Ruge Opinion
JF-Expert Member
- Mar 22, 2006
- 1,838
- 705
Katika gazeti la Mwananchii la leo (uk.2) kuna taarifa kutoka Makete, Iringa, kuwa watumishi watano wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete wamesimamishwa kazi kwa sababu ya tuhuma ya kujihusisha na maswala ya siasa katika uchaguzi mkuu uliopita. Mkurugenzi Mtendaj wa Halmashauri hiyo anadai kuwa hatua hiyo imechukuliwa "baada ya CCM kulalamika kwamba watu hao walishiriki katika kampeni za uchaguzi, kinyume na kanuni za utumishi wa uma". Swali, hivi hilo linakuwa kosa kwa wanaojihusisha na vyama vyote au wale wanojihusisha na upinzani tu? Maana haiingii akilini kuwa CCM wanaweza kulalamikia wale waliowasaidia katika kampeni. Katika mikoa mingi maofisa wa serikali kuu, serikali za mitaa, polisi, usalama wa taifa, n.k. walishiriki katika kukibeba CCM ikiwemo kutumia raslimali za serikali kama magari katika kampeni za CCM. Tunakumbuka hata ndege ya serikali ilivyotumiwa kumzungusha Salama Kikwete akimkampenia mme wake. Je, hao wote watachukuliwa hatua kama hizo? Ushauri wangu kwa CHADEMA (na vyama vingine vya upinzani ambavyo siyo matawi ya CCM) ni kukusanya ushahidi na kufungua kesi dhidi ya maofisa wa serikali walioshiriki katika kampeni za CCM katika maeneo mbalimbali ili haki itendeke kwa wote. Vile vile hao maofisa wa Makete wasaidiwe katika mapambano yao. Vinginevyo 2015 watu watakuwa na woga.