Thanks for recommending me to Canadian lad, nimenfuatilia sana video zake niseme tu he's the best. Natumaini kama nami ningepata tools za kutosha kama yeye ningeweza kufanya kitu. Ila kuangalia muvi kwa 0.25speed yataka moyo hongera kwake...Kwa bongo sidhani kama kunawasomaji wa comics wengi. But I'm really impressed and motivated to do such kind of thing [emoji7]
Niliangalia video hiyo ya Trailer la Multiverse of madness, kuna Sehemu wakati Christine Palmer anafunga ndoa anasema kwamba christine atakua ndio anaigiza character ya Clea, ambae ni mke wa Stephen strange kwenye comics...Mimi nakataa. Na nitatoa factors/theory zangu Kama ifuatavyo.
✓Kipindi Drew Goddard anatengeneza Series ya Daredevil alitaka kutumia character ya Night Nurse kutoka kwenye comics ambapo Huyu ni nesi/manesi anayehudumia Superhero waliopata majeraha kama vile Punisher,Luke Cage,Iron fist, Daredevil nk. Lakini Drew Goddard aligundua kwamba character hiyo inampango wa kutumiwa na MCU miaka ya baadae. (Ndio alikuja kutumiwa kwenye muvi ya Doctor strange akiitwa Christine Palmer)
Drew alibadirisha character ya night Nurse na kutumia jina la Claire Temple, waliotazama series za Daredevil, Defenders,Luke Cage walimuona.
So mpaka hapo tumejua kwamba christen Palmer mpenzi wa Stephen strange kwenye comics anafahamika kana night nurse....
Clea....
Clea ni mtoto wa Umar (kama sijakosea) mpwa wa Dormamu pia, Anaishi Dark Dimension huyu walikutana na strange wakapendana japo kuna uadui lati yao wakafunga ndoa, waliungana na kua wanapambana pamoja dhidi ya mystic beings.
#1: Sasa sidhani kama itakua sahihi kama MCU wataruhusu Character ya Night Nurse na Clea ichezwe na mtu Mmoja, yaani watuaminishe kua night nurse ndio clea sidhani kama watakua wamefanya vyema hasa kwetu tunaofatilia comics, Marvel studios creative team wapo makini sana sidhani kama wataweza kuruhusu mkanganyiko huu.
#2: Lakini pia sioni umuhimu wa kumleta clea kwa sasa maana tayari washamleta American Chavez powerful kama clea au zaidi yake... kwenye muvi strange atakua mentor wa American Chavez hivyo tunategemea Strange kurithiwa nae maana naona MCU wapo serious kwa swala la gender swapping kwa Superheroes.....Kama asingekuwepo american Chavez basi ningekubali theory ya kumfanya Christine Palmer kua clea.
Ila haya ni mawazo yangu tu.. naweza kua sahihi au sipo sahihi, kikubwa tusubiri may 6 tutapata majibu.