Marufuku ya ndege zisizo na rubani ni kitendo cha kujilinda kibiashara cha Marekani kwa kisingizio cha usalama

Marufuku ya ndege zisizo na rubani ni kitendo cha kujilinda kibiashara cha Marekani kwa kisingizio cha usalama

Yoyo Zhou

Senior Member
Joined
Jun 16, 2020
Posts
199
Reaction score
322
VCG111513928943.jpg
Tume ya TEHEMA ya Marekani (FCC) hivi karibuni ilitangaza kuweka ndege zote zisizo na rubani na vipuri vyake vilivyotengenezwa nje ya nchi kwenye orodha ya kudhibitiwa, kwa kisingizio cha “tisho kwa usalama wa taifa”, na kupiga marufuku ununuzi wa aina mpya za ndege zisizo na rubani kutoka nchi za nje. Kitendo hiki kinaonesha wasiwasi wa Marekani katika ushindani wake wa kiteknolojia na China, na kupuuza kwake utaratibu wa kimataifa wa biashara huria.

Mwenyekiti wa FCC Brendan Carr amedai kwamba teknolojia ya ndege zisizo na rubani inaweza kutumiwa na “wahalifu, magaidi, na vikosi vya kigeni vya kiadui.” Wakati huohuo, baadhi ya wabunge wamerudia tuhuma zisizo na msingi kwamba, ndege zisizo na rubani za China zinatishia usalama wa taifa wa Marekani, wakidai kuwa China inaweza kutumia ndege hizo “kuchora ramani kila inchi ya ardhi ya Marekani”. Kauli hizo si mpya. Tangu Wizara ya Ulinzi ya Marekani ilipoweka Shirika la Ndege Zisizo na Rubani la China DJI kwenye orodha yake ya vikwazo mwaka 2017, shutuma kama hizo zimekuwa nyingi, lakini hakuna ushahidi wowote unaoweza kuthibitisha shutuma hizo.

Ukweli ni kwamba, usalama wa ndege zisizo na rubani za China, hasa za DJI, zimethibitishwa na taasisi na wataalam wengi. Zinatumiwa sana katika nyanja mbalimbali za umma duniani kote, zikiwemo kilimo, uokoaji wa moto, ufuatiliaji wa mazingira, na ukaguzi wa miundombinu, na kuleta thamani kubwa ya kijamii na kiuchumi.

Madhumuni halisi ya marufuku yamewekwa wazi katika matamshi ya wanasiasa wa Marekani. Mbunge wa New York kutoka Chama cha Republican Elise Stefanik amesema, marufuku hiyo “itasaidia kuleta uongozi wa ndege zisizo na rubani za Marekani”. Seneta wa Florida Rick Scott ameitaja marufuku hiyo kuwa ni “hatua kubwa katika kuunga mkono wazalishaji wa Marekani”.

Katika miaka ya hivi karibuni, Marekani imekandamiza makampuni ya kiteknolojia ya China mara kwa mara, kuanzia Huawei hadi TikTok, na sasa DJI. Inatumia hatari za “usalama wa taifa” zilizobuniwa kama kisingizio cha ulinzi wa soko na udhibiti wa kiteknolojia. Hivi leo dunia inakabiliwa na changamoto mbalimbali, nchi zote duniani zinapaswa kufanya kazi pamoja, na kuzingatia utaratibu wa biashara wa pande nyingi unaotegemea sharia. Pia zinapaswa kuimarisha mawasiliano na ushirikiano katika teknolojia za kisasa, ikiwa ni pamoja na ndege zisizo na rubani, na kwa pamoja kuhakikisha kwamba teknolojia inatumika kukuza maendeleo ya binadamu wote, badala ya kuweka vizuizi. Kujenga ukuta na vikwazo hatimaye kutaikwamisha Marekani, na ushindani wa haki ndio njia pekee ya kuwa na mustakabali mzuri.
 
Mkuuu ,Lakini Mbon Wao China Wamezuia FACEBOOK , INSTAGRAM , Na Vingine Vingi vya Marekani ...

Kwa hiyo , Kila Mtu Anamaamuzi yake Kwenye Nchi yake
 
Back
Top Bottom