Martha Gwau awashukuru wajumbe, apita ubunge viti maalum mkoa wa Singida

Martha Gwau awashukuru wajumbe, apita ubunge viti maalum mkoa wa Singida

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
3,119
Reaction score
1,430
Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida, Martha Nehemia Gwau ambaye amemaliza muda wa miaka mitano 2020-2025 amefanikiwa kutetea nafasi yake kwav kupata idadi nyingi ya kura alizopigiwa na Wajumbe Mkutano Mkuu wa UWT Mkoa wa Singida

Katika jumla ya kura 1071 zilizopigwa, Martha Nehemia Gwau amepata kura 922 sawa na asilimia 86 (86%) zilizohesabiwa kwa uwazi mbele ya Wajumbe wote waliopiga kura kwa wagombea 8.

Martha Nehemia Gwau ameongoza kwa kishindo na amewashukuru sana wana UWT Mkoa wa Singida kwa kumuamini na kumpa kura za kishindo ikiwa ni dalili nzuri kuwa7 wameridhishwa na utendaji kazi wake aliofanya wakati wa Uhai wa Bunge la 12

Martha Nehemia Gwau amewashukuru Wajumbe, Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) na amesema ataendelea kuwa mtetezi wa haki za Wanawake na atakuwa Daraja la kuunganisha ndoto zao zitimie.

WhatsApp Image 2025-08-02 at 22.26.55 (1).jpeg
WhatsApp Image 2025-08-02 at 22.26.55.jpeg
 
Back
Top Bottom