Martha Gwau ametembelea na kushiriki ujenzi wa Shule ya Wasichana Mkoa wa Singida ya Solya

Martha Gwau ametembelea na kushiriki ujenzi wa Shule ya Wasichana Mkoa wa Singida ya Solya

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2019
Posts
377
Reaction score
435
#KutokaManyoni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida Mhe. Martha Gwau ametembelea na kushiriki ujenzi wa Shule ya Wasichana Mkoa wa Singida ya Solya iliyopo Wilaya ya Manyoni.

Akizungumza baada ya kushiriki ujenzi huo Mbunge wa Viti Maalum kwa niaba ya Wanawake Mkoa wa Singida ameishukuru Serikali ya awamu ya 6 chini ya Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza mradi huu ambao unakwenda kuwa chachu kubwa ya maendeleo kwa watoto wa Mkoa wa Singida ambao wanakwenda kuwa wanufaika wakubwa.

Aidha Mhe. Martha Gwau ametumia nafasi hii kuwahamasisha mafundi alioshiriki nao ujenzi kujitokeza siku ya tarehe 23 Agosti 2022 kushiriki zoezi la SENSA.

IMG-20220714-WA0005.jpg
IMG-20220714-WA0006.jpg
IMG-20220714-WA0008.jpg
 
Back
Top Bottom