Viongozi wakuu wa upinzani wameapa kusimama imara na kushikamana kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027, wakiahidi kusimamisha mgombea mmoja atakayekabiliana na Rais William Ruto
Wakiongozwa na kiongozi wa chama cha Wiper, Kalonzo Musyoka, na wakishirikiana na Naibu Kiongozi wa DCP Rigathi Gachagua, Kiongozi wa DAP-K Eugene Wamalwa, Kiongozi wa DP Justin Muturi na Mwenyekiti wa PLP Martha Karua, viongozi hao walituma onyo kali kwa wanachama wa upinzani watakaotaka kuondoka kwenye mstari wa umoja
Akizungumza jijini Nairobi katika Ukumbi wa Ufungamano wakati wa Mkutano Mkuu wa Wajumbe wa Kitaifa wa PLP, Karua alitangaza rasmi kugombea urais mwaka 2027, huku akiahidi kuhudumu kwa muhula mmoja pekee endapo atachaguliwa
“Nikichaguliwa rais, nitahudumu muhula mmoja tu. Kidole kimoja hakivunji chawa… tutasimamisha mgombea mmoja wa upinzani,” alisema Karua
Viongozi hao walimkosoa Rais Ruto kwa kile walichokiita kuendesha serikali isiyo rafiki yenye sera zisizotekelezeka tangu alipoingia madarakani mwaka 2022.
Wamalwa alisema, “Wakati unakuja ambapo tutatoa dhabihu… tutahakikisha muhula mmoja umetimia na Ruto anarudi Sugoi.”
Kwa upande wake Gachagua aliongeza: “Tuko tayari kutoa dhabihu zozote… niko tayari kumsaidia Martha kama nilivyomsaidia Ruto.”
Kalonzo naye alisisitiza, “Sisi ni serikali inayosubiri kuchukua madaraka, Martha. Tunajivunia wewe.”
Viongozi hao walidai pia kuwa kuna njama ya makusudi ya kugawa upinzani kuelekea uchaguzi wa 2027
“Kuna mpango wa kutusambaratisha… mtauona hivi karibuni,” alisema Gachagua.
Muturi naye aliongeza, “Kuwepo kwetu hapa ni ushahidi kuwa tupo pamoja… ukiona mmoja wetu akiteleza, jua huyo ni msaliti.”
Mkutano huo wa PLP uliidhinisha mabadiliko ya uongozi wa chama kwa kuunda nafasi tatu za manaibu mwenyekiti wa chama na pia kutangaza baraza la mawaziri kivuli lenye wanachama 16 litakalotayarisha sera mbadala kwa taifa
Source: CITIZEN TV KENYA