Platformtz
JF-Expert Member
- Apr 26, 2017
- 266
- 405
Bada ya Mahakama ya juu nchini Kenya kufuta matokeo ya uchaguzi wa awali wengi tulisifia uthubutu wa Majaji na uvumilivu wa Serikali iliyoko madarakani kuonesha ukomavu wa kisiasa na kidemokrasia.
Lakini kinachoendelea kwa sasa kinatia hofu na kutishia usalama na utulivu wa kisiasa nchini Kenya,na pengine hata kusababisha machafuko ya kisiasa kama ilivyotokea 2007/8.
1*Tume ya uchaguzi haiaminiki!
~Inatuhumiwa na upinzani kukosa maadili,uaminifu na uhalali wa kuendesha marudio ya uchaguzi.
~Tume kutofanya marekebisho dhidi ya mapungufu na makosa ya Msingi yaliyopelekea uchaguzi wa awali kufutwa.
~Wajumbe/makamishina wa Tume kutokuaminiana, kutoelewana,kukosa Ushirikiano,kufanya maamuzi bila kuzingatia kanuni na taratibu kwa mujibu wa Sheria.
~Maisha ya wajumbe wa tume/makamishina yapo hatarini kutokana na vitisho vya dhahiri dhidi ya uhai na ustawi wa maisha yao.
~Baadhi ya makamishina kuanza kujiuzuru mfano.Senior commissioner Dr.Roselyne Akombe.
2*Upande wa Serikali iliyoko madarakani(Jubilee) hauaminiki!
~Unaituhumu mahakama kufanya maamuzi kwa manufaa binafsi ya majaji kwa mlengo wa kuwanufaisha wapinzani.
~Unatuhumiwa na wapinzani kutoa maagizo kwa mwenyekiti wa Tume na kuingilia mifumo ya usimamizi na uhesabuji wa kura.
~Unatuhumiwa kutoa vitisho vya dhahiri kwa baadhi ya wajumbe/makamishina wa tume na wagombea wa upinzani.
3*Upinzani (NASA)hauaminiki
~Madai na mashinikizo dhidi ya tume yanazidi kila uchao.
~Kutokuwa na msimamo na kubadili maamuzi bila kuzingatia uzito.mf.Mgombea wa NASA Raila Odinga kutangaza kujitoa kwenye uchaguzi wakati huo huo anatangaza maandamano ya kupinga tume na uchaguzi wenyewe!!!
~Kuonekana wavurugaji kwa kushindwa kusimamia hoja na kushindana na changamoto.
Maamuzi na mwenendo wa kila upande unaotegemewa kufanya uchaguzi uwe wa amani,huru na haki yanatia Shaka na hofu kwa wananchi pamoja na jumuiya za kimataifa juu ya hatima Njema ya uchaguzi nchini Kenya.
Je,haya ndo matunda ya demokrasia au ubinafsi wanasiasa!!?