nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,860
- 5,801
Imeandikwa na Oscar Job; Tarehe: 16th May 2011
HALMASHAURI ya Manispaa Ilala, mkoani Dar es Salaam imepiga marufuku matumizi ya viwanja vya Mnazi Mmoja na vingine vya wazi kwa ajili ya mikusanyiko mbalimbali.
Halmashauri ya Manispaa Ilala leo imetoa taarifa na kubainisha kuwa, viwanja hivyo havipaswi kutumika kwa ajili mikutano, makongamano, maandamano, mihadhara ya kidini na siasa.
Viwanja vingine ambavyo havipaswi kutumika kwa ajili hiyo ni Kidongo Chekundu na viwanja vyote vya shule za msingi na sekondari.
Taarifa hiyo ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Gabriel Fuime, imesema viwanja vinavyoruhusiwa kisheria kwa shughuli kama hizo ni vya Jangwani.
Hata hivyo, Manispaa imeweka pia masharti katika kutumia viwanja hivyo vya Jangwani, ikieleza kuwa, anayependa kuvitumia anatakiwa awasilishe maombi siku saba au zaidi kabla ya tarehe ya kuvitumia.
Fuime alisema hatua hiyo juu ya viwanja vya Jangwani, inalenga kupunguza mwingiliano wa matumizi.
Mara nyingi pamoja na mwingiliano wa siku za mikutano yao, waombaji wa matumizi ya viwanja hivi pia wamekuwa wakitoa kwa kushitukiza, jambo linalotufanya tushindwe kuwasiliana na mamlaka zingine zinazohusika, zikiwemo za kiusalama, amesema.
Amesema, kama taarifa hizo zitatolewa mapema, zitawasaidia kujipanga vyema katika masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwa vyombo vya usalama kwa ajili ya ulinzi.