Marufuku magari ya serikali kubeba mkaa: Huyu Waziri anadhani madereva wanamshahara kama wake?

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2021
Posts
2,268
Reaction score
7,119
Imenishangaza sana kuona kwenye mitandao ya kijamii Waziri wa serikali ya CCM akipiga marufuku magari ya serikali kubeba mkaa.

Yaani dereva akitoka safari asichukue hata junia moja la kwenda kutumia home!

Huu ni unyayanyasaji unaofanywa na Waziri Kwagilwa kwa kigezo cha kutunza mazingira
 
IMG-20260916-WA0027.jpg
 
Wasiokuwa madereva wa Serikali kwao hawapikii mkaa? Wao wanawezaje kupeleka mkaa kwenye nyumba zao bila kutumia magari ya Serikali hadi madereva wa Serikali washindwe kutumia mbinu hiyo?

Tuache kutetea ujinga wa kutumia rasilimali za Serikali kwa manufaa binafsi. Hii inapelekea kuharakisha uchakavu wa mali za Serikali kutokana na kukithiri kwa matumizi ya hovyo.

Halafu kiswahili sanifu ni gunia na sio 'junia'
 
Tehe! Serikali hii inavyojua kubana matumizi, I support, madereva pia wabanwe magari yanachakaa
 
Back
Top Bottom