Marriage is an outdated concept

Kwa wanawake wa sasa lazima kuwa macho mkuu
 
Ni kweli
 
Mkuu hapo kwenye point yako namba mbili nafikiri umesahau kitu kimoja tu, hiyo zamani wakati sifa za mwanamke kuolewa zilikuwa ni bikira na tabia njema zilikuwa ni enzi ambazo wanaume hawatongozi wanawake hovyo ili wapunguze tu upwiru, bali mwanaume alikuwa akimpenda mwanamke anaenda direct kwao kumchumbia na kumtolea mahari kisha anapewa mke wanaanza maisha ya ndoa

Lakini kwa hii dunia ya leo ambayo watu wamefanya ngono kama chakula mahusiano yanajengwa based on one night stand, friends with benefit, kufurahishana, kulana kimasihara, na upumbavu mwingine kama huo, watu wanajifanyia tu sex halafu mwisho wa siku mwanaume akitaka kuoa, aje aseme eti anataka bikira na tabia njema huyo atakuwa mzima kweli kichwani

Na mbaya zaidi ukisema jinsia zote zibadilike wanaume wanakuambia eti wanaotakiwa kubadilika ni wanawake ndio waache kukubali wakitongozwa, ila wao wanaume wanaona ni haki yao kutongoza wanawake hata wasio na malengo nao kwa gia ya kwamba watawaoa kumbe lengo lao ni kupunguza haja zao tu, yani eti wao kuwahadaa wanawake wanajiona wako sawa na wanafaa kuwa waume ila wanawake kuwakubalia wanaonekana wana matatizo na hawafai kuwa wake

Yani mtu urukeruke huku na huko ufanye umalaya uchezee na uharibu wanawake to your heart's content halafu ukitaka kuoa, ndio uje ujifanye unawalalamikia na kuwatukana wanawake kuwa hawajitunzi na hawajiheshimu kana kwamba siyo wewe uliyeshiriki kwenye kuwaharibu na kuwachezea, huku ukidhani kwamba jinsia yako itakubeba kwa kuwa unajua kwamba siku zote wanaodhalilishwa kuhusu suala la ngono ni wanawake kwa sana

Mimi ninachoweza kusema ni kwamba hao wanaume walioamua kushusha standards siyo kwamba ni wapumbavu ila wameamua kuacha kuwa delusional na kukubaliana na hali halisi, kwamba huwezi kuzini na wanawake halafu ukitaka kuoa uanze kutafuta mabikira katika hao hao wanawake ambao ulikuwa unazini nao sasa hao mabikira watoke wapi, huwezi kuyachafua mazingira halafu utegemee yakupe hewa safi lazima uchague moja ni either uyatunze mazingira ili yakupe hewa safi au uyachafue kisha uikubali hewa chafu yatakayokupa

Yani wanaume mnatakiwa muelewe kwamba kujitunza is not about nani anaonekana malaya na anadharaulika na jamii kati ya hizi jinsia mbili bali it's all about kupata mwenza bora wa maisha, maana hapa tulipofikia wanawake hawajali tena na wameshaanza kuzipuuzia hizo gender stereotypes na ndio kwanza wanazidisha maovu na huko tunakoelekea ndio kubaya zaidi, so it's up to you wanaume kuamua either mbadilike muache kuchezea na kuharibu wanawake au muendelee halafu mwisho wa siku mje kuoa hao hao maana ndio ambao wapo wala msidhani mtashushiwa hao mabikira mnaowataka

Ni kwa sababu imeshaonekana kwamba wenye shida na hizo bikira na tabia njema kutoka kwa wanawake ni ninyi na siyo wao wenyewe so ninyi kama ninyi mnafanya jitihada gani ili mfike nao wakiwa na hizo sifa hadi kwenye umri wa ndoa, kama bado mtaendelea kushindana nao kwamba wao ndio wajitunze kwa visingizio vya kipumbavu eti maumbile sijui nini basi msitegemee lolote na wala msiwalaumu pale ambapo mnataka kuoa bali mkubali tu kushusha vigezo vyenu na kuvuna mlichokipanda, tangu jamii imeanza kuwatukana wanawake matusi na kuwaita majina yote mabaya kama wanawake wangekuwa wanajali basi wangeshaanza kubadilika lakini matokeo yake ndio kwanza wanazidisha tabia za hovyo so my point is wanaume mkiona mnaumizwa na mnachukizwa na umalaya na ukahaba wa wanawake basi chagueni moja either anzeni ninyi kubadilika au la hamuwezi basi kubalianeni na hali halisi
 
Kuna mkaka leo katoka kuniambia anataka kunioa😄
Unajua nikamjibu nini? 'Bado niponipo kwanza'
Umri ni kigezo kimoja wapo cha kupata wa kukuoa, umri ukienda haurudi, umri kadri unavyokwenda ndipo soko linaondoka na kutekwa na vibinti vya 2000's
 
Kuna watu sio waoaji wanatafuta visingizio tu! Which is very okay.

Kuna watu hawawezi kuishi na watu, hivyo kuoa kwako ni salama zaidi.

Mali gani? Majaba, masufuria, na sabufa za Alitop? Na plot za 20*20 😂
Unaongea nini wewe, si bora hayo majaba, na sufuria, kule marekani ambako wabongo tunasema kumeendelea kulifanywa utafiti, asilimia 20 hadi 30 ya wanawake walienda kwenye date na wanaume wasiowapenda, ili tu wakale chakula cha bure.

Hivyo mwanaume hata ukiwa na kijimshahara cha laki 2, kuna wanawake wanakivizia mkuu, tena mbaya zaidi hao wanawake wanakua hawana hisia na wewe, na pengine wamekuzidi kipato mara kumi, ila kwenye mahusiano hawatokupa support yoyote, hata kukupikia binti kiziwi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…