanaume anajua sana. Yaani ni msanii ninampenda sana

Unajua huyu sio kama akina Diamond ambao wanatafuta kiki sijui wanajibu watu wanafanya hivi ndio atoe wimbo, kitu kinachofanya hadi sasa hiyo ndio iwe trend yaani mtu anatafuta tukio ndio atoe wimbo

Marlaw wewe unajua sana. Usiondoke tena kwenye game sasa ukatukosesha utamu mashabiki wako
 
Yaani nakubali yooote uliyosema kasoro kwa uliposema sio kwa kishindo kikuu. Hiki ni kishindo kikuuuu mkuu.

Wenye mziki wao wamerudi
 
Habari yako mrembo beth

Naona umeonasha mahaba hapo. Ila yote kwa yote Marlaw anajua na nadra sana kukosea
 
Spotlight ikiwa kwako ndo uvune vyote
ikishaondoka hata ulete miujiza gani huna utakachokipata

Supu hunywewa ikiwa bado ya moto
 
Taa video binafsi sijaipenda,Audio safi sana. Baraka nalikua sijaipata bado ndio naipakua hapa.
 
Spotlight ikiwa kwako ndo uvune vyote
ikishaondoka hata ulete miujiza gani huna utakachokipata

Supu hunywewa ikiwa bado ya moto

Ni kweli kabisa ila kwa huyu Marlaw kanifanya kuamini yeye anajua muziki habatishi. Nadhani atarudi kuwa vizuri sana huwenda isiwe kama mwanzo ila sijaona hata aliyeweza kuziba pengo lake wakati hafanyi muziki
 
Taa video binafsi sijaipenda,Audio safi sana. Baraka nalikua sijaipata bado ndio naipakua hapa.

Kwenye video ya taa, kweli ni kawaida. Ila angalia baraka Mkuu utaipenda pia sana tu
 
Kajamaa kanapenda kurembua rembua macho.
 
Ni audio tu ili mimi nineipenda sana, naamini ataitendea haki kwenye kichupa chake
Wacha tungoje kichupa kama nilivongoja taa, Tatizo Taa nilikua na idea yangu kichwani ya kichupa sasa imekuja tofauti nimekua disillusioned. Pia Directoe anaitwa somebody Musiba atakua amechangia kuharibu kichupa huyu
 
Nilitaka kushangaa kama ungetoa uzi bila kumtaja Diamond....ama kweli mti wenye matunda lazina upigwe mawe
Marlaw ni msanii wa Kiume ninayemkubali sana hapa Tanzania aisee maana anajua sana kuimba anajua kupanga mashairi yake aiseee huyu mwanaume, na wala hana makuu kabisa

Sasa hebu angalia na sikiliza hizi nyimbo mbili alizoachia hivi karibuni ya ‘Taa’ na ‘Baraka’ yaani bora amerudi kwenye game japo sio kwa kishindo kikuu ila mimi roho yangu kwatuuu sana kwa sasa.

Mimi hapo nimependa nyimbo zote ila zaidi mahadhi ya Baraka yamenikosa aisee, huyu Mwanaume anajua sana. Yaani ni msanii ninampenda sana

Unajua huyu sio kama akina Diamond ambao wanatafuta kiki sijui wanajibu watu wanafanya hivi ndio atoe wimbo, kitu kinachofanya hadi sasa hiyo ndio iwe trend yaani mtu anatafuta tukio ndio atoe wimbo

Marlaw wewe unajua sana. Usiondoke tena kwenye game sasa ukatukosesha utamu mashabiki wako
 
Hii nayo ni moja ya nyimbo zake ambazo hazikusikika vizuri kabisa. Sijui shida inakuwa wapi
Marlaw ana nidhamu na heshima sana kiasi kwamba anashindwa kutafuta kick nahisi kama wengine.
 
Spotlight ikiwa kwako ndo uvune vyote
ikishaondoka hata ulete miujiza gani huna utakachokipata

Supu hunywewa ikiwa bado ya moto

Sidhani maana kuna vichaa kama dully sykes ambao wapo miaka yote na bado hitz zinasoma. Talent ya ukweli ni timeless na kama mtu akiwa flexible inakuwa rahisi kurudi
 
Ile ngoma yake inaitwa so Mimi, ninaapa mbele ya mungu so Mimi. nakupenda Sana.
 
Nilitaka kushangaa kama ungetoa uzi bila kumtaja Diamond....ama kweli mti wenye matunda lazina upigwe mawe

Sio yeye pekee anayetafuta kiki kabla kutoa nyimbo ni wengi tu yeye kaja hapo kama mfano tu. Na pia na yeye ana nyimbo zake nzuri tu
 
Back
Top Bottom