Marufuku kukusanyika Mnazi Mmoja, Kidongo Chekundu

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,801
Imeandikwa na Oscar Job; Tarehe: 16th May 2011

HALMASHAURI ya Manispaa Ilala, mkoani Dar es Salaam imepiga marufuku matumizi ya viwanja vya Mnazi Mmoja na vingine vya wazi kwa ajili ya mikusanyiko mbalimbali.

Halmashauri ya Manispaa Ilala leo imetoa taarifa na kubainisha kuwa, viwanja hivyo havipaswi kutumika kwa ajili mikutano, makongamano, maandamano, mihadhara ya kidini na siasa.

Viwanja vingine ambavyo havipaswi kutumika kwa ajili hiyo ni Kidongo Chekundu na viwanja vyote vya shule za msingi na sekondari.

Taarifa hiyo ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Gabriel Fuime, imesema viwanja vinavyoruhusiwa kisheria kwa shughuli kama hizo ni vya Jangwani.

Hata hivyo, Manispaa imeweka pia masharti katika kutumia viwanja hivyo vya Jangwani, ikieleza kuwa, anayependa kuvitumia anatakiwa awasilishe maombi siku saba au zaidi kabla ya tarehe ya kuvitumia.

Fuime alisema hatua hiyo juu ya viwanja vya Jangwani, inalenga kupunguza mwingiliano wa matumizi.

“Mara nyingi pamoja na mwingiliano wa siku za mikutano yao, waombaji wa matumizi ya viwanja hivi pia wamekuwa wakitoa kwa kushitukiza, jambo linalotufanya tushindwe kuwasiliana na mamlaka zingine zinazohusika, zikiwemo za kiusalama,” amesema.

Amesema, kama taarifa hizo zitatolewa mapema, zitawasaidia kujipanga vyema katika masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwa vyombo vya usalama kwa ajili ya ulinzi.
 
Mbona hawasemi viwanja hivyo ni kwa matumizi gani sasa.
 
Right now the public have an insatiable curiosity to know everything, except what is worth knowing so whatever happens they will give up!!!
 
Ahaaaa! Ahaaaaa! Kikwete maji ya shingooooo! Kwa taarifa yako mkuu wakaya na TISS, cdm hata wakiweka mkutano kule kisarawe au kule samvulachole watu watajaa balaa!!
 
Imeandikwa na Oscar Job; Tarehe: 16th May 2011

HALMASHAURI ya Manispaa Ilala, mkoani Dar es Salaam imepiga marufuku matumizi ya viwanja vya Mnazi Mmoja na vingine vya wazi kwa ajili ya mikusanyiko mbalimbali.

Halmashauri ya Manispaa Ilala leo imetoa taarifa na kubainisha kuwa, viwanja hivyo havipaswi kutumika kwa ajili mikutano, makongamano, maandamano, mihadhara ya kidini na siasa.

Viwanja vingine ambavyo havipaswi kutumika kwa ajili hiyo ni Kidongo Chekundu na viwanja vyote vya shule za msingi na sekondari.

Taarifa hiyo ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Gabriel Fuime, imesema viwanja vinavyoruhusiwa kisheria kwa shughuli kama hizo ni vya Jangwani.

Hata hivyo, Manispaa imeweka pia masharti katika kutumia viwanja hivyo vya Jangwani, ikieleza kuwa, anayependa kuvitumia anatakiwa awasilishe maombi siku saba au zaidi kabla ya tarehe ya kuvitumia.

Fuime alisema hatua hiyo juu ya viwanja vya Jangwani, inalenga kupunguza mwingiliano wa matumizi.

“Mara nyingi pamoja na mwingiliano wa siku za mikutano yao, waombaji wa matumizi ya viwanja hivi pia wamekuwa wakitoa kwa kushitukiza, jambo linalotufanya tushindwe kuwasiliana na mamlaka zingine zinazohusika, zikiwemo za kiusalama,” amesema.

Amesema, kama taarifa hizo zitatolewa mapema, zitawasaidia kujipanga vyema katika masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwa vyombo vya usalama kwa ajili ya ulinzi.

Viwanja vya Jangwani nionavyo si vya Manispaa ya Ilala tu ila vya Jiji zima kama si taifa. Kwa maana hiyo kwa maelezo ya Mkurugenzi ni sawa na kusema kwamba Manispaa haina viwanja kwa shughuli za kijamii. Hata kama (jangwani) ni vya manispaa bado haingii akilini kwa manispaa nzima kwa idadi ya watu wake kuwa na kiwanja kimoja tu! Kadiri mahali panapokuwa na watu wengi tegemea shughuli nyingi na hivyo uwezekano wa kuingiliana ukawa mkubwa jambo ambalo linaweza kuleta migogoro isiyo na lazima.

Au tusishangae kwamba hili limewekwa strategically kuhakikisha kundi fulani litakapohitaji kutumia viwanja husika siasa ziingizwe kwamba tayari kundi lingine walishaomba! Hilo linawezekana sana Tz; ni maandalizi maalumu hayo.

Chonde chonde Manispaa tumieni busara, tuepusheni na migogoro isiyo na lazima siku za usoni; tengeni maeneo ya wazi ya kutosha kwa ajili ya shughuli za kijamii katika maeneo mbalimbali - Buguruni, Kipawa, Kinyerzi, Ukonga, Gongo la Mboto, Chanika, Tabata, n.k. Manispaa zingine pia wafanye hivyo hivyo. Upumbavu kidogo tu waweza kuwa bomu - hukawii kusikia dini fulani wamepewa Jangwani sisi tumenyimwa, chama fulani wamepewa sisi tumenyimwa, mganga fulani, mhubiri fulani, mhadhiri fulani, ..., n.k.

Mwenye masikio na asikie.
 
wameogopa wamejua muda wowote tunaweka kambi maeneo ya ya kidongo chekundu na mnazi mmoja kuishinikiza serikali kujiuzulu,
 
Kuna maandamano ya cdm nini?

FEAR = 'False Evidence Appearing Real', which is always the cause of defeat kwani at this point people cease to be wise and through their panic they happen to create confusion which instead of solving the problem make it complex! CHADEMA vema; sanaaaaaaaaaaaaa! Peoples; poweeeeeeeeeer!
 
hiyo RED ni uhuni wa serikali kujaribu kuvunja haki za binadamu kwa kuondoa maeneo ya mikusanyiko, mbona wako fasta na mambo kama haya kwenye mafisadi wanakuwa wadogo
nadhani hapo wanaanda jinsi ya kuua watu maana lazima kutakuwa na pata shika,
hizo siku saba JAGWANI za nini?
POLISI uombe kibali kwa ajili ya maandamano na mikusanyiko halali baada ya hapo hakuna viwanja mpaka uwapige barua ya siku saba. na majibu yanachukua muda gani?
na ni nani nayetoa kibali maana hapo ndipo hadithi za hayupo kasafiri zitakapo tokomeza democrasia na haki za binadamu

Back
Top Bottom