Maroboti ya kielektroniki 'misukule ya kielektroniki' ndo future ya kutawala ulimwengu wa dijitali

Maroboti ya kielektroniki 'misukule ya kielektroniki' ndo future ya kutawala ulimwengu wa dijitali

N'yadikwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2014
Posts
7,427
Reaction score
10,905
Lugha hutoa fursa nyingi sana za utumiaji wa vipawa vyetu kama binadamu...

Lugha huakisi akili wa yaliyomo katika bongo, fikra na hisia zetu kama biandamu...

Badala ya kila mara kuweka mawazo yetu katika maneno yetu wenyewe, mara nyingi sisi huwasilisha hisia zetu kupitia maneno ya wengine... (Ndo maana sio ajabu humu JF kuna watu ili kuridhisha nafsi zao lazima wataje majina ya wengine wawakwoti na hata kuwatusi)

Mara nyingi tunaridhika kwa kunukuu, kuiga, kuazima, kutofautiana au kuangazia kile ambacho wengine tayari wamesema...(Timu Ukraine na Urusi wanaongoza kwa hili...wanasoma huko kisha wanakuja kutema uongo na ukweli humu)

Sasa; Mitandao ya kijamii kama vile Twitter huinua utumiaji wa lugha na hisia zetu kuwa kanuni muhimu ya mwingiliano wa kidijitali (digital interaction technique)...

Kwenye majukwaa kama haya, tunapenda sana kuwafuata watu tunaodhani wanatuvutia na kugusa hisia zetu kwa namna moja ama nyingine...wakati mwingine hatujaunganisha hisia zetu na binadamu wenzetu...huwa tunaunganisha hisia zetu na mashine

Sio kila mtu anayestahili kufuatwa kwenye haya majukwaa ya Mitandao ya Kijamii ni mwanadamu, na sio kila kitu ambacho kinafaa kutuma tena retweet kiliundwa kwanza na mtu halisi...wengine ni MAROBOTI na watu ghafi wanaobadili jinsia, utambulisho wao binafsi nakadhalika... (Hata mimi Nyadikwa usiniamini naweza kukwambia nipo Mafinga kumbe naandika hii sledi nikiwa kwenye handaki Yukleini).

Zaidi na zaidi ya maudhui yenye ustadi wa hali ya juu na ya kufikirika unayoyaona kwenye Twitter kwa mfano yanatolewa na maroboti, hii ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na
Tony Veale, Alessandro Valitutti, Guofu Li, wa School of Computer Science and Informatics, University College Dublin, Belfield, Dublin D4, Ireland.

Mifumo ya bandia ambayo huandika kiautomatiki imejengewa uwezo wa hali ya juu sana...na USHINDANI WA KISIASA TAYARI UNAHAMIA KWENYE MTINDO HUU...mifumo hii ina uwezo sasa wa kutuma jumbe (ku-broadcast) kwa watu wengi zaidi na kupendekeza aina fulani ya maudhui kwa watumiaji wapya...

WANASIASA jiongezeni huku ndo majukwaa mapya ya kampeni...next elections raia zitakupigieni kura mkiyatumia vizuri haya maroboti.
 
Dunia imeenda mbali sana na hicho ndio tunajivunia wapenda technology, sasa hivi ni mwendo wa kulipia bidhaa kwenye maduka, kwa chip zilizopandikizwa kwenye mwili
 
Mada nzuri kama hii imekosa wachangiaji, nitarudi.
 
Back
Top Bottom