Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 378
- 766
Rais Donald Trump amesaini rasmi amri ya kiutendaji jana, Jumatano, Februari 5, 2025, ya kupiga marufuku wanamichezo waliobadili jinsia kushiriki katika michezo ya wasichana na wanawake.
Amri hiyo, inayojulikana kama "Kuwazuia Wanaume Kuingia Kwenye Michezo ya Wanawake," inawapa mashirika ya serikali mamlaka pana ya kuhakikisha taasisi zinazopokea ufadhili wa serikali ya shirikisho zinazingatia Kifungu cha IX kwa mujibu wa tafsiri ya utawala wa Trump, ambayo inafasiri neno "jinsia" kuwa ile aliyozaliwa nayo mtu.
"Kwa amri hii ya kiutendaji, vita dhidi ya michezo ya wanawake vimefikia mwisho," Trump alisema katika hafla ya kusaini amri hiyo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mashariki walkulu, ikihudhuriwa na wabunge na wanamichezo wa kike waliounga mkono sheria hiyo, akiwemo Riley Gaines, aliyewahi kuwa mwogeleaji maarufu wa vyuo vikuu.
Msemaji wa Ikulu, Karoline Leavitt, amesema kuwa amri hiyo
"inalinda ahadi ya Kifungu cha IX" na italazimu "hatua za haraka, zikiwemo hatua za utekelezaji, dhidi ya shule na mashirikisho ya michezo" yanayoshindwa kutoa michezo na vyumba vya kubadilishia nguo kwa jinsia moja pekee.
Amri hiyo ilisainiwa sambamba na Siku ya Kitaifa ya Wasichana na Wanawake Katika Michezo na ni sehemu ya msururu wa maagizo ya kiutendaji kutoka kwa rais huyo wa chama cha Republican yanayolenga watu wa jinsia ya mpito (transgender)