Marufuku ya Bweni Shule za Msingi, Serikali imekurupuka

Kumpeleka mtoto mdogo boarding ni sawa na kumtelekeza mtoto wako mataa,zinduka hata Kama una majukumu kiasi gani jitahidi kutenga muda kulea mwanao mwenyewe
 
Hilo la watoto kusoma wikiendi nahisi ni msimamo wa mzazi tu. Binafsi hakuna mwanangu anayesoma wikiendi. Yawe maamuzi ya shule au ya kwake mwenyewe. Haendi na shule zinajua hilo.
Changamoto Bado inakuwepo sababu mtoto wa mwingine atakuja kuathiri jamii. Labda atakuja kuwa mkwe wangu ambaye amekosa malezi ya wazazi
 
Elimu ni biashara ebu tafuta msomi aliyesoma Kama utakuata mtoto wake yupo uko boarding, tunaohangaika na boarding ni sisi ambao elimu tulikkosa gafla mungu katupa vimia mbili Mia tatu basi tunajikuta tunalipa pesa nyingi kwa sifa na somesha na mnanyonywa balaa

Unatapesa unataka mwanao aongee kingereza mbona walimu wapo mtaani wengi tu tafuta mwalimu aje home afundishe watoto kingereza maana kingereza Cha shule watoto wanasoma darasani no vigumu mtoto kuongea kingereza ila akija mwalimu nyumbania akampa misingi ya kingereza akikijua hicho basi uko shule Napo atajua tu
 
Kama ww ulivyokurupuka kuandika uzi bila kuangalia athari za mapana kwa taifa ,malezi na familia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…