Marufuku ya mitumba wenzangu na mimi tutatoboa kweli?

HAO MAWAZIRI WANAZIJUA HALI ZA WATANZANIA?, WAACHANE NA HILI WAJIHIMIZE KWENYE MENGINE YA MSINGI, MAJI, BARABARA, MADAWA NAFUU KWA KILA MTANZANIA NA YA AINA HII.
 
Hizi nchi zote hazina viwanda vya kutengeneza nguo

Watapigwa biti na Marekani
 
Wamepiga hesabu ya ajira zitakazopotea? Wamejipangaje kuanzisha ajira nyingine kwa wale watakaopoteza ajira?
 
Quality ya mikate imeshindikana je Quality ya nguo? Serikali isicheze na Mwili wa mtanzania.
 
Kusema kweli mitumba ya nguo toka huko inakotoka ndizo nguo imara na ngumu kuvumilia mazingira magumu. Wale wamevaa mara moja au mbili wakavua nguo ikiwa bado mpya na haijachakaa kiasi cha kutovalika tena. Ikiletwa huku ni mpya na ni unique. Bei zake ni rahisi unaweza kujaza gunia kwa kuwa na nguo nyingi za kubadilisha. Shangaa jeans mzungu kavaa wee likiletwa huku ni jipya na linaendelea kuvalika. Sasa wakipiga marufuku kuingia nguo hizo wanataka tuvae malapulapu ya vitambaa vyetu vinavyopauka asubuhi tu
 
Unapo mwambia mwanao acha umalaya unawajibika umpe kazi ya kufanya!
Jee sababu ya Ujio wa mitumba Imeisha Lini?
Msituongezee maumivu! Kwa sasa tuna shida ya mkaa na bei ya Gesi haikamatiki Huku uswazi[emoji56][emoji24][emoji24]

Sent from my vivo Y67 using JamiiForums mobile app
 
Ni balaa
 
Hata watalii wakija huku huwa wanazinunua pia [emoji23][emoji23][emoji23]
 
kumbuka ili iwe mtumba ni lazima ianze kuwa mpya kwanza, so hakuna namna mtumba unaweza kuwa bora kuliko mpya kwa same brand.
 
Waafrika mmeoza vichwa kiasi kwamba mnashindwa kuona tatizo linalowakwamisha kupiga hatua. Chanzo cha kukosa viwanda ni kuwepo kwa hiyo mitumba. Wazalishe wamuuzie nani? Soko linakuwa hamna. Serikali za Afrika zote zikipiga marufuku mitumba ndani ya miaka mitano Afrika inakuwa mbali kwenye textile industry. Viwanda vitaongezeka na uzalishaji utaongezeka watafikia hatua ya kushindania soko kwa kushusha bei wenyewe. Ajira zitapatikana kwa wingi viwandani, malighafi kama pamba, n.k vitapata soko la uhakika hapa hapa sio mpaka kusafirishwa nje na hata hizo malighafi za bei chee wanazotumia wachina na wazungu zitaletwa hapa na zitatumika tu maana mfanyabiashara anahitaji kupunguza gharama za uzalishaji na ku maximize faida.

Adui mkubwa wa maendeleo ya mwafrika ni utegemezi tunaozoeleshwa na wazungu. Na ndio maana kila tukitaka kujitoa kwenye kuwategemea wanaleta vikwazo vingi sana ili mradi tubaki tunawategemea. Mfano hilo la kupiga marufuku mitumba litapingwa sana na mabeberu na vibaraka wao hapa Afrika na najua hakitafanikiwa.
 
Hao wanaopiga marufuku wanasahau kwamba itafika muda wataenda kuomba kura kwa wavaa mitumba je wanatarajia wawakute uchi.

Mimi napenda mtumba hasa kadeti na mashati ya mistari yanakua mazuri sana japo sio bora zaidi ya dukani kinachotuchanganya dukani kuna fake na og na bei sio kigezo cha kua og au fake mfano nilishanunua mkanda wa ngozi dukani kwa dau la 20k na nikaja kununuliwa mkanda mwingine wa dukani na wife nao alinunua 25k kama sijakosea lakini hizi bidhaa mbili zilionyesha utofauti haraka sana. Pia nina mkanda nilinunua opposite na china plaza buku 3 tu ila unafanya vyema sana mpka leo.

Watu wengi tunakimbilia mtumba kwaajili ya mazingira maji sabuni na uchumi hatuna uwezo wa kufulia mashine wengi wetu hivyo nguo za dukani zina maelezo kibao namna ya kufua aina ya maji nk.
 
Nadhani Hilo katazo litaishia kwenye makaratasi!
 
Sawa!!!lakini huo mmbadala wa hivyo viwanda vya kutengeneza vya kwetu vipo tayari au ni makatazo alafu ndio shughuli ya kujenga viwanda ndio ianze!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…