SoC02 Maroboti yanakuja kutunyang'anya kazi

SoC02 Maroboti yanakuja kutunyang'anya kazi

Stories of Change - 2022 Competition

Timothy Sawe

New Member
Joined
Jul 27, 2022
Posts
3
Reaction score
15
Hali ni mbaya!

mahindi-data.png

Chanzo: Mwananchi, Tani 7,400 za mahindi zakosa soko (2014)

Nilikuwa Kilombero, na kama masihara, gunia la mchele lilikuwa linamwagwa mbele ya uso wangu jalalani. Nisingeamini ningehadithiwa na mtu mwingine. Mazao mbalimbali yaliyokuwa yanaelekea masokoni yalitekelezwa pembezoni mwa barabara bado yakiwa yamefungwa kwenye magunia. Wakulima tofauti wakiwa katika hali ya kilio wakidai bei zao zilishushwa sana na kwa ghafla msimu huu wa mavuno.

Nilisikia kwa juu tu kuhusu mchina mmoja. Yeye alikuwa anajishughulisha na kilimo cha mchele chini ya kampuni inayoitwa Zhang Investment Limited. Aliweza kujipatia ukiritimba kwenye masoko mbalimbali ya zao hili.

Sifa kuu iliyotofautisha mazao yake na ya wakulima wadogo wadogo ni utumiaji wa mbegu zilizotengenezwa maabarani yaani, GMOs. GMOs ni aina ya viasilia vyenye uhai vilivyobadilishwa maumbile na wataalamu wa jeni. Vinabadilishwa viweze kutoa mazao mengi kuliko kawaida, kudumu katika hali tofauti za tabianchi kama kuweza kutoa mazao katika vipindi vya mvua, mafuriko hata ukame, na kutoa mazao ndani ya kipindi kifupi kisichokuwa cha kawaida.

Ni miezi michache baada ya wao kuleta bidhaa zao sokoni, ndipo hata wakulima wengine wa nje za nchi nao kuiga mfano huu na kuleta hizi mbegu za GMO masokoni, hivyo kutawala masoko yote ya wakulima wetu wadogo. Alizeti, bamia, mpunga, kahawa, ngano, mlonge, pamba, ndizi, matikitiki na mazao mengine mengi yalishikwa na aina hlii la zao.

Asali tu ilibaki kuwa zao pekee lililowaingizia wakulima wetu faida kwa kuwa wanunuzi wa zao hili wanapenda asali za asili, yaani kikaboni, hivyo basi wako radhi kulipa hela nyingi zaidi ilimradi kupata kitu kitakachokuwa cha uhakika. Nyuki wetu si wa ki-GMO, yaani hawajabadilishwa maumbile, ni wenye afya tele, na si kama wengine hali wakiwa wamechoshwa na mabadiliko ya mazao wanayohitaji kutengeneza vyakula vyao na kuwalazimu wanasayansi kuwabadilisha jeni. Hii hali imekumba nchi nyingi sana za Magharibi na wenzao wa bara la Asia Mashariki.

Niliteuliwa kama mshauri mkuu katika ofisi ya Raisi kukumbana na mabadiliko ya tabia nchi. Katika mashauri niliyoyatoa, moja ni, ili tuweze kupunguza makali ya mabadiliko ya tabia nchi, inatulazimu tuwe na viwanda vyetu hapa nchini vitakavyoshirki katika zoezi la kuchunguza aina ya mazao yanayotengenezwa kwenye maabara, GMOs, ambazo ni salama tujue mapema namna ya kushindana na asasi za kimataifa zinazojaribu kutawala uchumi wetu kwa njia ya kilimo. Endapo watafanikiwa kunyima wananchi wetu uwezo wa kuuza mazao yao ya kiasili, bila kununua mbegu zao, uchumi wetu utakuwa katika wakati mgumu. Mpaka sasa tumeshawaruhusu kuhodhi mazao tofauti, na kama basi mbegu zao zinachangia uharibifu wa mazingira na kuchochea mabadiliko ya tabia nchi, hatutaweza kusaidia nchi yetu kupona. Watatutawala kwenye masoko ya ndani na nje za nchi.

Nilisikitika sana mheshimiwa yule, muajiri wangu, aliepokea ripoti yangu alipoificha mezani mwake, akihofu kuwa nitachukua nafasi yake endapo raisi wetu atasoma ripoti ya namna hii. Mimi nilikuwa tayari hata kustaafu na kumuachia ofisi, lengo langu lilikuwa kuhamasisha jamii na Tamisemi kuchukulia swala hili kwa makini na kuanza kulitendea kazi. Nimeshindwa kutekeleza matamani yangu, kilichobaki ni dua tu.

Jana nilikuwa na bahati na fursa ya kuongea na kijana mmoja. Kijana huyo alinidokeza mpango wake wa kuanzisha madarasa ya kufundisha uhandisi wa kimekatronikia na robotiki. Aliamini ya kuwa hatima ya nchi hii si katika kushindana na wenzetu wa ughaibuni kwenye utengenezaji wa mbegu bora za GMO, bali katika maandalizi ya vijana wetu kwenye soko la ajira, kuweza kutumia fursa zitakazojitokeza hususani katika kipengele cha otomesheni, yaani mashine zinazoweza kufanya kazi bila usimamizi wowote. Yeye anaamini maroboti yatakapoanza kuajiriwa huku nchini, ni vijana wetu watakaoathirika zaidi na uhaba mkubwa wa ajira kuliko kuathiriwa na uchumi kwa upungufu wa mazao yetu ya kiasili.

Katika mazungumzo yetu, alitia sana mkazo swala la kuruhusu vijana kuwa na michezo na mashindano baina ya mashule itakayowafungua macho kwenye maswala ya kuandika lugha za tarakilishi kama C++ na Arduino, na kulea kizazi kijacho katika mifumo ya kiteknolojia ili pale mabadiliko ya ajira yakianza, wataweza kudaka kila fursa itokanayo na mabadiliko hayo.

DkQOYUFWsAAYORd.jpg


Sio lazima mtu awe amepitia masomo ya Sayansi, wala awe mtalaamu wa tarakilishi kuweza kutumia hizi teknolojia za kirobotiki. Hata mwasibu anaweza akatoa tu maelekezo kwa mdomo kwenye simu au tarakilishi yake na hio programu itatafsiri maelekezo hayo kuwa lugha za kitarakilishi. Alijaribu kunisaidia kuelewa jinsi huu mfumo unaoitwa GPT-3 unavyoweza kumsaidia mtu yeyote kutengeneza programu yeyote kwa maneno kama mazungumzo kati ya binadamu. Mtu mmoja ataweza kuiambia simu yake “nataka tovuti ya kuniwezesha kuuza nguo zangu mtandaoni,” nayo itatengeneza tovuti hio yenye rangi, vitufe na hata vipengele vyote vingine vitakvyomwezesha kuweka bidhaa zake na mnunuzi kuzilipia. Kwa jinsi alivyozidi kujielezea, kwa kweli uongo mbaya, mimi sikumuelewa. Nilibaki tu natikisa kichwa juu na chini na kutabasamu kumuonyesha sikutaka aache kuongea. Huenda katika yote kuna kitu ningaliweza kudaka kinisaidie na mimi.

Lakini dunia hii ni ya ajabu. Baada ya kuachwa na maswali mengi kuliko majibu, nalisafiri kutoka jiji la Nronga mpaka pale mpakani Simiyu. Sikuamini macho yangu tena kama ningalishuhudiwa na mtu. Shamba zima lilikuwa likimwagiliwa, kulimwa na kupaliliwa na matrekta na ndege zisizokuwa na binadamu akiziendesha na kuzirusha.

103940100-case_driverless_tractor.jpg

Chanzo: CNBC

Shamba lenyewe lilikuwa ni kubwa. Kwa jinsi nilivyoona tulipopita na basi, nilikadiria takribani eka hamsini! Yule kijana aliposema maroboti, nilitegemea kuona mashine-watu yaani mashine zinazofanana na binadamu zikiendesha shughuli za kilimo. Filamu ziliniharibu sana. Jinsi mfumo huu wa sayansi na teknolojia unavyozidi kukua kwa kweli huleta fursa nyingi na changamoto kwetu sie ambae tunakuwa wabishi na wavivu kujiongeza kifikra.

maxresdefault-2.jpg

Chanzo: Drones R Africa

Kwa jinsi ninavyoona mabadiliko yakizidi kutawala kila sekta ya uchumi wetu, ni vyema kama jamii tujiondolee hofu ya kujifunza vitu vipya, tusiwe wategemezi bali tuwe tayari kuongea kuhusu mifumo duni ya nchi hii tuyaboreshe kabla nchi za nje hazijashikilia kila soko na mizunguko ya fedha. Endapo tutakapofika huko, kutawaliwa na watu wenye maadili, tamaduni na siasa geni au hata potofu, basi waliotushindia uhuru na waliotoa maisha yao kwa ajli yetu watakuwa walifanya kazi bure.

Kizazi hiki kitaamua hatima ya vizazi vingi vijavyo.


95.png

Chanzo: IDTechEx
 
Upvote 13
Hongera kwa bandiko zuri lenye tija na lililopangiliwa vizuri.

Kwa bahati mbaya wenye Mamlaka hawapo tayari kuwekeza katika elimu sahihi yenye kuwainua raia wao ila wako bize kupanga nani atafata 20'25 akitoka flani

Shame, the end is near
 
"Nilisikitika sana mheshimiwa yule, muajiri wangu, aliepokea ripoti yangu alipoificha mezani mwake."..

iweke hapa tuisome kwa manufaa ya wote.


Kuhusiana na ma roboti tayari OpenAI wamesha zindua roboti lao chatGPT 3.5 na liko kwenye majaribio na limeleta kishindo kikubwa kwenye tech world kiasi kwamba Google wameonyesha ku panic wazi wazi kuhofia kufunikwa.
 
Kiukamilifu ni kua mfumo huu mpya wanauita AI yaani Artificial Intelligence, ishafika wakati sasa Technologia inaweza tawala kila kitu. kwa mfano, kufunga pazia ikiwa jua lishatua, kupika chakula unachokipenda yaani ilimradi, kuna Software inajua unawaza nini na kukufanyia..................!
 
"Nilisikitika sana mheshimiwa yule, muajiri wangu, aliepokea ripoti yangu alipoificha mezani mwake."..

iweke hapa tuisome kwa manufaa ya wote.


Kuhusiana na ma roboti tayari OpenAI wamesha zindua roboti lao chatGPT 3.5 na liko kwenye majaribio na limeleta kishindo kikubwa kwenye tech world kiasi kwamba Google wameonyesha ku panic wazi wazi kuhofia kufunikwa.
yes, infact, nimeandika jinsi ya kutumia mwenzake ChatGPT inayoitwa MidJourney AI kutengenza picha kutumia A.I. Refer hapa Jinsi ya kutumia Midjourney AI kutengeneza picha
 
Andiko linaogopesha sana..hatima yetu m
Kama wakulima ni hatari sana[emoji37]
 
Hii kitu inaogofya,Ila haipaswi kudharauliwa hata kidogo, it's really, Tujiweke tayari.Tutaikubali tukitaka au tusipotaka.
 
Back
Top Bottom