Marufuku Machinga kuwapo mtaani kuanzia Septemba 24, 2022

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Katika kutekeleza maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuwapanga wafanyabiashara wadogo maarufu machinga katika maeneo maalum, Halmashauri ya Jiji la Dodoma imesema ifikapo Septemba 24 mwaka huu, hakuna machinga atakayeendelea kubaki mtaani baada ya kukamilika ujenzi wa mradi wa soko la wazi litakalotoa huduma saa 24.

Soko hilo limegharimu Sh. bilioni 9.53 na lina uwezo wa kuchukua wafanyabiashara zaidi ya 5,000.

Mkurugenzi wa Jiji hilo, Joseph Mafuru, akizungumza na waandishi wa habari juzi ofisini kwake, alisema kukamilika kwa mradi huo ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya Rais Samia aliyotoa kwa wakuu wa mikoa Septemba 13, mwaka jana la kuwapanga machinga katika maeneo maalum bila kuwasumbua katika ufanyaji wao biashara.

“Mpaka sasa tunakamilisha mradi huu ni kama mwaka mmoja umepita toka agizo hilo kutolewa. Kwanza, tunamshukuru Mheshimiwa Rais kwa kutuvumilia lakini tulitaka mradi huu ukamilike kabisa ili machinga wote tuwapatie eneo sahihi na la kudumu kwa ajili ya biashara zao,” alisema Mafuru.

Alisema soko hilo lina ukubwa wa mita za mraba 14,235 na ndani yake linajumuisha huduma zote muhimu kama vile eneo maalum la kinamama kunyonyesha, kituo cha polisi, huduma za kifedha na maeneo ya vinywaji na vyakula.

“Tunataka mtu akiingia katika soko hili kila kitu akipate hapa, kama kuna bidhaa kaja kununua, basi huduma za saluni azikute hapa, akitoka arudi nyumbani siyo kwenda eneo lingine tena kutafuta huduma,” alisema.

Alibainisha kuwa kati ya fedha zilizotumika, Sh. bilioni 6.5 zimetokana na mapato ya ndani kutoka katika vyanzo mbalimbali na serikali kuu iliongeza Sh. bilioni tatu.

Mafuru alisema kutokana na kukamilika kwa mradi huo, machinga wote hadi ifikapo Septemba 23 mwaka huu wanapaswa kuwa wametoka mitaani.

“Hadi Septemba 24 hatutaki kumwona machinga yeyote anazunguka mitaani katika maeneo hatarishi ikiwamo kupanga bidhaa zao kwenye barabara na maeneo ya watembea kwa miguu,” alionya.

Mkurugenzi huyo alisema mradi huo utaliwezesha jiji kupata mapato ya Sh. bilioni 1.2 kwa mwaka kutokana na makusanyo mbalimbali ndani ya soko.

Alibainisha faida za kukamilika kwa mradi huo kuwa ni pamoja na kuongeza hali ya usafi katika jiji kwa kuwa wafanyabiashara wadogo ndiyo wamekuwa sehemu kubwa ya uchafunzi wa mazingira.

“Faida nyingine ya mradi huu ni usalama wa wafanyabiashara na bidhaa zao, lakini wanaweza kukopesheka kwa kuwa watatambulika wao na maeneo yao ya kufanyia biashara,” alisisitiza Mafuru.

Chanzo: Nipashe
 
Daslamu sasa ndio pameoza, huku machinga, huku boda, huku bajaji, huku malori, huku maguta, sijui unachomokea wapi, barabara zenyewe magari madogo yamepaki,
Siku pakija kuwaka moto hautazimika mpaka kiyama ngojeni viongozi wajitoe fahamu tu
 
Soko hilo liko sehemu gani?
 
Dar es Salaam ni kubwa huwezi kuweka soko moja la wamachinga ukakidhi nahitaji dawa ni kufungua maeneo machache sehemu mbalimbali na kuongeza maeneo ya minada ya siku kwa siku. Pia masoko ya jioni yaruhusiwe kwa wamachinga bila ya wao kujenga mabanda pia wajifunze dhana ya open air markets kutoka Uholanzi ni mfumo mzuri sana wa minada
 
Ni machinga afu ana soko[emoji23][emoji1787]hii nchi inawasomi wa hovyo sana.
 
Back
Top Bottom