Che mittoga
JF-Expert Member
- Mar 28, 2017
- 12,658
- 16,205
Mi naona unaendelea kuniuliza maswali ambayo mengine nimesha kufafanulia vizuri huko nyuma.Mkuu labda nikuulize neno shetani lina maana ya Malaika anayeasi au lina maana gani? Kwa sababu Lucifer alipoasi ndipo akaitwa hivyo,kwanini aliitwa hivyo?
Na je,kundi la malaika waliyoamua kumfuata Lucifer ndiyo hadi leo ni hao hao tu hakuna tena malaika wanao ongezeka kwa kumfuata Lucifer na kumuasi Mungu?
Mkuu tatizo sio kuamini bali ni wapi umekipata hicho unacho kiamini? na ndiyo maana nilikuomba vifungu kwa kwenye biblia.
Maswali mengine kama ya nani Malaika na nani Shetani, hata wewe umeshafafanua kwa jinsi unavyoelewa.
Naona kama tunatoka nje ya mada husika inayosema;-
Je Majini na Maluhani yanatolewaje ndani ya mtu ?
Napenda kwa sasa tujikite kwenye mada husika. Ili tuendelee na mtiririko wa mawazo.
Kama una wazo jipya unaweza kutueleza.