Dada, kwa kukusaidia, kwanza kabisa NAOMBA UDEFINE "UWOKOVU" WA HUYU RAFIKIYAKO, ni wokovu wa aina gani according to you, ameokokaje, anasalije na anasali wapi etc. hapo ndo utaeleweka kwa upande wangu. kwanini nasema hivi, ni kwasababu just because of your statement "waokovu", ume spoil waokovu wengine wote kuonekana kama ni wazinzi tu, hivyo kuna umuhimu wa wewe kueleza ni mwokovu wa vipi na wa wapi etc. mtu aliyeokoka hawezi kufanya kitu kama hicho, kama ameokoka na kukaa kwenye kanisa linalofundisha mafundisho ya kimungu. kama atafanya hivyo, Mungu atamshughulikia fasta fasta ili kuokoa kondoo wake. Mungu wetu ana huruma sana lakini pia hadhihakiwi....so, labda ungesema "NI MWOKOVU ALIYERUDI NYUMA NA KUACHA WOKOVU" ndo maana anatamani uzinzi. mtu aliyezaliwa kwa roho tamaa za mwili huwa zinaunguzwa na nguvu ya Mungu, Mungu anamsaidia kushinda dhambi kwasababu hatushindi dhambi kwa nguvu zetu sisi bali kwa uwezo wa Mungu ndo maana Yesu alikuja akafa kwaajili ya hilo, sisi tulishindwa.
kama ni wewe lakini umetumia tu jina la "rafiki yangu", naomba nikupe ushauri, kama ulishawahi kuokoka, ndoana kubwa kuliko zote ambazo shetani huwa anatumia kuwanasa watu waliookoka ili warudi nyuma na yeye awamalize, ni ndoana ya mapenzi kama ulivyoeleza hapa. nakushauri usifanye icho kitu, hauwezi kushinda kwa nguvu zako, mwombe Mungu aondoe hiyo kitu moyoni, mwambie uyo jamaa aachane na wewe kwasababu atakuangamiza roho yako muda si mrefu, hata kama ulishapokea vitu, hata kama ulishakubali kukiss au kufanya naye kitu lakini haujafanya, USIENDE KUFANYA, KUMBUKA, KUNA WATOTO WAWILI WA BABA MMOJA WALITUMWA, MMOJA AKASEMA SITAKI ILA BADAYE ALIJIHISI VIBAYA AKAENDA, MWINGINE ALISEMA NAENDA LAKINI BADAYE HAKWENDA KABISA, BABA ALIKUJA KUMPA IJARA YULE ALIYEENDA HATA KAMA HAKUSEMA KUWA ATAKWENDA NA YULE ALIYEKUBALI LAKINI HAKWENDA HAKUPATA KITU. so, hata kama ulikuwa umefika mbali, stop it righ there, mwambie jamaa umeamua kutokumsaliti Mungu wako kwa dhambi kama hiii, hivyo aende mbali na achukue vitu vyake vyote kama akitaka. NDOA NA IHESHIMIWE NA WATU WOTE NA MALAZI YAWE SAFI, nakwambia, kati ya vitu ambavyo unaweza kuja kujilaumu badaye ni kuiba ndoa ya mtu, Mungu atakupiga vibaya sana hadi utaaibika. mtu huvuna kile alichopanda ujue, kama wewe unaiba mume wa mwenzio, na wewe kuna siku utaibiwa mara mia na utaumia sana, kama wewe unalala na vitoto vya shule na watoto wako watakuja kulalwa na watu wakati wako tu shule, chochote ufanyacho utalipwa tena kwa kibaba cha kujaa hadi kumwagika.
dhambi zote ni sawa, lakini Mungu amedhihirisha kabisa kuwa dhambi ya uzinzi ni special sin kwasababu haifanyiki nje ya mwili bali ndani ya mwili..hivyo adhabu yake huwa ni kubwa, utaachwa na Mungu na shetani atakugaragaza hadi utalia Mungu atakuwa haonekani kwako, huwezi jua ni kwanini hadi leo upo, ni neema ya Mungu, Mungu AMEFNAYA MANGAPI KWENU HADI MFIKIE HALI KAMA HIVYO, Mungu amewafanyia mambo mengi mno mazuri, je umsaliti kwa kitu kama hicho haujui kama Mungu anakuona? unaamua kwenda kwa shetani hivihivi wakati Mungu anakuona? nakushauri ubadili mwelekeo haraka kabla mambo hayajakuharibikia, kama utafanya shingo yako ngumu, itavunjika na hakutakuwa na mtu wa kukupatia dawa...wakati mlango ungalipo ingia kwasababu kuna wakati utafungwa na utatafuta malango hautauona.
maadamu neema ya Mungu bado iko juu yako itumie, kwasababu kuna wakati itakapoondoka utatafuta hautaiona. wakati upo mzima wa afya na kila kitu mshukuru Mungu kwasababu kuna siku badala ya kukaa hapo kwenye computer uandike kitu utajikuta umelala kwenye kitanda ICU hata computer wala JF haipo, na hakuna wa kukufariji na Mungu umeshamwacha na kumsaliti. mwogopeni Mungu enyi ncha zote za dunia, yeye ni Mungu anayestahili kuheshimiwa na kila kiumbe. Mungu akusaidie.