Responded HOJA Marufuku ya Pombe zisizo na Ubora Rwanda: TBS imelala wakati Watanzania wanaweza kuwa wanapata Upofu na Kufa kimya kimya?

Responded HOJA Marufuku ya Pombe zisizo na Ubora Rwanda: TBS imelala wakati Watanzania wanaweza kuwa wanapata Upofu na Kufa kimya kimya?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika

Fascinating

Senior Member
Joined
May 14, 2025
Posts
146
Reaction score
351
Wakuu nadhani wengi mmeiona hiyo clip inayozagaa huko mitandaoni, ikionesha vyombo vya dola vikishirikiana na mamlaka ya kudhibiti vyakula na Dawa nchini Rwanda (FDA) kakita opareshi maalum ya kukamata, kuharibu na kuteketeza Pombe na Vinywaji visivyokuwa na ubora.

Kama kawaida yangu hili suala lilinivutia kidogo, na sikutaka kulitazama kwa Mtazamo wa kidiplomasia zaidi ya usalama wa afya umma maana sikuona kusudi lingine kwa Rwanda kufanya hivyo hususani kipindi hiki ambacho uhusiano wetu umeimarika.

Hili sakataka lilianza tarehe 5 Agosti 2026, ambapo Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Rwanda (Rwanda FDA) ilitangaza marufuku ya aina 52 za pombe. Kwa mtazamo wa haraka, tangazo hilo lilionekana kama taarifa ya kawaida ya kibiashara: waagizaji waliambiwa warejeshe bidhaa, wauzaji waliambiwa wasiuze, na wanywaji waliambiwa waache kunywa.

Lakini ndani ya maneno hayo ya kiudhibiti kulijificha ukweli mgumu kwetu Watanzania: Zaidi ya aina 14 ya pombe zilizopigwa marufuku zilitengenezwa nchini Tanzania, ikiwemo Konyagi ambayo ni pombe maarufu sana hapa kwetu, na kampuni saba tofauti za Kitanzania zikiwemo mbili kubwa za Tanzania Distilleries Limited na Serengeti Breweries.

RWANDA BAN.jpg
Rwanda imefikiaje uamuzi huu?
Rwanda haikufanya hivi kwa bahati mbaya. Wizara ya Afya ya Rwanda iliripoti vifo vya watu zaidi ya 50 tangu mwanzo wa mwaka 2026 kutokana na pombe haramu au zisizo na Ubora, zaidi ya watu 100 wamepata upofu na zaidi ya 500 wamehitaji matibabu ya dharura.

Hii ndio imepelekea kutokea operesheni hii ambapo Polisi wamekamata zaidi ya washukiwa 50, kufunga viwanda 130, na kuteketeza zaidi ya lita 470,000 za ethanol. Hatua hizi zilikuwa za wazi na za haraka, zikionyesha msimamo thabiti wa serikali juu ya afya umma.

DEATH.png


Rwanda haikueleza moja kwa moja tatizo la kila pombe iliyopigwa marufuku, kama ni uchafuzi, methanol, au makosa ya leseni. Lakini ukweli unabaki kuwa bidhaa za Tanzania ziliingia kwenye orodha moja na pombe zilizohusishwa na vifo na upofu, ni ishara ya hatari!

Swali linabaki: kama pombe hizi zimeonekana hatari Rwanda, kwa nini ziliingia sokoni bila kuzuiwa na mamlaka ya Tanzania? Je, TBS ilikuwa wapi?

Ni kweli, marufuku ya nje si ushahidi wa moja kwa moja wa janga la ndani. Huenda baadhi ya brand zilipigwa marufuku ni kwa sababu za formalities tu. Lakini ukimya wa TBS baada ya tangazo la Rwanda ndio tatizo kubwa.

Hakuna taarifa rasmi kwa umma, hakuna matokeo ya maabara, hakuna hatua za tahadhari za ndani. Ukimya wa mdhibiti wakati wa tishio la kiafya ni hatari.

Kilichotokea Rwanda si tukio la kupuuza. Ni dalili ya tatizo la kikanda: Linaloweza kuwa limesababishwa na soko la pombe lisilo na udhibiti madhubuti, bidhaa bandia na matumizi haramu ya ethanol ambavyo vyote vinasafirishwa kwa urahisi ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Marufuku ya Rwanda ilihusisha pia bidhaa kutoka Uganda, Kenya, Burundi, India na Poland. Hii inaonyesha tatizo si la nchi moja bali la mfumo mzima wa usambazaji.

Na kwa hili sisi si wa kuachwa pembeni. Tanzania ni muuzaji mkubwa wa pombe katika ukanda huu. Hali za uzalishaji na upungufu wa udhibiti ulioibua marufuku Rwanda zinaweza pia kuwepo nyumbani.

Bidhaa iliyoonekana hatari kwa mauzo ya nje nchi, haiwezi kuhesabiwa salama kwa matumizi ya ndani.

Tanzania imewahi kushuhudia visa vya watu kufa au kupoteza uoni kutokana na pombe, lakini mara chache vimeripotiwa kwa uwazi. Rwanda imeonyesha mfano wa uwazi: kutangaza idadi ya vifo, wagonjwa, na hatua za polisi. Binafsi sijakutana na takwimu hizi hapa kwetu (Tanzania), wala sijawahi kusikia hatua za tahadhari zimechukuliwa kwa bidhaa zilizopigwa marufuku.

Hii haimanishi kutokutangazwa kwa tatizo kuwa halipo, inaweza kuwa ni Willful Blindness (unaliona tatizo lakini lakini unalivungia), kitu ambacho sitaki kukiamini, lakini huu ukimya ukiendelea nitaamini kuwa tunalifumbia tatizo macho kwasababu hatutaki kulitatua.

TANZANIA.png


Na hapa yataibuka maswali mengi juu uwezo wa TBS kusimamia jukumu hili ambalo hapo mwanzo lilikuwa la TFDA sasa ni TMDA.

Inashangaza sana kuona mtu anayesimamia ubora wa Pikipiki au Kinanda cha Kanisani pia anasimaia ubora wa Vinywaji tunavyokunywa, ni Hatari!

Na hatari ya mdhibiti asiye na nguvu si kwamba anaweza kusababisha madhara moja kwa moja, bali madhara hutokea kimya kimya bila kufuatiliwa. Vifo vya mtu mmoja mmoja, upofu wa taratibu, kulazwa hospitali bila uchunguzi, vyote vinaweza kupuuzwa kwa miaka bila kuchunguzwa.

Wakuu, nisiwamalizie muda wenu na hizi paranoia zangu, pia naomba niweke sawa hapa, suala si kama Konyagi au pombe fulani ni hatari, hilo halijathibitishwa. Swali ni:

Kuna mtu au taasisi Tanzania anayechunguza kwa makini?

TANZANIA LIST.jpg


Rwanda imeonyesha uwazi na hatua kali. Tanzania, kwa sasa, tupo kimya na kesho ijumaa tunarudi tena kwenye viti virefu kuutafuta upofu au kuharakisha vifo.

Wakati kanda inakabiliana na janga la pombe hatari, mdhibiti wetu bado hajafumbua macho. Huu ukimya unaweza kugharimu maisha ya Watanzania wengi bila wao kujua chanzo cha tatizo. Wakuu naomba niwaache tu. Wenyewe bado wanafuatilia Siku 6 sasa 😁

KT Press
Rio Times
Webrwand

Pia soma ~ TBS: Tumewasilisha taarifa Sekretari EAC kuiomba Rwanda kutoa sababu za Kuzuia Vinywaji vya Tanzania
 

Attachments

  • R1.jpg
    R1.jpg
    322.4 KB · Views: 15
  • R2.jpg
    R2.jpg
    267.7 KB · Views: 15
  • R3.jpg
    R3.jpg
    365.8 KB · Views: 19
  • Screenshot_13-8-2026_143147_www.instagram.com.jpeg
    Screenshot_13-8-2026_143147_www.instagram.com.jpeg
    286.6 KB · Views: 16
ivi kwenye hili swala nani hasa wakulaumiwa? mana nijuavyo tbs ni msimamizi kwenye mambo ya ubora natamani kuelimishwa na kulielewa hili zaidi mana tunaweza laumu tbs kumbe kuna mamlaka pia ilipaswa kulipigania hili mana mwisho wasiku sote tutakuwa wahanga kama si wewe basi mmoja wapo wa wanafamilia.
 
ivi kwenye hili swala nani hasa wakulaumiwa? mana nijuavyo tbs ni msimamizi kwenye mambo ya ubora natamani kuelimishwa na kulielewa hili zaidi mana tunaweza laumu tbs kumbe kuna mamlaka pia ilipaswa kulipigania hili mana mwisho wasiku sote tutakuwa wahanga kama si wewe basi mmoja wapo wa wanafamilia.
Mwanzo kulikuwa na TFDA, ndio alikuwa mwenye jukumu, ikavunjwa 2019 na kuondolewa baadhi ya majukumu yake yakaenda TBS hususan hapa kwenye Vyakula na Vinywaji, TFDA ikabaki kuwa TMDA ambayo inajihusisha na Dawa pamoja na Vifaa Tiba tu
 
Vyema kabisa ..Uzi kama huu WALEVI wnaaupita kimya kimya kama wanaaga maiti... Tena mapombe kama konyagi na kvant wamepima wameona ni mataputapu na hayana maana. Na Kuna mataputapu mengine ya tanzania yamezuiwa ..zilizoruhusiwa ni bia zile ambazo kiuhalisia hazina shida.
 
ivi kwenye hili swala nani hasa wakulaumiwa? mana nijuavyo tbs ni msimamizi kwenye mambo ya ubora natamani kuelimishwa na kulielewa hili zaidi mana tunaweza laumu tbs kumbe kuna mamlaka pia ilipaswa kulipigania hili mana mwisho wasiku sote tutakuwa wahanga kama si wewe basi mmoja wapo wa wanafamilia.
tz na dunia uwa zinajali sana vyanzo vya mapato vikubwa na kuidhinisha biashara yake ata kama kuna madhara.iyo kesi ni ngumu sana maana na viongozi wanaokota na wanapata ufadhi kupitia izo sumu, uko mbeleni tutashuhudia bangi pia ikiruhusiwa na inaweza anzishwa kabisa BODI YA BANGI TANZANIA
 
tz na dunia uwa zinajali sana vyanzo vya mapato vikubwa na kuidhinisha biashara yake ata kama kuna madhara.iyo kesi ni ngumu sana maana na viongozi wanaokota na wanapata ufadhi kupitia izo sumu, uko mbeleni tutashuhudia bangi pia ikiruhusiwa na inaweza anzishwa kabisa BODI YA BANGI TANZANIA
Ndugu bangi haina madhara pia ni tiba ya baadhi ya changamoto ila ukizidisha ndo hukuletea maruwe ruwe inetegemea na familia na mifano tunayo mitaani kulinganisha na hili la afya ambayo changamoto zake ni mzigo kwa kila kona si serikali, familia au mtu mooja mmoja
 
Ndugu bangi haina madhara pia ni tiba ya baadhi ya changamoto ila ukizidisha ndo hukuletea maruwe ruwe inetegemea na familia na mifano tunayo mitaani kulinganisha na hili la afya ambayo changamoto zake ni mzigo kwa kila kona si serikali, familia au mtu mooja mmoja
Nafahamu madhara yake ni machache kuliko baadhi ya pombe,nasema hairuhusiwi kwa sababu hawajashuhudia ikiingiza mapato mengi kwa serikali
 
Vyakula na Vipodozi bora visingehamishiwa TBS. Hapa siasa ilizingua sana. TMDA wako makini sana
 
Nadhani kuna haja ya mamlaka za selikali kuja kutolea ufafanuzi kama sio ufuatiliaji wa kina maana kiukweli madhara ya pombe kali kuna mengine tunayaona kwa macho tu unakuta watu wa vi cuca wote wanafanana sura kama ndugu
 
Kama rwanda wameona hazifai na kuzipiga marufuku basi haziwezi kuwa salama hata kwetu pia, kwani sisi na warwanda tuna tofauti gani? Ingekuwa zinatoka huku na kuuzwa rwanda tu na haziuzwi hapa tanganyika ningesema ni hujuma za kiuchumi, ila kwa kuwa wote tunatumia ingekuwa vyema serikali ya tanganyika ikachukulia kwa uzito utafiti walioufanya wenzao na kuona kuwa hazifai na kuchukua hatua, sasa hivi tanganyika imejaa vipombe vingi vya ajabu ajabu, na tunavinywa tukiamini tbs imejiridhisha kuwa ni salama, sasa jirani ametushtua, serikali yetu haitupendi hata kidogo.
 
Bongo watu wapo ofisini wanasubiri tarehe 21 kila mwezi wapate ule ujumbe kutoka NMB,basi hawana habari na mengineyo.

Engine oils tu za magari sokoni nyingi feki za uchochoroni hazina hata hizo 5W30 wala 20W50 ni Korie tupu.
 
Back
Top Bottom