SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Najua reply zangu unazi ignore ila nitakuuliza tena swali ambalo nadhani nimewahi kukuuliza siku za nyuma. Unadhani klabu unayoishabikia ni ya watakatifu?Kwa ile clip walionesha Rivers united s, hao unaowaita ni mashahidi ( makamisaa) hawakuwepo wakati tukio linafanyika bali viongozi wa Rivers united ndio wakawafuata hao maofisa kutoka CAF na kutoa taarifa na wao wakaenda ndani gari ili kuthibitisha.
Hizi tuhuma zimechukuliwa hatua ya maamuzi lakini napata wasiwasi kama kuna vitu vya msingi vimefanyika.
Gari lina cctv camera, kwanini wasiangalie aliyefanya hilo tukio na akakamatwa na kufungwa kwa kesi ya kutaka kuua watu kwa sumu? Kisha klabu nayo iadhibiwe pia kama kweli ni shabiki wa Yanga.
Kitu kingine kinachonishangaza ni kwamba inadaiwa gari limewekwa sumu ndani lakini watu wanaingia mara mbili mbili pasipo kuvaa barakoa. Kweli! Sumu ipo kwenye gari halafu hata hakuna anayechukua tahadhari. Sumu hiyo
Dereva wa hilo bus je alihojiwa? Na kwanini gari lipaki sehemu pasipo kufunga milango na madirisha? Dereva kachukuliwa hatua gani?
Namalizia kusema soka la Africa ni ngumu kupiga hatua kama uwezo wa kufiiria kichwani upo hivi.
Nitaongeza maswali ya ziada, unadhani wewe ndiyo una akili kuliko GSM, wamiliki wa Yanga ambao hawajatoa tamko lolote la lawama jinsi uchunguzi ulivyofanyika? Unadhani wewe una akili kuzidi kamati ya nidhamu ya CAF ambayo inahusisha wataaalamu wenye uzoefu wa mambo haya kutoka nchi tofauti tofauti?