Hello Marvel Mates kuna jamaa alikua anaisema marvel bila kua na ufaham wa how marvel operates, Nimeona nilete comment yangu hapa ili wasiojua wajue pia[emoji3577]
Jamaaa katupiga kamba balaa sema bahati yake mwandishi hayupo humu ngoja nimuache. Ila kwa kuweka mambo sawa..
[emoji3581]Zack Snyder sio mwenye sauti kuu DC ni kiongozi kwenye upande wa creativity yaani DCEU. Warner bros ndio wenye sauti na ndio wanasababisha kufeli kwa DC kwakua hawampi full control ya creativity Zack Snyder. Na muvi za DC hua haziigizwi usiku bali ni tone Color tu walio ichagua DC ili kuweka radha tofauti.
[emoji3581] Umempamba Stan Lee lakini ukae ukijua yeye hahusiki kwenye creativity ndio maana hua credited kama Executive producer/Creator
Creativity team ya Marvel inaundwa na Kevin Feige, Victoria Alonso,Lois despacito,Stephen Broussard, Nat Moore,Jonathan Schwartz,Trinh Tran,Bran Winderbaum na kipindi cha nyuma hasa phase 2 alikuwepo Josh whedon
[emoji3581]Mpango mzima wa muvi 22 kwa miaka kumi zenye storyline moja umeundwa na vichwa vitatu ambavyo ni Avi Arad, Sami Raim na Kevin Feige ambae ni Boss wa Marvel studios.
[emoji3581] Paragraph yako ya mwiso ndio umeongea uongo mkubwa sana...Looh hadi aibu.
[emoji117] Marvel ilikua haina hela kabisa miaka ya 90 huko so ilikua inauza baadhi ya characters wake ili kuendesha Kampuni. Mfano iliuza Spiderman na Venom kwa kampuni ya Sony, ikauza XMen na Fantastic four kwa 21th Fox yaani marvel inapata kitu kama asilimia 10% tu kwenye mauzo ya hao characters.
Mwaka 1999 Marvel ilitoa muvi ya Blade hii muvi iliuza kiasi chake na hii ndio pesa zilizopatikana ziliwezesha kuanzisha marvel studio mwaka 2007. Kama kawaida Disney ni wazee wa kunusa hela tu kama walivyoinusa kampuni ya Pixar animation wakaichukua hivyo basi mwaka 2009/10 Disney rasmi iliinunua Marvel studios so Marvel character wote wapo chini ya Disney. Hivyo Boss wa Marvel anapokea naelekezo kutoka kwa CEO wa Disney ambae ni Bob Igler. Disney wenyewe wanachohusika kwenye Marvel studio movies wanakua kama wasambazaji (Distributor)
Hivyo basi Marvel studios ni stand alone studio inayojitengenezea muvi zake hata Bob Igler hahusiki kwenye creativity yeye anapewa taarifa tu kama boss kama kuna promotion na pesa zinatakiwa yeye ndio ana issue
[emoji117]Mwaka 2019 rasmi kampuni ya Disney ilinunua kampuni ya 20th Fox na 21th Fox hii ina maana character wa marvel waliopo Fox kaa vile Deadpool,Xmen na Fantastic four wote wapo marvel/Disney. Sio hivyo tu Hata James Cameron yupo chini ya Disney maana muvi zake zote za Titanic na avatar zote zilikua fox sasa zinamilikiwa na Disney.
[emoji3581] WanaBros wao ni wamiliki na wasambazaji wa DC movies