Mzee, naona ulinielewa vibaya. Sijaandika kwa hasira na wala sikuwa na nia ya kuandika kwa hasira. Ni katika kutoa tu mawazo yangu.
Juu ya Perry nilikuwa nasema kuwa Bob alisaidiwa na producer wengi na mmoja wao ni huyo miaka hiyo ya nyuma. Hiyo Black ark si ilikuwa studio yake anayodai aliichoma? Anyway achana naye ingawa bado ni muhimu.
Ukija kwa Chriss Blackwell na Island Record yake, ni kuwa huyu jamaa aliwaachia akina Bob studio yake, wawe wanaingia na kutoka anytime wakitaka. Hii iliwapa ari kubwa na nguvu kubwa kufanya vitu vya maana ukichukulia kuwa mwanzo Dodd aliwatia ndani hela zao.
Blackwell alikuwa mfanya biashara mwenye roho nzuri. Hakutaka kukamuwa watu hadi mifupa. Aliwapa na wao kidogo ili wawe na nguvu ya kuzalisha zaidi. Kama Bob, na yeye alikuwa Mu-Irish. Nafikiri hii ndiyo iliwagombanisha Bob na wenzake kwani walifikiri jamaa kawazika ila kwa maoni yangu ni kuwa walitumia jina la Bob (Irish) ili KUUZA album na huku pesa wakigawa kama walivyokubaliana. Jamaa wakawa na donge kuwa Bob kawazika na Bob akiwa na donge la kupakaziwa.
Juu ya Cliff na Blackwell, uko sawa kabisa mkuu. Na kama nilivyosema, jamaa alikuwa mfanya biashara, akiuma hapa na kupuliza pale. Ila ukweli unabaki palepale kuwa bila Blackwell, Mziki wa Reggae sijui kama ungelipata umaarufu huo. Jamaa ameutangaza si kawaida na hasa kwa kutumia studio lake la Island.
Nafikiri mwisho wa siku, inategemea masikio yako yamempenda nani. Mie ukweli ni mpenzi wa Tosh na the same reason nampenda Dube (copy ya Tosh). Bob sauti yake si mbaya na wala si nzuri ila QUALITY ya mziki (instruments) kwenye nyimbo za Bob hasa zile za mwisho kwa kweli INATISHA SANA. Ukiwa kwenye sehemu na chombo kikali, vynil ya Bob inacheza kwenye technics na spiker zinakwenda around 20Hz-20,000Hzs, kwa kweli utaona raha ya Mziki. Bob album zake alikuwa akifyatulia Jamaica ambako sijui kwa nini wana quality nzuri wakati Tosh alikuwa akifyatulia USA (baadhi ya album). Hivyo hata mie mwisho wa siku hujikuta nawapenda wote ila IN GENERAL, zaidi naelema kwa TOSH.