Martin Maranja Masese: Vipindi vya redio hapa Tanzania vinaharibu fikra na mitazamo yetu wasikilizaji

Martin Maranja Masese: Vipindi vya redio hapa Tanzania vinaharibu fikra na mitazamo yetu wasikilizaji

Inside10

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2011
Posts
29,909
Reaction score
32,414
Nimeisoma hii twit yake huko X naona kuna ukweli wa wazi kabisa..
God have mercy on US, tunatengeneza jamii isiyokuwa na fikra chanja na upembuaji wa mambo MTAMBUKA kwa nchi yetu.
Hii hapa twit yake;

"Taifa ambalo redioni asubuhi hadi mchana wanajadili michezo. Mchana hadi jua linapozama wanajadili umbea. Jua likizama wanarudi kwenye michezo. Usiku wanajadili ngono hadi pakuche. Hakuna vipindi vya taaluma, ujasiriamali, kilimo, midahalo. Hilo ni TAIFA lipo kaburini kitambo."

Screenshot_20240717_212341_X.jpg

-Nini kimekushangaza?
-Nini kimekufurahisha?
-Yapi maoni yako?
Inside10 Misungwi stand, Mwanza
 
kiukweli kuna muda vipindi vya redio hata tv vinatia kinyaaa na hii imefanywa makusudi na watawala ili tuweze kutawaliwa kirahisi. japo kutambua hili inabidi uangalie kwa umakini mkubwa.
wameamua kuzifanya akili zetu zisiwaze mambo makubwa na wao kutuelekeza ya kuwaza
 
redio zote zinamtiririko wa vipindi ambavyo havimake sense except vipindi vya sports and games vipindi vingine ni uozo mtupu
Na hivyo vya sports vyote vipo muda mmoja angalia hapo juu kwenye twit ya MMM utaona
 
Nimeisoma hii twit yake huko X naona kuna ukweli wa wazi kabisa..
God have on on US, tunatengeneza jamii isiyokuwa na fikra chanja na upembuaji wa mambo MTAMBUKA kwa nchi yetu.
Hii hapa twit yake

View: https://x.com/IAMartin_/status/1813497748336898383?t=b2lq6ET75rnkX7FPICy4rw&s=19

-Nini kimekushangaza?
-Nini kimekufurahisha?
-Yapi maoni yako?
Inside10 Misungwi stand, Mwanza

Nimeshangaa@Inside(10)kuwepo stendi Misungwi muda huu na hajatueleza anafanya nini baada ya kupost sledi hii.
 
Nimeisoma hii twit yake huko X naona kuna ukweli wa wazi kabisa..
God have on on US, tunatengeneza jamii isiyokuwa na fikra chanja na upembuaji wa mambo MTAMBUKA kwa nchi yetu.
Hii hapa twit yake

View: https://x.com/IAMartin_/status/1813497748336898383?t=b2lq6ET75rnkX7FPICy4rw&s=19

-Nini kimekushangaza?
-Nini kimekufurahisha?
-Yapi maoni yako?
Inside10 Misungwi stand, Mwanza

Wana promote na kutoa elimu ya michezo ili ushawishi wa kubet uwepo wa kutosha kwa njia ya michezo.
 
Nimeisoma hii twit yake huko X naona kuna ukweli wa wazi kabisa..
God have on on US, tunatengeneza jamii isiyokuwa na fikra chanja na upembuaji wa mambo MTAMBUKA kwa nchi yetu.
Hii hapa twit yake

View: https://x.com/IAMartin_/status/1813497748336898383?t=b2lq6ET75rnkX7FPICy4rw&s=19

-Nini kimekushangaza?
-Nini kimekufurahisha?
-Yapi maoni yako?
Inside10 Misungwi stand, Mwanza

BAO LA ASUBUHI la TBC lime-nishangaza linavyo waingia watu!
alafu mtangazaji wa Televisheni ya Taifa anamuuliza msikilizaji UNASKILIZIA BAO LA ASUBUHI ukiwa wapi?

Mtoto wa Jirani yangu alikuwa anakunywa chai , familia nzima wapo mezani, MTANGAZAJI WA TBC akasema "muulize mwenzako "BAO LA ASUBUHI AMELISIKIAJE"? basi mtoto akamuuliza mama yake kuhusu alivyolisikia bao la asubuhi, Familia nzima wakaona aibu, kila mmoja akajifanya anakohoa na hajasikia alichouliza mtoto!
 
Nina miaka kadhaa sisikilizi radio, kwanza unasikiliza radio ili usikie nini ambacho haujakipata huku mitandaoni?

Huwa navizia vipindi vya mziki tu.
Upo kama mm, kwenye Tv na radio nataka muziki tuu mana mengine yote nayapata mtandaoni kwa muda mfupi tuu
 
Sasa Contents zinatengenezwa kutokana na jamii inachopenda vijana wengi tunapenda mpira, pombe na ngono Sasa wenye radio ili wasipoteze audience ya vijana ambayo ndio kubwa in terms of population basi wanaishi na sisi kama tunavyopenda
 
Tulishasema humu kitambo sana

Ila mfumo ndiyo unataka hivyo

Za kuambiwa changanya na zako

Ova
 
They're customer oriented wameangalia watanzania wanahitaji nini na radio zimewapatia
Hivyo vipindi vinawalipa that's why Kila radio unaona vinashupalia hizo program

Mpira
Ngono
Umbea
Betting
Wachungaji wa Michongo
Uchawa
 
Back
Top Bottom