Marumo Gallants walipowasili asubui hii walikataa basi waliloandaliwa na wenyeji wao

Najua reply zangu unazi ignore ila nitakuuliza tena swali ambalo nadhani nimewahi kukuuliza siku za nyuma. Unadhani klabu unayoishabikia ni ya watakatifu?

Nitaongeza maswali ya ziada, unadhani wewe ndiyo una akili kuliko GSM, wamiliki wa Yanga ambao hawajatoa tamko lolote la lawama jinsi uchunguzi ulivyofanyika? Unadhani wewe una akili kuzidi kamati ya nidhamu ya CAF ambayo inahusisha wataaalamu wenye uzoefu wa mambo haya kutoka nchi tofauti tofauti?
 
Wazee wa kujitoa fahamu.

Utopolo bhana.

Umepata na likes 8,mazuzu yanasapotiana ujinga.
Huo ndio ukweli mkuu,walishatafuta mtu wao wa kuwaletea usafiri,faini Yao iko pale pale na ole wao wafungwee magoli mengi makolo dizain yako mtateseka sanaaaaaa[emoji23][emoji23]
 
Yanga kitu pekee inaweza kujifunza kwa Simba ni uchawi tu.
 

Kasome post namba 2 ina majibu yako kuhusu hoja yako ya utakatifu naona una dandia gari kwa mbele.

Umeniuliza mimi nina akili kuliko GSM kwani unatumia kipimo gani kupima akili? Kwani GSM yeye sio mtu? Kashushwa mbinguni? Usiwe na akili mgando hata wewe unaweza kuwa na akili kuliko GSM, hakuna binadamu aliyekamilika.

Kutotoa tamko, inategemea na walivyochukulia maamuzi (uzito) kwasasa uongozi + wachezaji + benchi la ufundi focus yao ipo kwenye kufuzu nusu fainali pekee na hiyo faini wameona ni ndogo. Embu fikiria kama CAF wangetoa maamuzi ya Yanga ku disqualify kucheza nusu fainali kutokana na hayo matukio. Halafu uone kama uongozi usingekata rufaa juu ya tukio hilo.

Nakuuliza swali, wale washabiki wa Wydad waliosababisha mechi isimame kwa kuwasha fataki kwa Mkapa, je hao watalamu unaowasifia wanaounda kamati ya nidhamu, iliichukulia hatua gani timu ya Wydad?
 
Hayo maswali yako kwenye post #2 na mimi nilikujibu kwenye uzi mwingine ya mada hii hii nikakukumbusha kuwa siku ya tukio nilikwambia hamkutoa ulinzi muda wote basi lao lilipokuwa limepaki ndiyo maana CAF conclusion yao ikawa kwamba "mliwajibika" kwa matukio yale (ama mliyafanya nyie au Wanaija walijifanyia ila kuwasakizia). Kama sikosei kioo kilivunjwa, sasa mlinzi angekuwepo ni wazi angesikia na angeweza kulitolea majibu hilo tukio.

Kwenye masuala ya kitaasisi "kuwajibika" haimaanishi kuwa wewe ndiye uliyehukumiwa kufanya tukio fulani ila kuna uzembe ambao umehusika kuwezesha au umeshindwa kutoa majibu ya kutosha kujitenga na uhalifu husika.

Nakumbuka baadhi yenu mkawa mnatoa hoja kwamba nyie siyo kampuni ya ulinzi, hapo nikajua naongea na watu wa aina gani.
 
Wydad wamepigwa sana faini kwenye matukio ya kuwasha moto na baada ya tukio lile la Mkapa walipewa onyo kali ndiyo maana kwenye mechi ya marudio hawakuyafanya hayo mambo. Yanga pia wamewahi kupigwa faini kwa matukio ya kuwasha moto.

Tukio la Mkapa kwenye mechi ya Simba/Wydad kwa kiasi kikubwa ni uzembe wetu sisi wenyewe. Kuna uzi nilihoji, iliwezekanaje wale mashabiki walipita na mafataki yale JKNIA na pia pale kwa Mkapa tukijua wazi wana tabia hizi na ingeweza kuigharimu Simba mchezoni au kuhatarisha usalama wa mashabiki? Nadhani CAF walizingatia uzembe wa upande wa pili pia ukizingatia haya matukio zaidi yanafanywaga na mashabiki wa timu mwenyeji.
 
Kuhusu "akili", inahitaji kuwa mtu special sana kusema kwa kujiamini kabisa kuwa una akili za masuala ya mpira, uchunguzi na utawala kuwazidi CAF, TFF, na taasisi yako pendwa ya Yanga/GSM.

Milioni 80 siyo pesa ndogo kabisa kwa standard yoyote ile hapa Tanzania au huko duniani hasa kama ikiwa imetokana na matukio ambayo yangeweza kuepukika. Msijidanganye mkalinganisha na zawadi mnayotegemea kupata huko CAF ukaona ni chenchi tu. Hiyo pesa ni zaidi ya nusu ya mapato ya timu katika dabi kwa Mpaka ikiwa full house.

La mwisho, Yanga haijapigwa faini kwa wizi uliotokea maana huo ndiyo hasa ungehitaji uchunguzi unaoulilia maana ingehitaji ushahidi wa uwepo wa hizo pesa na mambo kama hayo. Mengine yalikuwa wazi, kama harufu waliingia kwenye basi wakaisikia, kioo wakaona kimevunjwa, kama fataki waliziona zikipigwa karibu kabisa ya camera.
 
Jukumu la kutoa ulinzi kwa wageni ni la Yanga au ni la TFF?
 
Una hoja za kitoto sana eti wanepitaje na Airport what if kama hayo mafataki wamenunua Dar so ulitaka Simba wawakague mizigo yao?
 
Jukumu la kutoa ulinzi kwa wageni ni la Yanga au ni la TFF?View attachment 2616404
Nilikuwa najua utakuja kuitaja TFF. Ni kweli TFF ndiyo wenye mamlaka ya kuandaa na kusimamia mechi za kimataifa ndiyo maana hata ile barua ya CAF wameiaddress kwa TFF na siyo Yanga moja kwa moja maana TFF ndiyo mwanachama wao na walikuwa wanaitaja Yanga kama "klabu yako" wakiiambia TFF. Ukija sasa kwenye uhalisia, TFF anashirikiana na timu husika kuhakikisha majukumu yote ya mechi yako sawa, kuanzia usafiri, malazi, ulinzi, nk. Mwisho wa siku kasoro zozote inawajibika TFF kwa niaba ya klabu, na klabu inawajibika kwa TFF kwa kasoro hizo hizo zilizojitokeza.

Huo ndiyo mtazamo na ufahamu wangu, niko tayari kukosolewa.
 
Sasa kwanini kutokuwepo kwa polisi ulipeleka lawama moja kwa moja kwa Yanga kama ulikuwa unalijua hilo?
 
Una hoja za kitoto sana eti wanepitaje na Airport what if kama hayo mafataki wamenunua Dar so ulitaka Simba wawakague mizigo yao?
Ni kweli ila nilikuwa najaribu kufupisha maelezo yangu. Sidhani kama fataki walizotumia zinapatikana Dar, ni wazi zile walikuja nazo labda walipitisha kwenye mizigo ya wachezaji.

Moja ya mkakati wa mchezo ule kwa upande wa Simba ungekuwa kuhakikisha mashabiki wa Wydad hawavurugi mchezo kwa namna ile kwa hiyo hata ukaguzi tu wa kawaida getini kwa Mkapa hasa kwa kundi lao ungepangwa, ungetosha kuepuka hilo. Nadhani hakuna aliyelitegemea hilo kutokea maana mashabiki wa Raja walivyokuja hawakuwa na fataki ila siku nyingine waarabu wowote wakija naamini watakaguliwa vizuri tu.
 
Sasa kwanini kutokuwepo kwa polisi ulipeleka lawama moja kwa moja kwa Yanga kama ulikuwa unalijua hilo?
Yanga kama timu mwenyeji anahusika moja kwa moja kwa kila kinachotokea kwa timu inayokuja kucheza nayo, CAF kuiwajibisha TFF ni suala tu la kiutendaji maana TFF ndiyo mwanachama wa CAF na siyo Yanga.

Kiuhalisia timu mwenyeji haiiachii tu chama chake cha soka kufanya maandalizi, wanahusika katika kila jambo sasa kama ulinzi ulipelea, kuna namna wanawajibika kwa hilo.
 
Una kichaa wewe, Yanga ijifunze nini kwa Makolo? Labda Muifundishe Yanga Uchawi na Ulozi kama ule mliozindika pale S.Africa na kuambulia adhabu
na nyie mmeambulia adhabu, tena ya fedha 82M
 
WANANCHIIIIIII LEO NI SIKU AMBAYO TUNAENDA KUUONESHA ULIMWENGU KWAMBA YANGA INA UKUBWA KIASI GANI.MAKOLO
WAMEJARIBU KUIKUZA MARUMO KWA KILA NAMNA ILA LEO TUTAENDA KUWAONESHA YANGA NI NANI.
EWE MWANANCHI TEMBEA KIFUA MBELE KWANI LEO NDIO TUNAENDA KUINGIA FAINALI RASMI.
LEO MADUNDUKA YATALILIA CHOONI.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…