Marriage is an outdated concept

Ni kweli! Lakini mpango wangu sio huo uliotolea mfano hapo juu
 
Ukiwa na watoto na mke wako mfanyakazi au mfanyabiashara na wewe pia mfanyakazi au wote wafanyabiashara utaelewa dhana ya mke mama wa nyumbani anashiriki vipi kutafuta mali za familia.

Watoto wanaumwa au mzazi unahitajika shuleni kwa mtoto huku wote shughuli zenu zinawahitaji muwepo ofisini utaelewa hii dhana.

Wote mnahitajika kusafiri au mmoja kazini mwingine safari ya kikazi no changamoto. Huwezi kumuachia majukumu yote mfanyakazi wa ndani hasa hayo niliyotolea mifano.

Ukiwa na mke mama wa nyumbani unarudi unakuta vitu vyote vipo sawa, watoto Wana maadili na tabia njema, wanavaa nguo safi, wanakula vizuri japo kwa pesa yako unakuwa na mawazo kama yako.
Sababu hujapata changamoto nilizo toleq mifano kwa vile mkeo alikuwepo badala yako kusimamia hayo yote.
 
Akitokea mwanaume anaeleweka narudia ANAELEWEKA just get married.
nwdays they don't come twice.

Labda kama kuolewa kwako si kipaumbele.
 
Kutokana na tafiti zilizofsnywa na taasisi moja nchini Kenya imebainisha kuwa ukilinganisha amani na utangamanonkayi ya ndoa za:-
1. Mume mfanya(kazi/biashara) VS mke mfanya(kazi/biashara).
2. Mume mfanya(kazi/biashara) VS mke mama wa nyumbani.

Ndoa namba 2 zina more stable families living joyfully and happily ukilinganisha ndoa namba 1.

Namba 1 pesa ipo lkn wala haifanyi kazi ya kulea vema watoto mliowatafuta. Watoto muda maisha yao % kubwa wako na house girls tu. Na mwisho pesa hiyo hiyo itasimama kama shetani wa kuisamabaratisha hiyo ndoa.
 
1. Mipango gani ambayo unahitaji kufanya before ndoa na haitaweza fanyika ukiwa ndani ya ndoa?

2. Kwann ndoa iwe mpango wa 3 why usifanye isiwepo kabisa si haina umuhimu au?

3. So unahisi mwanaume anapokuja kukutongoza akuoe ni kwa faida yake pekee yake yaani kwa maneno mengine unasema ndoa ni 100% kwaajiri ya mwanaume wewe unakwenda kumfaidisha tu na bila wewe kama mwanamke basi mwanaume hana maisha ya nje ya ndoa kama wewe hapo unavyojinasibu kuwa una mipango yako nje ya ndoa unahisi mwanaume hana?

4. Mipango gani ambayo mwanaume amekamilisha ndipo aoe hebu nipe ufafanuzi eneo hilo labda mimi kuna vitu kama mwanaume sivifahamu au sijavikamilisha.

5. Ni stress gani ambazo anakuwa nazo mwanamke ambazo zinaweza kuwa kikwazo katika kutumikia ndoa yake kwa umakini?

6. Kitu kinakuwaje cha muhimu halafu kisiwe cha ulazima?

7. So una muda gani wa kufanya mipango yako na wakati ukifanya hiyo mipango unakuwa single bila kuwa na mahusiano yaani hakuna kuingiliwa kimwili na mtu?

8. Je hiyo mipango yako inafaida gani kwa huyo unayekwenda kuolewa nae na kuishi nae pamoja na kama ina faida nae why ufanye pekee yako?

Naomba unijibie hayo maswali kwanza.
 
Kenya tayari wamefanyia amendment sheria ya ndoa yao.
Wanawake wa kiafrika wameiga life style ya wanawake wa kizungu bila kujua wenzao wana advantage ya kiuchumi kuwa na mazingira na maisha mazuri so hata maswala ya kifedha sio issue sana kwao.

Ila hawa Waafrika wanaleta viburi huku uchumi wenyewe huu unatandika balaa hata mkiwa wawili, sasa wao wakiwa bado wabichi dharau kibao, balaa ni wakishafika 30+ hapo ndipo wanaelewa kwann afrika ndoa ni muhimu kwa mwanamke kuliko elimu.

Ila ngoja watajifunza kwa vitendo kama kuwafundisha kwa maneno tumeshawaambia sana hadi tumechoka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…