Mkuu katika kipengele hiuki nadhani ipo haja ya kuelezea vizuri unapozungumzia NYUIMBA.. kwa sbaabu serikali inaweza kuwa na majumba kwa malengo ya HUDUMA sio BIASHARA..
Nina hakika hakuna nchi duniani ambayo serikali yake haina nyumba hata iwe zile tunazoziita PROJECT!.. yaani kuwasaidia wananchi wasiokuwa na uwezo wa kununua ama kupangisha nyumba ktk bei za soko.
Hapa alikuwa anaongelea nyumba za kuishi viongozi na watumishi wa ngazi za juu, sio project wala mafleti ya Ubungo National Housing au Magomeni Quarters!
Anasema Serikali isiendelee kuwa na nyumba za viongozi.
Sasa sijui kama anakubaliana na uamuzi wa Mkapa administration kuuza nyumba za Serikali. Mimi nadhani ulikuwa sawa, japo utekelezaji wake ulikuwa wa kifisadi.
Mchungaji,
Uzee umenizidi, leo ndio nimeiona hii thread! Kwa kweli nimefurahi mno kuona kwamba umeweza kuketi chini na kututengenezea kitu kizuri kama hiki!
Sasa nasema hivi, lini utarudi nyumbani na kugombea uongozi ili tukuunge mkono kabla bwana God hajatuita?
Aidha, natoa changamoto kwa nyie vijana na wazee wenye kuunga mkono mawazo mazuri kama haya, na wale wote ambao mmekuwa mkitoa michango ya 'kimapinduzi' yenye dhamira ya kuliokoa taifa letu linaloelekea kusikoeleweka. Jana wakati namsikiliza Kubenea na leo niliposoma hii thread nikajua nchini tunao vijana wanaoweza kuliokoa Taifa letu endapo utakuwepo mshikamano wa dhati.
Tatizo lenu humu ndani kila mtu ana chama chake anachoshabikia! Mie ningeshauri muachane na vyama vilivyopo, unganeni kwa mawazo mazuri na dhamira ya kutaka kulikomboa Taifa letu. Wekeni mikakati na ikibidi anzisheni chama kipya kabisa chenye lengo la kuinusuru nchi. Mtaungwa mkono na wengi.
Bob Mkandara,
Shukrani kwa masahihisho. Nitarekebisha na kuainisha vyema.
Kinto,
Waraka huu unaanza kwa kumhoji Mtanzania, unamsukuma Mtanzania ajichunguze kwanza pamoja na kuwa matatizo makuu yanajulikana Uchumi na Uongozi.
Waraka unaendelea kumhiji Mtanzania ni maendeleo ya namna gani anayoyataka na kumuuliza matarajio wake.
Waraka unatoa tafrsiri rahisi kuhusu Uongozi bora, na kumrudia msomaji Mtanzania kumuuliza, je amefanya nini katika kutafuta kiongozi bora?
Waraka unahama kutoka kumuuliza Mtanzania kama anajijua na kuelewa umuhimu wa Uongozi na hasa Uongozi bora ili kuwa msukumo wa maendeleo na kuanza kupembua vigezo vya kumpa Mwananchi huyu maendeleo na hasa kujikwamua kibinafsi na kama Taifa kiuchumi.
Dhumuni la waraka si Sera, bali ni kumpa Mwananchi fursa ya kujiuliza afanyeje ili awe na maendeleo ya kweli na yale yanaoonekana kuwa ni Sera, ni mambo ya kawaida ambayo yalipaswa kufanyiwa kazi lakini hayafanyiwi kazi kutokana na Uongozi mbovu.
Mtanzania akishajua anachokitaka, na kuelewa kinachowezekana na kuamua kwa umakini Uongozi anaoutaka, safari ya maendeleo itafanikiwa.
Ndiyo maana Waraka huu ni kwa Mtanzania, si kwa Chama au Serikali.
Umenikumbusha tukio moja ilitokea kijiji cha Lugombo kata ya Ngonga, wananchi walimdai Diwani wao report ya mapato na matumizi ya kata.Badala ya kuwapa report hiyo yeye akatamka kuwa wale watu wametumwa na vyama vya upinzani,akafunga mkutano na kupanda pikipiki na mtendaji wa kata.Hiyo ndio hali ya uongozi ulivyo wa hovyo huko kyela.Waungwana,
Najua nimeandika kwa kirefu mawazo yangu na kuyawasilisha hapa kwenu ili muyachambue. Jambo moja, la muhimu ni hili, hakuna mpango wowote utakaoweza kufanikiwa kama uongozi na watendaji ni wabovu!
Hata kama hiyo master plan, manifesto au Marshall plan italetwa na Muumba mwenyewe, ikiwa tuna viongozi wabovu, kamwe tusitegemee kuona yaliyoandikwa na kupangwa yakitimilika.
Uongozi si mtu mmoja tuu, kosa lililotokea na Mwalimu Nyerere na mambo ya Azimio, Vijiji vya Ujamaa na Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea.
Waliokuwa upande mmoja na Mwalimu walikuwa wachache sana. Wengi walikuwa ni wafuata mkumbu huko nyoyo zao zilikuwa zinasubiri nafasi ya kutanua kama walivyoona wale mabwana DC wa Kizungu wakitanua na kujichana.
Tutakapo kuwa na viongozi wa kutosha wenye mwamko na changamoto la kuleta maendeleo, basi Taifa letu litapiga hatua. Kinyume na hivyo ni sawa na mbwa kutaka kung'ata mkia wake!
Any updates wadau mliousoma waraka?
Inaendelea...
Mfumo wa elimu wa Tanzania unabidi kubadilika na kuhakikisha kuwa tunajenga mfumo wa elimu ambao unachochea ubunifu, unarahisisha uzalishaji mali na unawiana na maendeleo yetu. Kuna haja ya kuachana na mfumo wa Elimu ya kufaulu na kuhakikisha kuwa kinachofundishwa kinaeleweka na kinaweza kutumika ipaswavyo na wanafunzi wote, kuanzia chekechea, shule ya msingi, sekondari, vyuo vya fani stadi na hata elimu ya juu.
Mkuu Rev. Kishoka, takwimu zetu kielimu bado siyo nzuri sana kwa kuzingatia idadi ya watu. Wanaomaliza elimu ya msingi bila kuendelea baada ya hapo bado ni wengi. Hivyo hivyo kwa Sekondari. Je hii ina maana gani katika suala zima la kuleta maendeleo?
Naungana na wewe kwamba ni vema sasa kuangalia mahitaji yetu ili kufahamu ni elimu ya namna gani inatufaa. Kwa maoni yangu Elimu iliyobora inayotufaa na hasa kwa walio wengi ni elimu ya ufundi stadi ambayo inao uwezo wa kumjenga muhitimu aweze kuanza maisha ya kujitegemea kuliko elimu yetu ya sasa ya Msingi na hata Sekondari.
Kuna kitu ambacho Rais wa Msumbiji Armando Guebuza alizungumza wakati wa Sullivan Summit. Namnukuu kutoka: http://allafrica.com/stories/200806040900.html
"He once again stressed the importance of technical and vocational education. Most African countries, he said, had built schools that taught theory, and that gave pupils the ability to read and write, but did not teach the practical skills, the know-how, that would enable them to develop their countries.
Guebuza declared that his dream is to build technical schools throughout Mozambique, particularly in the rural areas where the majority of the population lives. If the money were available, the Mozambican government would build at least one technical school in each of the country's 128 districts, so that young rural dwellers could conclude their basic and mid-level studies learning useful skills."
Changamoto yangu ni kuwa Elimu ya Ufundi Stadi ndiyo mkombozi wetu. Rev. Unaweza kuangalia namna gani ya kuliboresha hili na ikiwezekana ikawa ni mafunzo ya lazima katika ngazi ya Elimu ya Msingi na Sekondari.
inaendelea...
Kilimo
Asilimia 80 ya Watanzania wanaishi vijijini na wanategemea Kilimo, Uvuvi na Ufugaji kama vyanzio vuya mapato ili kujipatia maendeleo. Kilimo chetu ni cha kujikimu, tunalima japo kidogo kututosha kwa leo na kesho, lakini msukumo wa kulima chakula cha kutosha hata mtondogoo na wiki mbili zijazo hatuna.
itaendelea....