Martin Kadinda, manager "MPYA" wa Lulu Michael

Martin Kadinda, manager "MPYA" wa Lulu Michael

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Taarifa ikufikie kwamba sexy lady wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ' Lulu' amemnasa aliyekuwa meneja wa Wema Isaac Sepetu , Martin Kadinda ambaye ndiye atakuwa meneja wake kwa sasa.

Akizungumza kwenye Hoteli ya Hyatt Regency The Kilimanjaro iliyopo Posta jijini Dar hivi karibuni waliponaswa wamegandana kama ruba, Kadinda alimuwahi mwanahabari wetu na kumsihi kuwa hawana uhusiano wa kimapenzi bali kuna habari mpya.

Kadinda ambaye hivi karibuni alimwaga kibarua kwa Wema , alisema kwamba aliongozana na Lulu hotelini hapo kwa kuwa kulikuwa na Fainali ya Shindano la Miss Ilala , Dar , wakiwa ni mtu na meneja wake kama alivyokuwa kipindi yuko na Wema .

"Kwa sasa ' nammeneji ' Lulu. Naomba ieleweke hivyo ili baadaye watu wasiseme tunatoka kimapenzi kwa sababu nitakuwa naonekana naye kila mara na kwenye sehemu tofauti ," alisema Kadinda ambaye pia ni mbunifu wa mavazi.

Kwa upande wa Lulu, alionekana kufurahia maneno hayo na kufanikiwa kumpata meneja huyo huku akiongezea kuwa amefarijika kuwa na meneja kama Kadinda."Huyu ni meneja bora na siyo bora meneja kwa hiyo kama mtu anataka kufanya kazi na mimi , aanze kwa meneja wangu, " alisema Lulu .

Ukaribu wa Lulu na Kadinda ulianza kitambo hata kabla Kadinda hajafahamika kama ilivyo sasa .
 

Attachments

  • 1410856242510.jpg
    1410856242510.jpg
    68.3 KB · Views: 2,099
Wema kwisha manenoo alimtuza pesa yule mwanamuziki,kisha pesa akarudishiwaa
 
na lazima tukodishe fast jet mimi na binamu yangu Dinazarde kutangaza msiba hadi vijijini kabisa uko, wote wajue

Ngojea mrembo by nature asikie.Nimenunua popcorn na fanta yangu baridi niangalie mtanange huu.
 
Last edited by a moderator:
Huyu Kadinda nae anatuchoshaaa! mara Wena hana hela ya kunilipa mara sijui ufukunyuku gani kumbe alishaanza kuona Wema ameishiwa na Habari,haya atuonyeshe huyo mwanamke wake anae mmeneji mbona hatusikii kakutwa na mwanamkee sehemu au huyo ndio mchuchu wake?
 
na lazima tukodishe fast jet mimi na binamu yangu Dinazarde kutangaza msiba hadi vijijini kabisa uko, wote wajue

Na viroba vya jogoo huku tukicheza viduku eti binamu
 
Last edited by a moderator:
Hivi hawa Mameneja kazi yao ni nini hasa?

Afadhali Fellah nimeanza kumuelewa baada ya ujio wa Yamoto band, lakini hawa kina babu Tale sijui Kadinda kwakweli mimi sijui kazi yao ni ipi hasa?
 
Back
Top Bottom