Marriage is like quicksand... easy to get in difficult to get out

Marriage is like quicksand... easy to get in difficult to get out

Baada ya kutafakari kwa makini nimepata wazo ambalo linaweza kusaidia. Zianze ndoa za mikataba mifupi mifupi (kama vile lease). Mkataba ukiishi kila mtu anaanza vyake au kama wanataka kuendeleza wanaingia tena mkataba mpya wa miaka mitatu.
 
Asante Superman.

Lakini inakuwaje katika nchi zilizoendelea kuachana ni rahisi mno kuliko kwenye nchi maskini kama Tanzania?

TZ kuachana sio raisi kwa sababu wanawake wengi hawana kipato na wanategemea wanaume kwa maisha yao, kwa hiyo ni bora wa fight mpaka mambo ya tulie...

ukiangalia sasa hivi wanawake wengi wanafanya kazi na rate ya kuachana imeongezeka

mfano UK kuna wa kina dada wengi wa kiTZ wanamakaratasi basi kila siku wanawafungia wanaume zao nje na kuwatoa ndani ya nyumba, vitu kama hivi hawawezi kuvifanya TZ kwa ajili wao ni tegemezi, kwa hiyo kama unataka kujua the true colours za wanawake waTZ wape hela
 
Tatizo la Tanzania maswala ya utunzaji wa kumbukumbu ni mzozo sasa kama uko vijijini watu wanaoana na kuachana kila leo.

countries-with-lowest-divorce-rates.jpg

countries-by-highest-divorce-rate.jpg
 
When two people are under the influence of the most violent, most insane, most delusive, and most transient of passions, they are required to swear that they will remain in that excited, abnormal, and exhausting condition continuously until death do them part. ~G.B. Shaw, Getting Married, 1908

Inakuwaje wanandoa pamoja na kuwa na matatizo mengi... kuachana inakuwa vigumu?Je ni kwa sababu ya watoto, mazoea au hali ya kuwa tegemezi?
Hebu tujadili......

Vyote hivi. Lakini hasa watoto na mazoea. Ni ngumu sana kuanza upya nadhani.......

Waweza kuongeza na umri, mkiachana choka mbaya utakwenda wapi? Ni mtizamo tu....
 
Vyote hivi. Lakini hasa watoto na mazoea. Ni ngumu sana kuanza upya nadhani.......

Waweza kuongeza na umri, mkiachana choka mbaya utakwenda wapi? Ni mtizamo tu....

Hiyo choka mbaya... sijui kama ni ishu.Kuna watu wanakaa mwaka au miwili na ndoa yao kuyumba vibaya mno na bado wanasita kuachana.
 
WoS:

Je hii mada inaku-touch kwa namna fulani? Just Checking lol. Kinamna.

Hii mada nimeileta baada ya kuangalia programme moja ya TV. ..na kuona ugumu wanaoupata wanandoa katika kuachana japo wana matatizo makubwa.
 
Hiyo choka mbaya... sijui kama ni ishu.Kuna watu wanakaa mwaka au miwili na ndoa yao kuyumba vibaya mno na bado wanasita kuachana.

That's exception to the rule. Na dini za kikoloni zachangia....lol. Sababu ikiwa nzito nikashindwa kuivumilia, sina watoto, two years in marriage, naanza mbele kirahisi tu......
 
TZ kuachana sio raisi kwa sababu wanawake wengi hawana kipato na wanategemea wanaume kwa maisha yao, kwa hiyo ni bora wa fight mpaka mambo ya tulie...

ukiangalia sasa hivi wanawake wengi wanafanya kazi na rate ya kuachana imeongezeka

mfano UK kuna wa kina dada wengi wa kiTZ wanamakaratasi basi kila siku wanawafungia wanaume zao nje na kuwatoa ndani ya nyumba, vitu kama hivi hawawezi kuvifanya TZ kwa ajili wao ni tegemezi, kwa hiyo kama unataka kujua the true colours za wanawake waTZ wape hela
Hapo ulivyoongea ni kweli kabisa, rate ya watu kuachana sasa hapa tz ni kubwa mno. Watu wanafunga ndoa lakini baada ya muda tu wanaachana, nafikiri na hii ya wanawake kufanya kazi nayo inaweza kuwa sababu mojawapo. Maana ukiangalia ndoa za zamani zilidumu miaka na miaka kwa kuwa mwanamke alikuwa tegemezi, tofauti na sasa baadhi ya wanawake wanainuka kiburi maana hawataki tena unyanyaso, haki sawa kwa wote. Hivyo akiona mitikiso ndani ya ndoa anaamua kujitoa mapema maana hata yy anaweza kulea familia yake(watoto) maana kama pesa anazo.
 
Kwa hakika mwanzo mzuri uko katika uchaguzi mzuri, atakayefanya uchaguzi mzuri atakuwa ameweka mguu wake katika njia ya bora na furaha na ndoa itakuwa na furaha na amani daima.

Mwanamke na Mwanaume wanapaswa kuwa kwenye misingi sahihi ya kuchaguana. Mume au Mwanamke ambae akiongoka kwa uongofu wake basi maisha yao ya ndoa yatakuwa mepesi yenye baraka, na hivyo kuwa na familia njema yenye mapenzi, huruma na mambo mazuri.

Baadhi ya watu wanaangalia ndoa kana kwamba ni mkataba wa kibiashara, mshindi na mwenye kupata faida ni yule anayepata kiasi kikubwa cha mali, bila ya kujali matokeo yake mabaya yenye kuangamiza familia, hawajali tabia wala Iman zao, lakini wanachojali zaidi ni kiasi gani cha mali au fedha alichonacho mtu.

Hii haina maana kuwa mimi nataka watu kwachagua mume au mke fukara, lakini kumbuka kuwa fukara mwema ni bora kuliko tajiri muovu. Kama ambavyo mwanamume ana haki ya kuangalia tabia ya mwanamke. Ni vyema pia mwanamke aangalie iman ya kijana anayekuja kuposa hali yake na tabia zake.

Kwani jambo la ndoa halimalizikii kwa Mume na Mke tu, bali Ndoa ni muunganiko wa Koo mbili tofauti... Ili kuleta heshima kwenye jamii uvumilivu na kusameheana na kutofanyiana hiyana kunaitajika sana, ili kuepusha magomvi na kutoelewana kutakapo pelekea watu kuachana.

Upendo na maudhi, Vinapokutana basi mapenzi hayakai huondoka.
 
Baada ya kutafakari kwa makini nimepata wazo ambalo linaweza kusaidia. Zianze ndoa za mikataba mifupi mifupi (kama vile lease). Mkataba ukiishi kila mtu anaanza vyake au kama wanataka kuendeleza wanaingia tena mkataba mpya wa miaka mitatu.

...Za10, umetafakari nini hatma ya watoto wataozaliwa ndani ya ndoa hizo?
 
Vyote hivi. Lakini hasa watoto na mazoea. Ni ngumu sana kuanza upya nadhani.......

Waweza kuongeza na umri, mkiachana choka mbaya utakwenda wapi? Ni mtizamo tu....

Watu wanaogopa kuachana kwa vile wanaona ugumu kuanza upya na wengine? Ni kweli hiyo? ingekuwa hivyo watu wangekuwa na nyumba ndogo? Au ni ugumu upi unaongelewa hapa?
Au ni ile ya kusema better the devil u know than the angel you dont know?
 
Binafsi naunga mkono heading ya thread MOJA KWA MOJA!swala la msingi ni kumshirikisha mungu katika kumpata mtu wa type yako,mnaeendana,mnaevumiliana.ukikosea kuchagua BASI TENA.kila mnapogombana watu watawashaurini 'VUMILIANENI JAMANI,NDOA NDIVYO ZILIVYO'

Hommie hongera ; huu ni ujumbe mahsusi kwa WOTE MNAOFIKIRI KUWA NDOA NI GUNIA LA MCHELE!

Unapooa/ ama kuolewa unajitolea kushre ya kwako na kupokea ya mwenzio; mema kwa mabaya! Ukiliewa hili linkusaidia.

mnaosema mngependa ndoa za mikataba; mmeifananisha ndoa na bidhaa dukani ambayo unainunua ukiihitaji si basi mbakie na kaina eliza ama wale sungu sungu wa Sinza makaburini?
 
Eglypz; ni wazi nchi za kiafrika ukiondoa Libya hazikuhusishwa hapa ningetaraji kuziona South Afrika na nigeria na Botswana walau katika kundi mojawapo!
 
Hakuna cha ze dataz.. ndiyo ukweli.... huko majuu mtu anaweza kunyanyuka na sanduku lake huyooooo akaishia.Bongo..watu wanang'ang'aniana utadhani luba! Mtu ataondoka aende wapi?lol!
Sbbu ni nyingi zinazo sbabisha watu wang'ang'aniane wakati mwingine ni watoto, wakati mwingine utegemezi kama mke anamtegemea mume kwa kila kitu ataenda wapi zaidi ya kuvumilia tu?!, na wakati mwingine mtu hufikiria kuzaa pembeni ana amua avumile azae na mtu mmoja? na wakati mwingine mazoea mtu umekaa naye miaka unafikiria jinsi ya kuanza upyaa na mtu mpyaa na nyingine nyingi tu!
 
Baada ya kutafakari kwa makini nimepata wazo ambalo linaweza kusaidia. Zianze ndoa za mikataba mifupi mifupi (kama vile lease). Mkataba ukiishi kila mtu anaanza vyake au kama wanataka kuendeleza wanaingia tena mkataba mpya wa miaka mitatu.

Hehehe..... KULA 5 Z10. Hilo ni wazo langu haswaaaa kama ikitokea nikampata mwenza ambaye nataka tufunge ndoa. Sitaki kabisaaa ndoa ya 'TILL DEATH DO US APART' mh mh.. Ni mkataba kwa kwenda mbele. Atakuja huyo padri kutuvalisha pete tu, lakini katika yale maneno yao yale.... hicho kipengele kitolewe. Manake ndoa cku hizi zimekuwa ndoano.
 
Inakuwaje wanandoa pamoja na kuwa na matatizo mengi... kuachana inakuwa vigumu?Je ni kwa sababu ya watoto, mazoea au hali ya kuwa tegemezi?
Hebu tujadili......

From african point of view, sababu kubwa ni : FINANCIAL INSECURITY. Most women (no offence) hawana uwezo wa kujikimu kwa sababu ya mfume dume unaotamalaki na hivyo, hata kama waume zao wanawafanyia madudu, hawawezi kuondoka na kudai talaka.

Si kama wanawake wa Ulaya ambao kudai divorce nje nje
 
Back
Top Bottom