Marufuku ya mitumba wenzangu na mimi tutatoboa kweli?

Sawa!!!lakini huo mmbadala wa hivyo viwanda vya kutengeneza vya kwetu vipo tayari au ni makatazo alafu ndio shughuli ya kujenga viwanda ndio ianze!!
Magonjwa yakitaka kuja hayaanzi kuuliza kama dawa zake ziko tayari? Yangekuwa yaanza kuwataka watu waandae dawa za kuyadhibiti ndio yaje yasingefanikiwa kuua. Badala hake yanakuja tu na watu wana respond haraka sana kulingana na urgency au fursa inayokuwepo baada ya kutokea tatizo. Waafrika tumekuwa watu wa kutafuta visingizio kwanza kwenye kila tunaloamua kulifanya badala ya kulifanya kwanza. Matokeo yake tunajitisha wenyewe tunaishia njiani
 
Mbona naona Tangazo kama ni la Kenya au linatuhusu mpaka sisi wa Manyoni huku.
 
Kwa hiyo viwanda navyo vitaibuka tuu kama magonjwa!!
 
Kuna mambo hata yasikuumize kichwa
Kuna majitu yakiamka tu yakiwaza ujinga yanakuja kuuleta kwenye jamii kwa sababu tu wako na mamlaka
hayanaga hata mda wa kukaa na watu na kujadili mambo na kupata mawazo
Hiyo inaishia kuwa habari tu na inaisha hivyo lakini kitu kama hicho hakiwezi kuwepo nimekaa pale mzee


Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Hata vipuri vya magari (spare) kuukuu (used) ni bora kuliko mpya.
hata hiyo kuukuu (used) ilikuwa ni mpya kabla ya kuwa kuukuuu mkuu... ili upate used ni lazima uwe na Mpya kwanza.
 
Mguo za bluu china ni nini wanapendeza tu na sisi tujaribu
 
Utakuta kuna vigogo wamepanga kuanzisha biashara ya nguo sasa wanawapoteza kwanza washindani.
 
Kwa hiyo viwanda navyo vitaibuka tuu kama magonjwa!!
We unafikiria viwanda vijengwe na serikali, sio? Kwenye fursa watu wanachangamka haraka sana labda wazembe kama nyie ndo mnaolala. Hata wakipiga marufuku mitumba leo, ndani ya mwezi tu viwanda vitakuwepo. Usicheze na watu wa biashara
 
Karialoo huwa kuna nguo mpya za bei chini kuliko mituba sijui huwa wanazitoa wapi.
Mikoani ndio shida ya nguo.
Marufuku yoyote huleta ubunifu, rejea marufuku ya rambo. Leo kuna kila aina ya mifuko.
Nakuhakikishia utaona kila aina ya ubunifu.
 
Karialoo huwa kuna nguo mpya za bei chini kuliko mituba sijui huwa wanazitoa wapi.
Mikoani ndio shida ya nguo.
Marufuku yoyote huleta ubunifu, rejea marufuku ya rambo. Leo kuna kila aina ya mifuko.
Nakuhakikishia utaona kila aina ya ubunifu.
Mhhh, umeona kwanza mifuko ya plastiki inavyoongezeka mtaani? Tunakurupuka sana wakati hatuna mbadala wa kinachokatazwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…