Martha Karua na Falsafa ya Wagombanapo ndugu!

Martha Karua na Falsafa ya Wagombanapo ndugu!

Joined
Apr 8, 2023
Posts
43
Reaction score
29
Adabu. Niruhusuni mimi nitumie neno "kiasi" kuelezea utovu wa adabu na ukosefu wa nidhamu wa kuingilia mambo ya kifamilia ya familia nyingine na kudai hiyo ni "haki". Kuna tofauti kati ya upumbavu na hekima na yaonekana baadhi yetu somo hili bado ni gumu kwetu.

Moja ya tabia za wakoloni wa babu zetu na falsafa zao watuleteazo na kutumezesha na baadhi yetu bila hata kufikiri, ni kudai "haki" ya Demokrasia (haki ya walio wengi kuchagua) huku wakitaka pia kututafsiria Demokrasia pasina kuiacha Demokrasia ijitafsiri yenyewe, na kila falsafa isiyoweza kujitafsiri yenyewe miongoni mwa jamii, falsafa hiyo ni mfu.

Tabia hii inajionyesha kwenye upumbavu wa Generali Langley kutangaza mbele ya umma kwamba "Traore anatumia dhahabu ya Burkinabe kujilinda" kana kwamba hilo ni kosa, akijipa mamlaka yeye ya kuwasemea Wananchi wa nchi ile bila kuombwa ama kualikwa, kama inavyojionyesha kwenye tabia ya Mkuu wa Bunge la Ulaya kuitisha kilinge na kijadili mambo ya ndani ya Tanzania kana kwamba Tanzania haina Bunge, Afrika Mashariki haina Bunge, au Afrika haina Bunge. Inajionyesha kwenye tabia ya Martha Karua kuvuka mipaka akijifanya ni Mwanasheria na mwanaharakati wa Afrika Mashariki sasa, kutaka kuingilia namna inavyoendeshwa nchini kesi ya Mwenyekiti wa CDM Tundu Antipas Lissu. Huu ni upumbavu wa harakati za kipumbavu.

Watanzania tuna maoni yanayokinzana kwa namna siasa zetu zinavyoendeshwa hapa nchini, tuna maoni kinzani ya tafsiri ya neno "haki" na jinsi inavyotolewa, tuna maoni kinzani ya jinsi wanasiasa wa upinzani wanavyotendewa na watawala na hiyo ni haki yetu, lakini katu hilo halimpi jirani fursa ya kuingiza pua zake kwenye mambo yetu hayo, huo ni utovu wa adabu na ukosefu wa nidhamu ya kawaida tu ya maisha.

Huenda Martha Karua hana ndoa. Angekuwa na ndoa, angeelewa kwamba kwenye familia, kuna nyakati hata baba na mama hawaingilii ugomvi wa watoto hasa watoto hao wakiishakuwa wakubwa, wanachofanya wazazi ni kuzielewa "grievances" za watoto wote na kuwashauri hata kuwashawishi kuzitafutia suluhisho, lakini siyo kuchagua upande, kwa vile huo ni "ugomvi wa ndugu". Lakini Martha hawezi kuielewa hii kwa vile wanaharakati wa aina yake, ni wale ambao kila siku wako majukwaani kutafuta Wanawake wenzao wavunje ndoa zao kama wao wakiamini huo ndiyo "ukombozi" dhidi ya unyanyasaji wa mfumo dume, kwa vile wao waliposhindwa ndoa wakavunja zao, wala senene huita tabia hiyo kuwa "lwango" au "katwishane" na ingekuwa upumbavu kuruhusu hilo kutokea hapa kwetu.

Huenda kila Martha na wenzake hawakukijua ni kwa kitendo cha Martha na wenzake kuanzisha "upashkuna" huo, wameyagawanya tena maoni ya wananchi na kushusha hari ya watu kuhusu Lissu na kesi yenyewe. Mitandao na vyombo vingine vimekuwa ni kuhusu Martha na upashkuna wake badala ya kesi ya Uhaini kati ya Lissu na Serikali. Nguvu kubwa iliyowekwa nyuma ya juhudi za kuhakikisha kwamba kesi inasikilizwa kwa wazi na watu wanaruhusiwa kuhudhuria, ilipaswa kuwa ujumbe tosha kwamba Watanzania tunafahamu tunachotaka Mahakama zetu zifanye, tunafahamu namna ya kukidai na tunaweza kukidai bila kutumia vurugu.

Wakati Martha na wenzake wakicheza upashkuna wao, Watanzania wamesahau kwa muda kuhusu mwanaume aliyeburutwa kutoka ndani ya nyumba yake, mbele ya mkewe, akivuja damu na kupotea, wamesahau kuhusu mwanaume aliyeuawa kwa risasi ya Askari magereza kule Singida, mbele ya mkewe na watoto, tena mkewe akiwaomba askari wale wasimuue mumewe, kwa sababu ya pashkuna mmoja aliyeamua kijitafutia umaarufu wa harufu kwa jambo halimuhusu.

Martha kumtaja Mwalimu Nyerere kwenye upumbavu wake, inaonyesha tu jinsi asivyokielewa kizazi cha leo cha Watanzania na hivyo kama ilivyo kwa mabwana zake wanaomlipia gharama za kuzunguka kueneza 'haraka tu' zake, kudhani kwamba kumtaja Nyerere kutampa huruma za umma, umma ambao walio wengi ni "vijana wa 2000" ambao kwao Nyerere ni 'shujaa' kama Mkwawa ama Kinjekitile kwa vijana wa 80 na 90.

Jifunzeni kwenda na nyakati katika "haraka tu" zenu, ama chutameni maana nguo zimevuka na mwatuonyesha uchi wa bongo zenu. Mmekera!!!!
 
Back
Top Bottom