Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Anaandika Martin Maranja Masese, Mtikila
Waziri Mkuu, Naibu Waziri Mkuu, Mwanasheria mkuu wa serikali, Spika wa bunge, Naibu Spika wa bunge, Mawaziri na Wabunge wote, wanalipwa posho ya kujikimu (perdiem) kwa siku ni Sh220,000.
Jumla ya idadi yote ya wabunge ni 393. Wabunge wa majimbo ni 264. Wabunge wa viti maalum ni 113. Wabunge wa baraza la wawakilishi ni 5. Wabunge wa kuteuliwa na Rais ni 10. Mwanasheria Mkuu wa Serikali 1.
Jumla ya wabunge wote bungeni ni 393. Hivyo, jumla kwa siku moja Dodoma wanalipwa Sh86,460,000. Hizi ni fedha zenu. Hebu tazama hapo kwenu, kata zenu zina vituo vya afya? Visima? Barabara? Shule?
Kwa maoni yangu, katiba ieleze; fedha ya kujikimu inapaswa kutolewa kwa wabunge (ukiondoa mbunge wa Dodoma Mjini), kwa hoja kwamba makazi yao siyo Dodoma, wapo nje ya kituo cha kazi, jimboni.
Kwanini watu hawa hapo juu walipwe fedha za kujikimu (perdiem) Sh220,000 wakati serikali imewajengea makazi yenye huduma zote Dodoma? Makazi yao yana walinzi wanaolipwa na serikali. Kujikimu vipi?
Waziri Mkuu na Naibu Waziri Mkuu, Spika na Naibu Spika wa bunge, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, wanastahili hayo malipo ya Sh220,000 kwa siku kwa ajili ya kujikimu wakiwa Dodoma? Kwanini wanastahili?
Waziri Mkuu, Naibu Waziri Mkuu, Mawaziri na Spika wa bunge na Naibu Spika wa bunge, Mwanasheria Mkuu wa Serikali; vituo vyao vya kazi ni Dodoma (lilipo bunge la JMT). Serikali imewapa makazi Dodoma.
Je, watu hawa wanalipwa kwa sababu tu na wao ni wabunge kama wabunge wengine? Au kuna sababu nyingine? Kama hiyo ndio sababu ya msingi, Je, hii ni sahihi? Je, sio matumizi mabaya ya fedha za umma?
MMM, Martin Maranja Masese, Mtikila.