niaje wakuu, natumai mpo pouwa. mimi ninataka ku-share some nuggets of gold katika maswala ya film, ingawa sio mcu, ila madirector au events, na actors ni favourite kutoka mcu.
1. The gray man
Aisee, hii kitu iko pouwa. kama mliangalia terminal list mkaipenda, basi hii utaipenda pia. ina vibe la "john wick, nobody na extraction" kwa pamoja. Directors ni The Russo bros(hakuna mcu bila hawa jamaa), wameitendea vyema movie, pia yupo "cap A" katika nafasi ya roho mbaya, kwa maoni yangu kaitendea vyema sana, Pia kuna ryan gosling, mwamba alipotea sana, kafanya vyema sana, hopefully ndo itakuwa time ya yeye kurudi kwenye spotling.
imeshatoka, imeandalia na netflix.
2. The Woman King
Bila shaka wote tunawafahamu "Dora miraje", wale walinzi wa familia ya kifalme ya Wakanda, pia wanashika nafasi ya ujenerali katika nchi ya wakanda(kwenye what if tuliona mama yake black panther ni general anayeongoza jeshi la waknda, pia alitoka katika kikosi cha Dora miraje){Pia Black ponther ali-freeze alivyomuona lupita nyongo ambae ni covert operative/spy kutoka kikosi cha dora miraje, labda tungekuja kuona black panther akimuoa huyo dora miraje.[Until Valhalla, Chadwick.]}.
Sasa, tushawahi kufikiria labda Dora miraje ni "Inspiration" kutoka historia ya kweli? Kwamba kuna kikundi cha kijeshi cha wanawake watupu kilichowahi kuwepo hapa africa? Na kilikuwa vyema katika medani za vita?
Woman King inatupa muono kidogo wa kikosi cha walinzi wanawake wa ufamle wa Dahomey(Dahomey women warriors), waliokuwa na jukumu la kulinda familia ya kifamle na ufamle wa dahomey kwa ujumla. imekaa pouwa sana{trailers}, pia humo ndani kuna fight scenes{kutoka kwenye trailer} zimekaa ki-dora miraje sana(tunajua kutokana na mcu, dora miraje wako pouwa sana, si waoga, na wanajua wakifanyacho, well, bucky, cap A mpya na yule Cap A wa muda kutoka falcon and winter soldier, wanaifahamu shughuli yao ipasavyo). Dahomey inapatika huko Benin.
Waigizaji, mimi nimemuona na kumfahamu mmoja tu, yule mother black wa kwenye Suicide squad. anatoa shoo ya nguvu.
bado ni trailer tu, ila inatoka mwezi wa 9 au 10. kwa maoni yangu, ni worth the watch.