Marriage intelligency: Je, ni kitu gani au tabia gani ulitaka kuiondoa?

Marriage intelligency: Je, ni kitu gani au tabia gani ulitaka kuiondoa?

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2012
Posts
20,561
Reaction score
24,428
Ndoa Kwa wenzetu wenye I.Q kubwa sio kama vile tuzaniavyo sisi huku afrika, kwao ndoa huwa zinaenda au huwa na malengo ya ndani zaidi, ambayo pengine ni ya kitabia, akili za familia fulani na kadhalika.

Mimi binafsi katika kufuata logic hii niliangalia mapungufu yaliopo ndani ya familia yetu kwa ujumla nilichogundua ndani ya familia yetu life span ya vizazi na vizazi walikuwa hawafikii umri wa miaka 45 na wakizidi sana basi hufikisha miaka 50.

So baada ya kulidadisi hili kwanza nilivunja kanuni Kwa kuoa binti kutoka mbali na mkoa wangu, pili nilikagua life span za koo zake na kujiridhisha lifespan yao Kwa kizazi chao ni above 90yrs.

Je, wewe ndugu yangu uliangalia lipi ili ku-balance mapungufu ambayo huwa hayakosekani katika familia zetu, au uliangalia tu mzigo na urembo?
 
"Huyu ni dada angu Baba mmoja mama mbalimbali" au "huyu ni Kaka angu mama mmoja Baba mbali mbali" nataka niifute hii dhana, nataka ianze na Mimi!
Hivi inakuwaje yaan unakuta Watoto mama mmoja baba tofautii ,hii inapelekea watoto hawapendani hawaelewani inakuwa kama laana hivi.

Inakuwaje mwanamke unazaa na kila mwanaume tu ,hadi watoto watano
 
Angalia Sana magonjwa sugu...
Kisukali. N.k usije kurithi kwenye kizazi chako
 
Angalia Sana magonjwa sugu...
Kisukali. N.k usije kurithi kwenye kizazi chako
Exactly!!,magonjwa sugu,Ukichaa,Uwehu...!"uvivu mkali"uliopindukia maana zipo familia ni wavivu by nature.

Pia endapo kwenu ndio kumeathirika inabidi uselect pure from others side! Ili ujaribu kubalansi situations!..Leo hii watu wame concentrate kwenye "figure" au matako manene na si kwenye kizazi cha mbele,ukizingatia sisi Wote ni Stranger with a limited time.
 
Babu yangu alioa huko mazinde upareni. Aliambiwa asioe akaleta kiburi maana ndugu zake wawili ni wakike yaani wadogo zake na hao wadogo zake wote waliolewa huku lushoto na wasambaa .

Matokeo babu ambaye kazaa na kupeleka wanae huku upareni yaani mmoja wapo ni mzee wangu mmi ndo wa kwanza katika wanae.

Kazaa watoto 12 wawili walikufa hata miaka 10 hawakufika ,baba yangu aliondoka huko kwao mapema akiwa na 16 ana kuja kuishi maeneo ya mjini basi hakuadapt tabia nyingi za huko upareni, the rest wanawake kati ya watano kaolewa mmoja pekeake pia aliolewa huko lushoto ndoa yake Ina miaka 30 na kitu mpaka sasa waliobaki wanazlishwa tu...hawana ndoa.

Wakiume wamekuwa wapenda kesi kila siku mahakamani kuuza mashamba kuendesha kesi maendeleo hakuna wamekuwa wabahili yaani hata kuwekeza zero. Ila life span yao ni ndefu kwa wengi washavuka 60 wanaishi fresh. Ujinga wao wanamtegemea baba na alishawakimbia kitambo sana kila kitu hata ishu za kusomesha watoto wao.

Wale dada zake babu waliolewa huko milimani ,mmoja ana watoto sita wote wakike wawili wameolewa safi ,wanaume wanne wanashindana kwa utajiri wako town ukienda Tanga ni miongoni wa wasambaa wanasumbua sana kwa pesa na wanabebana sana wako njema kila kona wameshika dini hawanaga mambo ya ukorofi wala kesi za ajabu.

Point yangu angalia nasaba za ukoo utakuja kuingia sipo uje kujuta utakuja kuzaa matoto zero tupu, kwa kufauta misambwanda, koo nyingine ni laana ukifika huko polisi kesi za ovyo majina ni hayo hayo tu kila siku .Tuwe makini tutakuja kubeba magonjwa mno
 
Hivi inakuwaje yaan unakuta Watoto mama mmoja baba tofautii ,hii inapelekea watoto hawapendani hawaelewani inakuwa kama laana hivi.

Inakuwaje mwanamke unazaa na kila mwanaume tu ,hadi watoto watano
Ni mtihani Kwa kweli, tena kwenye malezi ukute mtoto mwingine Baba yake ana uwezo na anamuhudumia mwengine Hahudumiwi...usipokua makini watoto wanaweza kuwa maadui.
Basi tu changamoto za mahusiano zinapelekea hivo, unakuta kila chaka unalooingia ni bovu.
 
"Huyu ni dada angu Baba mmoja mama mbalimbali" au "huyu ni Kaka angu mama mmoja Baba mbali mbali" nataka niifute hii dhana, nataka ianze na Mimi!

Kama ni dini ya mwarabu.. kuifuta hii sio rahisi
 
Hivi inakuwaje yaan unakuta Watoto mama mmoja baba tofautii ,hii inapelekea watoto hawapendani hawaelewani inakuwa kama laana hivi.

Inakuwaje mwanamke unazaa na kila mwanaume tu ,hadi watoto watano

Uwezo wa baba zao ukiwa tofauti lazima wachukiane..

Maana huyu baba yake anamlipia ada tusiime anafatwa na school bus.. mwingine baba yake hana hela anasoma kayumba.. hapo lazima chuki iwepo ya watoto
 
Inawezekana, hata huyo aliyeleta Dini Alizaa watoto Saba na mke mmoja, kumbuka alikuwa na wake 9....wengine hakuzaa nao.

Sijasema haiwezekani..

Ila nimesema sio kazi rahisi kwa kupima wastani wa hiyo hoja yako

Mume awe na Wake 4 halafu azae mke mmoja tu. Inahitaji miujiza
 
Uwezo wa baba zao ukiwa tofauti lazima wachukiane..

Maana huyu baba yake anamlipia ada tusiime anafatwa na school bus.. mwingine baba yake hana hela anasoma kayumba.. hapo lazima chuki iwepo ya watoto
Hili ni shida,double standard within hapa mama itabidi atumie akili kubwa kubalansi familia Yake jambo ambalo ni gumu Kwa kweli katika familia ya watoto 5 mmoja tu baba Yake awe actives wanaweza hata kumuwekea sumu.
 
Back
Top Bottom