Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mwenyekiti wa UWT Taifa, Mary Pius Chatanda, amesema wanawake nchini wanamshukuru kwa dhati Rais Samia kwa juhudi zake kubwa katika kuboresha huduma za afya kupitia ujenzi wa Zahanati, Vituo vya afya, Hospitali za Wilaya, Mikoa na Kanda.
Amesema kuwa kabla ya maboresho hayo, wanawake – hususan wajawazito – walikumbana na changamoto nyingi ikiwemo kutembea umbali mrefu kutafuta huduma za kujifungua, lakini sasa adha hizo zimepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na uwekezaji huo muhimu wa serikali.
"Wanawake Tanzania wanamshukuru sana Mh. Rais Samia Suluhu Hassan kwa ujenzi wa Zahanati , vituo vya afya, hospital za wilaya, mikoa , Kanda. Na wanawake walikuwa walipata tabu sawa wanapokuwa wajawazito, waliokuwa wakitaka kujifungua, walikuwa wakitembea mwendo mrefu lakini amewapunguzia adha wanawake"