GE2025 Mary Chatanda (UWT) awataka Wanawake kujitokeza kwa wingi kushiriki Uchaguzi 2025

GE2025 Mary Chatanda (UWT) awataka Wanawake kujitokeza kwa wingi kushiriki Uchaguzi 2025

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
459
Reaction score
644
Mwenyekiti wa UWT Taifa Mary Pius Chatanda (MCC) tarehe 27 Juni, 2025 amewataka Wanawake wote Nchini Tanzania kuitumia fursa hii ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 kujitokeza Kwa wingi kwenda kugombea nafasi mbalimbali za uongozi udiwani, Ubunge kwenye majimbo na Viti Maalum, amesema Chama Cha Mapinduzi zoezi la kuchukua Fomu linaanza kesho Tarehe 28 Juni, 2025 Wanachama wenye sifa wote wanayohaki ya kujitokeza kugombea hususa kundi la Wanawake.

 
Mimi nina hakika CCM hatuwezi kuhalalisha uchaguzi Mkuu kwa kutumia CHAUMA na ACT Wazalendo.

Jumuiya za ndani ya nchi na za kimataifa zinakitambua CHADEMA kuwa ndiyo Chama kikuu Cha upinzani.

Jumuiya hizo pia zinatambua kuwa taratibu za uchaguzi haziko sawa.

Ikumbukwe kuwa Magufuli,pamoja na ubabe wake,lakini alihakikisha Chadema kinashiriki uchaguzi Mkuu.Hii ni kwa sababu katika nchi yoyote jambo linaloangaliwa kwa unzito mkubwa na wananchi na Jumuiya za kimataifa ni uchaguzi Mkuu.

Tujiulize kama nchi tunaweza kumudu uchaguzi utakaogharimu fedha yote halafu ustambuliwe na Watanzania walio wengi na Jumuiya ya kimataifa.Ni sawa na kupanda shamba kubwa na usivune chochote.

Madhara yake ni kutengwa na Jumuiya ya kimataifa,kukosa uwekezaji,kukosa misaada na mikopo.Hatuwezi kumudu kujiendesha bila misaada au mikopo.
Mapato yetu bado yako chini mno.
 
Back
Top Bottom