jamni mbona mnaleta mambo ya siasa na muziki, hebu tumpongezeni kijana wetu mtanzania Marlaw kwa hatua anazopiga deily, watanzania ni watu wenye wivu sana especially pale mtu anapofanikiwa.
zaidi hubaki kuponda tu, wenzetu wazungu mtu anapofanya kitu kizuri hutuzwa na kusifiwa na pia watu wengi huongezeka kumpa sapot ili hiyo kitu alichokifanya kizidi kuwa juu zaidi.
hapa ilikuwa inaongelewa juu ya marlaw kuachia website nzuri na inayovutia sana ambayo imetengeneza na watanzania, mimi niliona ni muhimu sana kulisifia hili swala la kuwa na website.
faida za website ni kama sasa watu toka duniani kote wasiomjua marlaw sasa wanaweza mfahamu na kusikilaza muziki wake hii itapelekea jamaa kupata show za kimataifa hivyo kuja kuwa mwanamziki maarufu duniani.
faida nyingine ni kama watu walioko mikoani, kama mimi, ni vigumu sana kupata nyimbo, habari n.k kutoka kwa wasaniii mfano nimesikia wimbo mpaya wa marlaw kwenye redio inakuwa ngumu mimi kuupata mpaka nisubiri albamu itoke au nisubiri upigwe redioni.
sasa kijana marlaw ameturahisishia sisi watu wa mikoani kupata nyimbo zake tena bure na kuangalia video hata kwenye simu,
jamani hamuoni kama ni maendeleo hayo?? pia kupitia website yake tunaweza kuwasiliana nae, na jamaa kweli hujibu messege zote tunazomtumia iwe kwa email, facebook au kupitia form ya mawasiliano kwenye website yake.
swala la siasa ile ni biashara jamani kama wanavyofanya wasanii wengine, mfano kwenye uchaguzi wa marekani 50cent alimpigia kampeni mpinzani wa obama.
hata hapa bongo hao ccm walikuwa ni wateja wa marlaw katika biashara yake ya muziki,
Narudia tena, mfano wewe ni mfanya biashara wa sukari na vitu vya dukani, je akija mtu aliyevaa jezi za kijani na njano ambaye ni mwana ccm piwa na anaipenda toka moyoni na wewe hukipendi hicho chama je utaacha kumuuzia bidhaa??
hebu tuamke watanzania wenzangu, tusiendekeze siasa kwenye mambo ya maendeleo kama haya, japokuwa siipendi ccm ila kwenye ukweli tuwe wakweli,
mimi mwenyewe ni chadema damu damu, na ninaupenda sana muziki wa marlaw, kwasabu napenda maendeleo marlaw alipowaimbia ccm haikuniuma bcoz niliamini alikuwa anafanya bishara tu,
hata chadema au cuf wangemuwahi na kuongea nae kibishara basi naamini marlaw angewaimbia tu.
sasa tuache kuingiza siasa, wanasiasa wa ki africa hawana uzalendo na nchi bali miili yao na familia zao tu.
website ya marlaw ni
www.marlawmusic.com
hongera sana marlaw hope wasanii wengine watafuta nyayo zako.