Kwani watu wanaomkubali Twitter, wanamkubali kwa sababu tu ni Martin kutoka Mara au kutokana na vitu anavyopost?..
Kwani posts anaandikiwa au anaziandika mwenyewe kutokana na uwezo wake, na vipi kuhusu reactions zake kwa watu. Nazo hizo ni mambo ya "X" au ni ufunguo wa kujua charisma, brains na emetional intelligence yake?..
Na vipi kuhusu viongozi ambao tunawaona kwenye TV, je nao tuwategeshee camera majumbani mwao ilhali kupitia interviews tu wanazofanya kuna kitu wanakiwasilisha.
Unachokionesha kwa watu ndicho kitakachotumika kukupima wewe ni mtu wa aina gani. Ndio maana watu wanaajiri brand strategists na publicists kwa kazi hiyo mkuu