Marwa kutoka Kenya atumia miezi 3 kutembelea nchi 23 barani Ulaya

Marwa kutoka Kenya atumia miezi 3 kutembelea nchi 23 barani Ulaya

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869
Anatuletea habari za ndani kabisa jinsi bara la Ulaya lilivyo 2022 na viza ya Schengen


Msafiri jasiri Marwa toka Kuria Kenya anatuonesha jinsi bara la ulaya lilivyo na mambo mengi ambayo ni shule kwa nchi za bara Afrika kuhusu umuhimu wa mifumo isiyotetereka na endelevu.

Huwezi kuona tofauti ya masikini na tajiri kwa kuangalia aina ya mavazi, magari n.k

Mifumo yote inafanya kazi kwa ufanisi kuanzia miundo-mbinu, usafiri wa reli, mabasi na ndege

Elimu ya msingi ni bure kuanzia shule ya msingi mpaka upili

Mipango miji na vijiji yote imekaa sawa .... usafiri wa reli ni muhimu hivyo unaona mitandao ya reli kila sehemu ndani ya miji pamoja na kuunganisha mikoa bila kusahau nchi jirani ..

Bara ulaya linavyohifadhi historia mbalimbali kupitia majengo-kale, maktaba, chakula,

Source : iam_marwa

What is Schengen?

Schengen refers to the EU passport-free zone that covers most of the European countries. It’s the largest free travel area in the world.

Maeneo ya Pangani, Bagamoyo, Kilwa, Vilimani vya Miamba Mwanza, Mikindani Mtwara n.k vinaweza kuwa Santorini ya Ugiriki ikiwa tutawekeza ktk maeneo hayo ya Tanzania

Santorini Greece known since ancient times as Thira, is one of the most famous islands in the world. The fact that you can sit in front of the caldera
 
Paris, France

MIFUMO BORA YA MIUNDO MBINU ULAYA, NI MFANO WA KUIGWA


Mifumo ya usafiri ya Ufaransa inatupa picha jinsi ambavyo wamewekeza kurahisisha usafiri mijini, kuunganisha mikoa na nchi za bara la ulaya, tofauti na Afrika ambapo mipaka ya nchi imewekewa vikwazo siyo vya usafiri bali hata biashara baina ya nchi mfano EAC, SADC, ECOWAS n.k

Source : iam_marwa
 
Vatican City
Maria msafiri jasiri akitupitisha ktk mitaa na vichochoro vya taifa hili dogo maarufu duniani.


Source : iam_marwa
 
Rome, Italy
Marwa msafiri jasiri afanya ziara jijini Rome na kutuonesha jiji lilivyo jengwa kwa mpangilio na kutunza historia yake.



Source : iam_marwa
 
sijui ni mimi ndio nimeshindwa kuelewa au ni google translate ndio imesababisha kutoelewa
 
sijui ni mimi ndio nimeshindwa kuelewa au ni google translate ndio imesababisha kutoelewa

Unachohitaji ni bundle la kutizama video za safari zake ktk nchi 23 na utayaona mazingira yote hivyo kupata ufahamu nchi hizo zilivyo maana ni dunia nyingine, kujua lugha haina ulazima ila macho yako kwa kuziangalia video hizi chache utaweza kuona utofauti.
 
Unachohitaji ni bundle la kutizama video za safari zake ktk nchi 23 na utayaona mazingira yote hivyo kupata ufahamu nchi hizo zilivyo maana ni dunia nyingine, kujua lugha haina ulazima ila macho yako kwa kuziangalia video hizi chache utaweza kuona utofauti.
aise,kwahiyo wewe umeangalia hizo video za hivyo zote! hongera mkuu
 
aise,kwahiyo wewe umeangalia hizo video za hivyo zote! hongera mkuu

Elimu ni gharama, inabidi serikali za kiAfrika kama yetu ya Tanzania zipunguze gharama za intaneti .

Wenzetu marekani ya kaskazini, ulaya, Japan, Republic of Korea n.k intaneti ni huduma muhimu imewekwa fungu moja na huduma za msingi kama maji, umeme, gesi kupasha moto nyumba, huduma za afya, makaazi na chakula.

Hawa jamaa wanaamini information is power hivyo kuwanyima baadhi ya raia uwezo wa kutumia intaneti ni mbinyo wa haki za kibinadamu kwani kama huku kwetu ni vigogo pekee ndiyo wanapewa bundle tena za buree huku wakiwabinya raia wa kawaida wasipate uhuru wa habari na shule kupitia intaneti.

Tanzania imeenda mbali zaidi mbali ya kukaba huduma za intaneti kiaina imebana waTanzania wa kawaida kusoma somo la lugha za kigeni ikiwemo lugha ya kiingereza ili wachache tu waweze kuimanya lugha hiyo ya kigeni. Hii haina tofauti na karne nyingi zilizopita wakati watawala walichoma moto vitabu na maktaba kwa hofu raia wa kawaida watainuka katika ufahamu wa mambo mbalimbali.

Canadian lawmakers declared that access to an inexpensive, dependable, and fast Internet connection is a basic right for all Canadian citizens no matter where they live. This announcement from the Canadian Radio-television and Telecommunications Commission (CRTC) came as welcomed news to the 18% of Canadians who live beyond the great technological divide in some of the most remote areas of the country. Source : The Canadian Government Says High-Speed Internet is Essential..
 
Historia ya kuchoma moto vitabu dunia ya kale ipo hadi leo ila watawala wa sasa wanatumia njia ya kufanya huduma za intaneti ziwe gharama kubwa hivyo kuwanyima nafasi idadi kubwa ya raia kujifunza na kusoma

https://www.smithsonianmag.com › ...
A Brief History of Book Burning, From the Printing Press to Internet ...

31 Aug 2017 — According to Knuth, the motives behind book burning changed after the printing press helped bring about the Enlightenment era ....

Hitler Youth burning books.jpg
Hitler Youth members burn books. Photograph dated 1938


......What changed everything was the printing press, invented by Johannes Gutenberg in 1440. Not only were there suddenly far more books—there was also more knowledge. “With the printing press you had the huge rise of literacy and modern science and all these things,” Knuth says. “And some people in authoritarian regimes, in a way they want to turn back the effects of the printing press.” .....
 
Back
Top Bottom