'Marshall Plan' - Restoration and Recovery Plan for Tanzania

'Marshall Plan' - Restoration and Recovery Plan for Tanzania

Rev,

Kama unaweza, naomba unitumie nakala ya article yako hii katika PDF au word format niweze kuisoma kwa makini. Unatoa mawazo mazito sana lakini kwa vile ni ndefu sana, nashindwa kuifuatilia yote. Ama sivyo, nitaweza kuikopi hapa na kuinganisha mwenyewe ukishaikamilisha.
 
Mchungaji,

Je watakusikiliza,watakubeza tu,.Mie nina mpango wa kukata tamaa,wiki hana nilisikia wana mpango wa kujua humu JF ni nani ni nani na huyu ni nani na anafanya shghuli gani.Personal wameshaniumia E-mail..

Gembe,

Unajua hii si mara ya kwanza wewe kuyasema haya maneno, sentenso kwa senteso, je ni nani huyo anayekutafuta au kukunyanyasa? je hukuwaambia wasome ile thread yangu ya Mwamtafuta Mchungaji, ni mimi wajue Mchungaji ni nani?

Je umepokea zaka na msaada kutoka kwao au wanajaribu kukununulia shamba na kukupa zawadi?
 
Rev,

Kama unaweza, naomba unitumie nakala ya article yako hii katika PDF au word format niweze kuisoma kwa makini. Unatoa mawazo mazito sana lakini kwa vile ni ndefu sana, nashindwa kuifuatilia yote. Ama sivyo, nitaweza kuikopi hapa na kuinganisha mwenyewe ukishaikamilisha.

Mwalimu,

Nikiimaliza nitakutumia kama word document, it is work in progress....
 
Mimi ngoja niwaze tofauti kidogo na Rev

Tatizo mimi ninaloona ni kua sisi wengi wetu ni kujaribu fikiri matatizo yetu ni kutokana na muono mbovu ama ufupi wa uelewa wa viongozi wetu kuhusu matatizo ya nchi yetu na kujaribu kutumia nguvu nyingi kuwapa plan B na namna ambayo ingefaa kuchukuliwa.

Ukweli ni kwamba hawa viongozi wana uelewa mkuu juu namna mbinu na mikakati ya kututoa ktk umasikini. Sasa basi kwanini hawafanyi hivyo

Ni jaribio hatari kwao na falme zao za kimwinyi kujaribu kumletea masikini maisha bora,kwao ktk hali hiyo ya umasikini ni Bora zaidi ya mara mia kuliko kuwaendeleza wananchi na hatimaye utawala wao kupeana vijiti kua ktk hali tete.

Yani kwao kumuendeleza masikini ni sawa na kumpa adui yako silaha makini na mbinu maridadi.

Wao wana endekeza mfumo huo ili wapokezane madaraka watoto wajukuu,vitukuu,vining'ina.
Na ukitaka kuangalia kwa makini na kuunganisha nukta ni kwa nini bodi ya mkopo pale wanataka lazimisha mtoto wa masikini lazima asome Engineering?? Maana akisoma masomo mengine ama asipate kabisa mkopo ama wampe 50% sasa hizo zingine atatoa wapi??.
Tatizo la TZ sio mipango wala sera ,tatizo ni patriotism tupiganieni patriotism kwanza.
 
Mkuu Rev. Kishoka,

Unajua hata yule mzee marehemu George Marshall ambae ndie alieandaa huo mpango ulobatizwa hilo jina lake, angeuona huu wa kwako angekupa waleu alama 50%, kwanini?

Mpango wako ni mzuri lakini unakosa namna (strategy) ya kuuanzisha au kuutekeleza au (implemetation).

Kama tujuavyo katika historia ni kwamba ile Marshlall Plan ya Ulaya ya wakati ule iliokuwa imeharibiwa na vita kuu vya dunia iliundiwa hio "recovery programme" ili isimame yenyewe na ndio maana mpaka leo nchi kama Ugiriki ambayo ilikuwa haina kitu walipewa hata ng'ombe kama mitaji.

Ulikuwa ni mpango ambao ulilenga kwa kila nchi ambayo iliathirika kwa vita ile.

Sasa inasikitisha sana kwamba Tanzania iliathirika na ukoloni na baadae baada ya miaka zaidi ya 47 ya uhuru wake, bado athari za kikoloni zinatutawala na nnakupongeza mheshimiwa Rev Kishoka kwa kujitahidi kuandika haya maana yanatukumbusha kwamba Tanzania bado ni maskini wa kujitakia.

Nimeipenda Kishoka Version ya Marshall Plan yako lakini nimeona kwamba bado inahitaji maeneo yafuatayo kuangaliwa kwa undani na utaniambia kama umeonglea vya kutosha.

1. Kilimo- Je utazuia vipi bidhaa mbalimbali za vyakula kutoka nje kama kuku, maziwa, na unga na kukuza ubora wa vyakula vya kutoka Tanzania. Kwa mfano maharage kutoka Rukwa yatatayarishwa vipi ukizingatia packaging, labelling na hadi kifike katika duka kubwa la shoprite?

Umezungumzia viwanda vya uzalishaji lakini unakumbuka baadhi ya majengo ya viwanda vilivyokuwepo huko miaka ya nyuma vinaweza kufufuliwa na kusukwa kwa mitambo mipya ya kisasa na kutoa uzalishaji na ajira kwa vijana wa kileo?

Kwa ujumla ni kwamba mheshimiwa raisi wa sasa alikuwa na Marshall Plan ya wananchi kwamba amekuja kuleta mabadiliko makubwa na hatimae ameshindwa kutekeleza hayo.

Sasa hii Marshall Plan yako inabidi ibebane na Marshall Plan ya chama kingine cha siasa ambacho kinahitaji kuwa makini "strategically" mwaka 2010.

Watanzania lazima waelewe kwamba dunia inabadilika na watu wanabadilika. Haiwezekani kwamba walewale watu waliopiga kura ya asilimia 80 mwaka 2005 ndio hao hao leo hii watapiga kura hizo hizo, ni lazima sasa watu tuanze kuwa na "second choice" kwa chama kilichopo madarakani na tujifunze kutanabaisha wale wanasiasa walipo kama wabunge.

Bila hivyo tutaendelea kuwa wajinga milele.
 
Waungwana,

Marshall plan ya Mchungaji si "Fikra za Mwenyekiti" ambazo zilikuwa absolute and omnipotent.

Marshall plan hii ni kutoa changamoto kwetu sisi ambao ndio Taifa la sasa kujikimu na kujikwamua ili Watoto, Wajukuu, Vijukuu na zao 7 baada yetu wanufaike kwa matunda ya msingi bora tulioujenga.

Ndiyo nimekuwa pioneer hapa ndani lakini haina maana kuwa ninachoandika na kufikiri ni changu pekee.

Marshall Plan ya Mchungaji ni yetu sote na kama frame work na blue print ndiyo nimeanzisha, details and specifics zinahitajika kwa kila mtu. Anzia kina Bin Maryam waliopotea, Kahangwa, Nyambala, Richard, Mwanakijiji, Mpaka Kieleweke, Kada Mpinzani, FMES, Kuhani, JMushi, Madela wa Madilu, Susuviri, Koba, Game Theory, Kibunango, Steve D, Nyani Ngabu, Mkandara, Jasusi, Mpanda Merikebu, Bi Kirembwe, Mama, Asha Abdallah, YNIM, na wengine wote, hii ni kazi ya Ushirika na ni jukumu letu wote kuchangia na kuunda Marshall Plan ya Tanzania.

Ikiwa CCM, CUF, Chadema, TLP na Watanzania kwa ujumla wataona Marshall Plan yetu ndiyo njia ya kweli kujikwamua kutoka Umasikini, ndiyo iwe faraja yetu.

Kitu kimoja ambacho JF member wengi hawakijui na wanakipuuzia ni ile fursa kubwa tuliyonayo katika kulijenga Taifa letu.

We have the greatest opportunity to have solid and massive contribution to our country future.

Si suala la kupiga vita ufisadi tuu, bali inabidi tuanze kutoa solutions na njia bora za kutatua matatizo yetu ili future generation za Tanzania, zisiinshie kwenye Unyonge.

The time is now for us to work collectivelly. We need people to brainstorm to offer solutions and not always think how to criticise.

Challenge aliyotupa Allien, nimeichukua moyoni kwa kuwa nimeshalaumu sana, next thing ni kuanza kutoa njia za kusahihisha.

Sitegemei kuwa ninachoandika ni infinite na final, kila mmoja wetu anajukumu la kuingia na kuchangia, kujenga Taifa letu bila kujali tofaui zetu.

Adui wetu si wa Chadema pekee, ni wa CCM wenyewe, TLP, CUF na hata wale ambao hawana Chama.

So join me in the struggle and offer simple and workable solutions!
 
Rev. Kishoka,

Nakupata vizuri sana mkuu lakini mimi hapa sina mchango ktk marshal Plan hata kidogo ikiwa kiwanja hiki cha Tanzania bado hakijapatiwa kibali cha kujenga hayo unayokusudia. Ni mawazo mazito sana ulotoa lakini mkuu binafsi nayaona kama vile tunataka kujenga daraja toka Dar hadi Zanzibar..

Sii kwamba haiwezekani! - Inawezekana sana, lakini hii ni ndoto ya mchana kweupe hasa nikizingatia kwamba sasa hivi nchi za Kiafrka zinaongozwa na wakoloni weusi...
Sasa fikiria wakati wa mkoloni mtu mweusi aje na Marshall plan kuhusiana na Utawala wa mzungu ambaye kwanza alituona sisi ni nusu binadamu tuna kasoro fulani ya Ufahamu..Tazama Nigeria mkuu huko jimbo la Delta yaani viongozi wanakunya pale wanapopata riziki zao, hivi kweli hawa viongozi wa Nigeria hawaoni hali za wananchi wa sehemu hiyo...ni marshal plan ipi hawa wananchi wanaweza kuipeleka Lagos ikasikilizwa kwa fikra huru!
Tazama Sudan, Somalia, Zimbabwe, Egypt, Gabon, Siera Leone, Chad yaani kila mwaka wakoloni weusi wanazidi kuongezeka Afrika...what's going on?

Na ajabu ni kwamba hawa marais wetu na viongozi wake ni matajiri kuliko hata viongozi wa nchi zilizoendelea na bado wanataka Utajiri zaidi!..
Sijui mkuu wangu sijui, lakini hata hivyo nimechukua nakala ya maelezo yako nitayapitia taratibu kwa wakati na nafasi yangu lakini above all mimi naamini kwamba before all that ni lazima turudi nyuma tuone mababu zetu walifanya nini!...
Ni umaskini uliowasukuma kutafuta UHURU wa nchi zetu lakini baada ya miaka 40 au 50 Umaskini huo huo umezidi hata kiasi cha kusema AFADHALI ya MKOLONI!..

Hivyo hatua ya kwanza ni jinsi ya kujikwamua toka kamba hizi za shingoni!..tumegeuzwa mbuzi malishoni mkuu wangu! Hatua ya kwanza ni kuunda Upinzani wa nguvu..Nadhani ni bora zaidi tukiziweka nguvu zetu kuunda mkakati kwa vyama vyetu vya Upinzani, kisha tuwakabidhi mawazo yako (kama hakuna marekebisho) ambayo yatakuwa YAMINI yao kwetu wananchi kuwapa kura zetu...
 
...Kishoka ni vizuri kuwa na plan za maendeleo lakini bila kuwa na nchi inayozalisha na wananchi wenye income/kazi ambao watakulipa Tax ili kutekeleza hizo programs huoni kama net product ni zero hapo? tatizo la TZ ni hatuzalishi na wananchi hawana kazi wala income yeyote,nafikiri tuna plan zote tena nzuri sana kuanzia kujenga highways ,vyuo vikuu mpaka madaraja ya kubembea lakini pesa iko wapi?hakuna mkato lazima tuzalishe ili tuendelee huwezi kutekeleza programs zote hizo kama wananchi wako hawana kazi/income na hawalipi kodi na hawana any purchasing power,angalia state kama Idaho ni matajiri sana kwa sababu ya kulima viazi na vitunguu tuu...mfano nasikia Tabora wangeamua kuwa serious na kuzalisha asali tu wangeweza kulipa nusu ya kodi ya bugdet nzima ya TZ maana wana hiyo potential na soko liko wazi sana nasikia huko Asia,jiulize mikoa mingapi ina potential kama hizo kuanzia kilimo mpaka viwanda
 
Kishoka ninakupata, ninakupata mkuu
endelea kutumwagia plani, binafsi ninakubali kwamba tunapozungumzia mabadiriko tunazungumzia kitu dynamic na progressive, na mabadriko hayo yataanza tu pale mtu unapotambua kwamba unataka kubadili kitu gani, au kwa lugha nyingine ni kwamba unataka kufanya kitu gani mbadala!. kwa hii plan aliyotengeneza Rev. Kishoka bila shaka ni hatua ya awali ya kutambua tatizo na kapendekeza njia ya kuondoa hilo tatizo.kwa hivyo ni vyema sisi wadau hapa JF tukaviangalia vipengele vya Rev Kishoka kimoja baada ya kingine na kukosoa,ama kuunga mkono ili hatimaye tukubariane katika plani nzima.
binafsi naichukulia hii plani very serious,kwa sababu critcism ya situation peke yake haitoshi, bali kuunganisha nguvu ya mawazo na vitendo ili kuondoa tatizo
wahenga walisema "ADA YA MJA KUNENA , UUNGWANA NI VITENDO!!"
 
From Mkamap
"...Tatizo la TZ sio mipango wala sera ,tatizo ni patriotism tupiganieni patriotism kwanza"

Mkamap
Patriotism au kwa kiswahili uzalendo unapatikanaje au unapandikizwaje mioyoni mwa watanzania?
 
From Mkamap
"...Tatizo la TZ sio mipango wala sera ,tatizo ni patriotism tupiganieni patriotism kwanza"

Mkamap
Patriotism au kwa kiswahili uzalendo unapatikanaje au unapandikizwaje mioyoni mwa watanzania?

Mkuu Invincible,

Hii ni nukuu kutoka kwa Charles De Gaulle

"Patriotism is when love of your own people comes first; nationalism, when hate for people other than your own comes first."
~ Charles de Gaulle, General


Sasa hapo anamaanisha kwamba kama wewe ni kiongozi unatakiwa uone na kutatua matatizo ya nchi na wananchi wake.

Pia kila mara kusisitiza wananchi kuipenda nchi yao hata kwa kuhakikisha wanatundika bendera katika nyumba zao.

Na hio ya mwisho inajieleza yenyewe- wakoloni ndio wa kuangaliwa kwani bado wapo na wanakuja na nyimbo nzuri za misaada, mikopo na midubwana mingine.

Kwa hio, kiongozi wa nchi kazi yake ni kusema kwamba kuanzia sasa nataka iwe hivi na itakuwa hivi na mwisho wa kila hotuba aseme God bless Tanzania na kuonekana ameshika moyoni kwake.

Kiongozi wa nchi akifanya hivyo watu wataona na watafuata kila asemalo na kutekeleza na neno UZALENDO litakuwa na nguvu.
 
When are we going to stop self doubting? All the existing plans were created by others for us, not by us!

Je tunajisalimisha hata kabla ya kuanza kujaribu? Hii plan ni yetu,si ya hao walioko madarakani au washauri wao.

Plan hii inajengwa kwa matakwa yetu kama wananchi, kwa kuangalia mazingira yetu na kwa manufaa yetu. Tukianza kuwa na mashaka kuwa mbona tuna plan nyingi nzuri tuu, basi ina maana tunasalimu amri na kuruhusu waliotuangusha waendelee kuboronga.

Ukiangalia hii plan, aya nne za kwanza zinazungumza kwa Mtanzania na kumsihi ajichunguze nafsi na ajiulize anataka maendeleo ya namna gani na ni yapi aliyoyaona. Utangulizi unamwambia Mtanzania apime kwa makini kauli za wanaokuja kujiuza kutaka dhamana ya kuliongoza Taifa. Utangulizi unampa Mtanzania tahadhari na kisha unaanza kubadilika kwa kumfundisha na kumfahamisha Mtanzania kile kinachowezekana ambacho Mtanzania amedanganywa kuwa hakiwezekani.

Tumezoea kuambiwa kuwa hili na lile haliwezekani, ni gharama sana, Serikali haina pesa, itatuchukua muda mrefu na visingizio vingi tuu. Na kama utamaduni wetu, tumekaa chini na kukubali wala si kwa shingo upande tena bali kifua mbele kuwa tunayoyataka kamwe hayatawezekana.

Sasa kama tuliweza kununua ndege ya Kifahari, Rada ya Kifahari, kutumia pesa kulipia madeni hewa na kuhalalisha uhujumu, je hizo pesa zilitoka wapi? mbona tulilipia ndege haraka haraka bila kusita au kujuta? Mbona mkataba wa Richmond tuliulipia kwa haraka bila kujali mayowe kuwa kuna ubatili?

Kinatushinda nini kuhakikisha kuwa kila kata na tarafa ina shule ya msingi na zahanati, kila wilaya ina shule za Sekondari mbili, hospitali, chuo cha veta, Mkoa una hospitali kuu, chuo kikuu, kila kon kuna umeme na maji na barabara zetu, reli na vyombo vya usafiri majini ni bora na vya kuaminika?

Je ni ukosefu wa pesa au ni ukosefu wa kufanya yale ya msingi na lazima na kuishia kufanya na kutumia hazina kwa yale yasiyo ya msingi?

Sasa ukimwonyesha Mwananchi na kumfundisha haki yake ya msingi na kumtahadharisha kuwa si kweli kuwa hawezi kuwa na Zahanati, Hospitali, Shule, Chuo, Umeme, Maji na Barabara nzuri, je hamuoni huo ni mwanzo mzuri na msingi bora wa kuondokana na utawala mbovu ambao unamnyanyasa Mtanzania na kumfanya awe Mnyonge na Masikini wa daima?

Hivi ukimwambia Mtanzania ukweli kuwa Dhahabu yetu tulioruhusu Mgeni aje kuigema na kuiuza kwa niaba yetu tunachopata ni Shilingi Elfu Tatu lakini huyo mgeni anakomba Laki tisa na sabini elfu, hiyo haitatosha kumwamsha Mtanzania na kuhoji uzalendo wa mwakilishi na Serikali yake?

Inasikitisha tunapoanza kwa kukata tamaa. Huku ni kuwapa mwanya wale ambao wanalidanganya Taifa kuwa wanataka kutuongoza na kutupa maendeleo huku wakitumia vitisho na sababu za kijinga kuwa Tanzania haiwezi kujitegemea au kuwa na Shule kila kona.

Marshall Plan hii ni yetu, kwa utashi na mawazo yetu. Si kwa kuiga Great Leap, si kwa kupangiwa cha kufanya na Wafadhili, si ya Kikundi haramu kinachotuibia kila siku.

Hii ni yetu, hii ni FUBU, For us By us! Achaneni kuwa ma-Tomaso, jiaminini, kuweni na tumaini kuwa tunaweza kufikisha mbiu hii kwa Mtanzania na safari mpya ya kujenga nchi itaanza!
 
inaendelea...


Maji na Mazingira

Maji ni kitu muhimu katika Uhai wa Taifa. Maji yanahitajika kwa mwili wa binadamu, kurahisisha ukuaji wa mazao, kuendesha viwanda na matumizi mengine ya kawaida na hasa usafi. Kama nilivyosema awali, Tanzania tuna bahati kubwa sana ya kuzungukwa na Maziwa makubwa matatu, maziwa ya wastani wa kati karibu manne, mito mikubwa karibu sita pamoja na mabwawa na bahari.

Mjerumani alipokuja Tanganyika 1885, aliweka mpango wa kilimo "masterplan" ya kulisha Afrika Mashariki na Kati kwa kutumia bonde la Wembere ambalo liko Singida jirani na Tabora. Ikiwa MKoloni aliona rutuba hiyo na kuona vianzio bora vya maji ili kuhakikisha umwagiliaji unatokea, inakuwa je sisi tunashindwa kujitosheleza chakula huku tuna maji na vianzio vya maji tele?

Kwa nini mji kama Dar Es Salaam unaendelea kupanuka na kukua lakini mfumo wa maji ni ule wa Mjerumani na Muingereza? Je viwanda vyetu vinaposhindwa kufanya kazi kutokana na kukosekana maji, hasara ni ya nani? Je wananchi wanapougua magonjwa kama Kipindupindu, linaloumia si Taifa?

Kwa wastani, Mtanzania wa kijijini hutembea si chini ya kilometa mbili kwenda kwenye mto au kisima kuteka maji. Umbali huu kwenda na kurudi utamchukua Mtanzania huyu si chini ya nusu saa kubeba ndoo moja. Sasa kama Mtanzania huyu inambidi aende safari tatu au nne kwa siku mtoni au kisimani kuteka maji, hatuoni kuwa tunaingia gharama za MUDA kwa mwananchi huyu kutumia masaa matatu ambayo angekuwa anafanya kazi nyingine au kujisomea na si kuhangaika kwenda kuteka maji au kukata kuni?

Wizara ya maji na Idara za maji zinapaswa kushirikiana na idara na taasisi nyingine kuhakikisha kuwa ile sera ya kumfikishia Mtanzania maji nyumbani kwake ifikapo mwaka 2025 inatimia.
Mapendekezo yangu ni Serikali kuweka fungu maalum kwa ajili ya mradi wa kusambaza maji, kuondoa au kupunguza kodi na ushuru kwa vifaa na pampu za maji na mashine za kumwagilia, kuhakikisha kuwa kila wilaya inalipa kipaumbele suala la maji kwa matumizi ya watu, maji kwa umwagiliaji na kuendesha viwanda na biashara.

Maji yanaendana na Mazingira. Vitu hivi vinashibana na vina tegemea. Suala la mazingira si kuhusiana na uchafuzi wa mazingira pekee (pollution) bali ni uratibu mzima wa kuhakikisha kuwa Uoto wa asili haupotei na kudumaa kutokana na matumizi mabaya ya ardhi na mazingira.
Dunia yetu sasa hivi inakabiliwa na kubadilika kwa hali ya hewa ambayo imesababisha ukosefu wa mvua, kuongezeka ukame na jangwa, kuongezeka kwa kina cha maji ya bahari, uchafuzi wa mazingira kutokana na mabaki ya kemikali za viwandani na matumizi ya mafuta, kupotea kwa misitu kutokana na biashara ya mbao na kuni, kupotea kwa viumbe hai na wanyama kutokana na kushindwa kuhimili mabadiliko ya mazingira.

Tanzania kwa kuwa bado tupo katika hatua ya kujijenga upya kama Taifa, tuna nafasi kubwa sana kuwa mabingwa wa hifadhi za mazingira kwa kuchochea msukumo kwa Watanzania kulinda mazingira na kudumisha usafi wake.

Mapinduzi ya Kijani yanawezekana sana Tanzania. Tunauwezo kwa kuotesha misitu mikubwa, kupunguza mmomonyoko wa ardhi na udongo, kupunguza takataka ambazo haziozi, kulinda vianzo vya maji, kutumia nishati za upepo na jua ili kupunguza matumizi ya mafuta na kusafisha maeneo ya mito na maziwa ambayo yanapoteza samaki na viumbe wengine kutokana na uchafu.

Tanzania ina bahati sana kuwa uzorotaji wa viwanda vyetu pamoja na kuwa kumelidumaza Taifa, lakini kunalipa Taifa fursa kubwa ya kuwa nchi yenye mazingira safi na mazuri kwa Wananchi wake hivyo kusaidia uimara wa afya, kuongezeka kwa uzalishaji mali na kuendelea kuwa kivuti cha utalii.
Kampeni za kulinda mazingira, kata mti panda mti, zitaendelezwa na kuongezewa fedha za maendeleo. Serikali itoe nafasi maalumu na ufadhili kwa taasisi na watu ambao wanabobea katika mambo ya mazingira na hata ubunifu wa uzalishaji mali kupitia mapinduzi ya kijani.

Wajibu huu wa kulinda na kusafisha mazingira utasukumwa kwa mamlaka za miji na vijiji chini ya uongozi wa Wizara na idara husika za mazingira na TAMISEMI.

Lengo ni kurutubisha nchi, iweze kuendelea kuwa na ardhi nzuri, maji mengi, afya njema na hivyo kukua kiuchumi.

itaendelea...
 
Mkuu Rev. Kishoka,
Maisha ya Mdanganyika hayatazami mbali zaidi ya riziki ya tumbo yaani SHIBE.. mtu mwenye njaa ama kiu cha maji mshikaji fikra zake kwanza ni kuondoa adha hiyo....
Hapa JF ni kundi ambalo tumebanwa haja kubwa na ndogo kwa mpigo..Tunahitaji kushusha mzigo huu kwanza kabla hatujafikiria vizuri mlo unaofuata, lakini sii wachovu wa mbinu za kutafuta kula!
Sasa unapokutana na makundi kama haya yaani wenye njaa kali na sisi ambao tunataka kushusha mzigo, vipaumbele vinagongana...Huu ni upande wa wananchi...safari ni ndefu mkuu kuwaweka watu hawa kitako wakapata kukuelewa... ndio maana unaona Bungeni wawakilishi wetu (walioshiba) huuchapa usingizi tu.. wafanyeje!..
 
Mkuu Rev. Kishoka,
Maisha ya Mdanganyika hayatazami mbali zaidi ya riziki ya tumbo yaani SHIBE.. mtu mwenye njaa ama kiu cha maji mshikaji fikra zake kwanza ni kuondoa adha hiyo....
Hapa JF ni kundi ambalo tumebanwa haja kubwa na ndogo kwa mpigo..Tunahitaji kushusha mzigo huu kwanza kabla hatujafikiria vizuri mlo unaofuata, lakini sii wachovu wa mbinu za kutafuta kula!
Sasa unapokutana na makundi kama haya yaani wenye njaa kali na sisi ambao tunataka kushusha mzigo, vipaumbele vinagongana...Huu ni upande wa wananchi...safari ni ndefu mkuu kuwaweka watu hawa kitako wakapata kukuelewa... ndio maana unaona Bungeni wawakilishi wetu (walioshiba) huuchapa usingizi tu.. wafanyeje!..

Hawa ndio hatuwataki! angalia matumbo yao, hivi kweli wanatokea vijiji gani? Huko wilayani mwao Utapiamlo na Kwashiakor ni kiasi gani? maana kama Mbunge amenona kiasi hiki, basi hata Wananchi wa jimbo lake wana NEEMA!

attachment.php
 
Kwa wote mnaosubiri kwa hamu hitimisho la Marshall Plan ya Mchungaji, nitaimalizia wikiendi hii na kuwapa attachment muichape muisome, ikosoeni, ongezeeni, punguzeni na kisha ikiridhia kila mtu, iwe tamko letu JF kulijenga Taifa letu.

Samahani kwa kuchelewsha kuikamilisha!
 
Rev. Kishoka,
tana hapo umesema haswaaaa!
Sasa nenda kawambie wananchi kuwa Obese ni maradhi!...ama watu hao hapo juu wana matatizo ya kiafya!...
Ukishinda vita hiyo labda awepo mzungu kushinikiza hoja laa sivyo utaambiwa huyu naye katoka Ulaya basi yeye ndio anajua kila kitu..Hawa jamaa Afya tupu, jasho jebamba linawatoka hata bila kukimbia leo anasema ati wagonjwa!..
kazi sio ndogo mkuu wangu lakini tutafika tu!
 
Rev. Kishoka,
Mkuu vipi mbona umeniacha pale Ubungo kituoni?... nasubiri mkuu nasubiri vitu kama ujuavyo mimi hupenda sana vitu kama hivi..
Maoni yangu yatakuja tu baada ya kupokea mkanda mzima..Shusha manyanga mkuu shusha.... tunayahitaji kesho.
 
Kwa wote mnaosubiri kwa hamu hitimisho la Marshall Plan ya Mchungaji, nitaimalizia wikiendi hii na kuwapa attachment muichape muisome, ikosoeni, ongezeeni, punguzeni na kisha ikiridhia kila mtu, iwe tamko letu JF kulijenga Taifa letu.

Samahani kwa kuchelewsha kuikamilisha!

..rev,

..mpangilio mzuri kabisa wa maoni.

..sasa,ili iwe marshall plan inahitaji projections za mapato na matumizi. pia inahitaji time frame ya utekelezaji na kubainisha wasimamizi,watendaji,wadau,n.k wakuu.

..nadhani wapo wataalamu au na wasomi wa kutosha humu watakao iboresha kadri itakavyowezekana, bit by bit mpaka iive!

nb:tanzania ina viongozi wachache sana, wengi ni wahuni,wezi,wababaishaji na wabinafsi.
 
Back
Top Bottom